Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,840
Kipande hiki cha muziki kilitengenezwa na mmoja kati ya wakali wa muziki wa zamani wa Ujerumani.
Huyu bwana alitambulika kama Wolfgang Amadeus Mozart, kipande hiko cha muziki kikiwa ni Serenade No. 13
Mozart alizaliwa tarehe 27 Januari 1756 na akafarika tarehe 5 Desemba 1791. Gwiji huyu amepata heshima sana enzi zake hata hivi sasa nchini ujerumani kwa kuwa kazi zake zimeendelea kuenziwa na watu wengi nchini humo.
Nchini Tanzania tumewahi kupata mtu mwenye kipaji cha pekee. Midundo na ufundi wa Mzee Morris Nyunyusa mlemavu wa macho aliyekuwa na kipaji cha ajabu cha kupiga ngoma 17 kwa wakati mmoja, na midundo hii ilihusisha ngoma zote hizi. Tatizo ni kuwa hatuheshimu uwezo wa watu wetu na kuwatangaza, ndio sababu hata baadhi ya midundo tunayotumia kwenye vipindi vyetu ni midundo iliyotengenezwa na watu wa nje
Mzee Moris aliwahi kupata fursa nyingi ikiwa ni pamoja na kutembea nchi mbalimbali kuuonyesha uwezo wake wa kupiga ngma kwa wageni. Kama maonyesho japan ambayo yaliimbwa na Mbaraka Mwinshehe