Amani ikiendelea kuwepo Nchini tusikimbize tena Mwenge, una gharama kubwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,138
157,076
Huu ni mwaka wa kwanza tangu tumepata Uhuru kushuhudia Mwenge ukiwa umezimwa na kufungiwa huko unakokaa.

Rais wetu mwema Sana H. E. John Pombe Magufuli aliamuru tusikimbize mwenge ili tupambane na adui aliye washinda wengi CoronaVirus COVID-19. Hakika brother COVID-19 tulimgaragaza mapema tofauti na matarajio ya nchi hisani za kimagaribi walivyotarajia.

Miongoni mwa sababu za kukimbiza mwenge Ni kwamba mwenge unaleta amani nchini. Hakika taifa letu limekuwa kitovu na kisiwa Cha amani kwa miongo mingi.

Swali langu kwenu wana jamii, je Kuna umuhimu wowote wa kuendelea na mbio za mwenge Kama tu mwaka huu hatuujakimbiza na hamna uasi, Vita wala fujo zilizotokea?

Isaya 50:11
 
Hawa jamaa
IMG-20200820-WA0043.jpg
 
Mwenge una umuhim sana ila mwaka huu hatuja utembeza kwa7bu maalum kuwa kulikuwa na janga la corona kwaiyo mwakani tuendelee kama kawaida
Kwa mazingira ya sasa,mwenge una hasara kuliko faida!Siku hizi mwenge imekuwa kama sehemu ya anasa,pombe na ngono ndio vinaongoza kwwnye shughuli za mwenge!Mimba zisizotarajiwa na magonjwa hupatikana kwa wingi kwenye mkesha wa mwenge!Ukiuliza wananchi hata maudhui ya mwenge wengi hawajui,sana utakuta wanapanga namna ya kulewa siku hiyo!
 
Palipo na chuki ulete upendo,kazi ya mwenge,giza lete nuru,vitu vyote hasi viwe chanya
 
Mwenge hauna faida yeyeto kiuchumi Wala kisiasa,zama hizi labda tu Kama unatumika kutakatisia Kodi zetu toka kwa wajanja wachache
 
Back
Top Bottom