mayoscissors
JF-Expert Member
- Nov 24, 2009
- 975
- 479
Ndugu zangu madaktari chonde chonde safari hii kuweni wastahimilivu kidogo kuokoa maisha ya watanzania. JK ame prove kuwa ni rais asiye msikivu, sana sana utasikia jumatatu au jumanne ameenda zake Uingereza kwa best yake David Cameron na yote yatakayotokea hatakuwepo nchini.
SULUHISHO: Mtuamuru sisi waTanzania tuandamane kwenda kuwatoa kwa NGUVU OFISINI Mponda na Naibu wake ili mambo yaishe. Hakuna aliyetegemea baada ya mateso yale waliyopata watanzania serikali ingechelea kutekeleza madai yao na hata madaktari kuamua kugoma tena, hasa dai rahisi kabisa la waziri kujiuzuru.
jamani hii logic mnayoitumia mimi siielewi kabisa, eti mbona walimu nao wana madai hawagomi...... Ooh mbona mapolisi nao wana maslahi duni hawagomi............ So whaaat???kama wao wanaridhika au ni waoga haijustify kwamba madokta nao wawe waoga. Au unataka tuongeze na madai ya walimu,mapolisi,etc kwenye madai yetu? Msitulazimishe madokta na sisi tuwe waoga waoga. Aluta continuaYuko wapi Ananilea Nkya na Deus Kibamba? mnaotaka kuandamana andamaneni mimi nabaki nyumbani, lakini kwa upande wangu nawaomba madaktari wawe na uvumilivu maana si wao tu wenye madai serikalini. Watambue kuwa watumishi wa serikali wako wengi na wote wana umuhimu katika nafasi zao je nao wakigoma itakuwaje? inawezekana wao hawana ndugu wanaohitaji tiba au wataweza kuwatibu katika zahanati zao binafsi au wanazofanya kazi part time lakini naye mwalimu akigoma wajue kuwa watoto wao hawatafundishwa, Polisi wakigoma pia watavamiwa na hata hayo madai yao hawatanufaika nayo. Ni takribani watumishi wote nchini wana madai sawa na madaktari iweje wao ambao tena serikali imeshaahidi kuyashughulikia wanaendelea kutishia tu? wafanyeje wale ambao hata kukutana na Pinda hawajawahi?
Wewe si mmoja wa mafisadi wa nchi hii, unadhani hatukujui? Wacha watu wadai haki zao. Sasa ni madaktari na siku nyingine watagoma wengine.Haiingii akilini kumtaka Mwalimu akaandamane ili Daktari atimiziwe madai yake wakati na yeye ana madai pia.
Yuko wapi Ananilea Nkya na Deus Kibamba? mnaotaka kuandamana andamaneni mimi nabaki nyumbani, lakini kwa upande wangu nawaomba madaktari wawe na uvumilivu maana si wao tu wenye madai serikalini. Watambue kuwa watumishi wa serikali wako wengi na wote wana umuhimu katika nafasi zao je nao wakigoma itakuwaje? inawezekana wao hawana ndugu wanaohitaji tiba au wataweza kuwatibu katika zahanati zao binafsi au wanazofanya kazi part time lakini naye mwalimu akigoma wajue kuwa watoto wao hawatafundishwa, Polisi wakigoma pia watavamiwa na hata hayo madai yao hawatanufaika nayo. Ni takribani watumishi wote nchini wana madai sawa na madaktari iweje wao ambao tena serikali imeshaahidi kuyashughulikia wanaendelea kutishia tu? wafanyeje wale ambao hata kukutana na Pinda hawajawahi?