Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa, amekemea vikali madai yanayosema viongozi wa chama hicho, akiwemo yeye na Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, wanafaidika na kufungwa kwa Mwenyekiti wao, Tundu Lissu. Akizungumza nje ya Mahakama baada ya kesi kumalizika, Golugwa amesema ni vyema Lissu akaachiwa ili kuondoa shaka na hasara yoyote kwa chama na viongozi wake.