Mkuu
Kigarama,sidhani kama tatizo letu kubwa ni lugha.
Mbona Kiswahili kinaeleweka kwa watanzania wengi,lakini bado hali ni mbaya kwenye shule zetu za msingi?
Nadhani kuna tatizo kubwa kwenye:
1/MITAALA YA KUFUNDISHIA.
Mitaala yetu ya kufundishia si relevant na mazingira halisi ya watanzania tunayo ishi.
Mwanafunzi anasoma maeneo ya vijijini ambayo kazi kuu ni kilimo na ufugaji;badala ya mwanafunzi kuwa trained ku acquire skills za kuweza kuendeleza maeneo haya,mwanafunzi anafundishwa vitu irrelevant kabisa.
Hii hupelekea mwanafunzi kupoteza mori wa kujisomea na kupelekea kufeli.
2/MASLAHI DUNI YA WALIMU.
Hii imepelekea kuwa na mgomo baridi wa walimu,baada ya kuona wanapuuzwa na serikali yao.
Kwa mazingira haya kufeli ni inevitable.
3/ALAMA ZA KUFAULU ILI KUJIUNGA NA UALIMU.
Inasikitisha sana kuwa ualimu umegeuka kuwa taaluma ya wale "walio feli"!
Kwa mfano,wale walio maliza form four na kupata div. 1V,hivyo kushindwa kuendelea A Level,huenda ualimu wa shule za msingi.
Mambo ni yale yale kwa diploma na hata degree za ualimu.
Hii inachangiwa na MASLAHI DUNI ya walimu,hivyo mtu akipata marks za juu,kamwe hatapenda kwenda ualimu(with few exceptions).
Sasa tutegemee nini toka kwa hawa walimu "walio feli"?
Sasa ndugu
Kigarama,ili tutoke hapa tulipo,ni vyema kuyaangalia haya yote kiundani,badala ya kudhani Lugha ndio tatizo pekee.