Ama kweli, Tanzania itauzwa kwasababu ya mikopo

Alafu tatizo kama saa hivi ambapo mfumuko wa bei umepanda hawa wote walioingia mikataba ambayo (tuseme ukweli) wanajua wazi inatuumiza wao wanatumia misaada hii hii kujifanyia 'uwekezaji', kwa hiyo hata mafuta yafikie 5000 au kilo ya sukari ifike 7000 wao wanapata peza kutoka kwenye 'uwekezaji' wao walioufanya hivyo mzigo kuendelea kumelemea mtu wa kawaida.

Ndio maana ukihoji wako tayari hata kukuondoa maana wanadhani njia pekee ya kuwaongolea matatizo ni hiyo pekee. Ila kna njia mbadala ambayo tukikubali kujibana kwa pamoja baada ya muda unafuu utakuja sio kwa watu wote milioni 60 lakini walau 60% yao
 
Duh! Kweli iko kazi !
 
Tatizo lililopo ni kwamba ubadhirifu umetamalaki, kila MTU anataka ajilimbikizie Mali, na ile falsafa ya kazi na bata !!! Waziri mkuu alikuta Ofisi imejengwa kwa gharama ya milioni mia moja !! Lakini ukiiangalia hiyo ofisi haifiki hata milioni kumi !! Hiyo ni sehemu moja tu !!
 
Well said
Tanzania tusipokuwa makini tutakuwa kama wenzetu Sri Lanka ambao deni la taifa halishikiki wala kukamatika.

Jamaa wanadaiwa mabilioni ya dola na China.

Wamejikuta wameshanyanganywa moja ya bandari yao kubwa na mdeni wao.

Hali ya uchumi kwa sasa nchini humoni mbaya sana.

Watu wanapanga foleni ili kupata mahitaji ya kawaida (mafuta, sukari,nk).

Watu wanakufa kwa dhiki, njaa na magonjwa.

Serikali haina akiba fedha za kigeni.

Mpaka wameanza kufunga balozi zao katika mataifa mbalimbali kama vile Iraq, Norway, and Australia, na kuanza punguza idadi ya wanadiplomasia wake katika balozi zake mbalimbali.

Karibu China itajitwalia Sri Lanka sasa ili kufidia deni lake.


Zaidi ya yote inasikitisha kuona na sisi tukipita mule mule alikopita Sri Lanka.

Serikali ya CCM, someni alama za nyakati, mshaurini M/kiti wenu, maana kazi kubwa anayoiweza kwa sasa tangu aingie madarakani ni kukopa fedha na kuzunguka na bakuli huku akidai analifungua taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…