PreGE2025 Amani Golugwa: Kuhusu kushiriki zoezi la kujiandikisha uchaguzi iulizwe Tume, hawakujibu barua yetu

PreGE2025 Amani Golugwa: Kuhusu kushiriki zoezi la kujiandikisha uchaguzi iulizwe Tume, hawakujibu barua yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,


CHADEMA kupitia Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Amani Golugwa wamegusia kuhusu zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa kwenye daftari la mpiga kura ambapo wanasema waliletewa barua na Tume watoe maoni kwenye kanuni kadhaa ambazo walikuwa wamepelekewa na waliijibu tume kwa barua kuhusiana na mabadiliko wanayoyataka ikiwemo suala la uandikishaji wa wapiga kura.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amewaambia waandishi wa habari wawafate tume na kuwaambia barua walioandikiwa Disemba 29, 2024, je majibu yake wamefanyia kazi? Maana haikujibiwa. Hivyo waulizwe hayo majibu kwasababu walijieleza kwa kirefu.

Mkutano huu na waandishi wa habari umefanyika katika ofisi ya Makao Makuu ya Chama Mikocheni, Dar.
 
Back
Top Bottom