DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 302
- 274
Wanabodi,
Misaada na mikopo iliwahi kuwa mizuri katika kuleta maendeleo haswa katika kipindi cha baada ya vita vikuu vya pili vya dunia. Nchi kama Uingereza na Ufaransa zilipata maafa makubwa sana vitani na kwasababu hiyo ilibidi wapate misaada kujenga uchumi wao upya. Mpango wa misaada hii ilipewa Jina liitwalo "The Marshall plan" na ilitolewa na wamarekani kwa ajili ya nchi za ulaya magharibi. Malengo ya misaada kama hii ilikuwa kuwezesha nchi husika kujikwamua kutoka kwenye hali waliyokuwa nayo. Hadi sasa, tunashuhudia umuhimu wa kipindi hicho katika historia ya nchi hizo. Mpango huu wa Marshall ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kusaidia nchi hizi za ulaya kujikwamua kiuchumi.
Katika kipindi hiki, ilionekana kabisa kwamba misaada na mikopo inaweza kusaidia nchi yoyote kutatua changamoto zake na kuboresha maisha ya wananchi wake. Baada ya mafanikio ya Marshall plan,, mfumo kama huo ulitumika kusaidia nchi za dunia ya tatu zilizopo Afrika. Cha kusikitisha ni kwamba nchi za Afrika, zimeshindwa kutumia misaada na mikopo hii vizuri. Inawezekana kabisa kwamba deni la taifa Lime sababishwa na maamuzi mabaya haswa katika kukubali misaada na mikopo inayo semekana kuwa ya gharama nafuu.
Kuna umuhimu sana wa kuwa na nchi inayoweza kujiendesha yenyewe na kwasababu hiyo, sikubaliani na maoni ya Rais Samia ya kupata mikopo ya gharama nafuu kuendeleza miradi mbali mbali nchini, haswa ya ujenzi. Sio sahihi kukopa fedha kwa ajili ya matumizi ya kila siku na kwasababu hio ingependeza sana kama mikopo hii ingetumika katika sekta zinazo ingizia serikali faida. Kwa mfano, ujenzi wa madarasa mengi unasaidia wananchi lakini haiongezei serekali mapato yoyote na wakati wa kulipa ukifika lazima fungu litoke sehemu nyingine.
Je ni kweli kwamba serikali inakopa fedha kwasababu ina uhakika wa kupata fedha hizo baadaye?. Je changamoto kubwa katika kuendeleza miradi ni ukosefu wa fedha nyingi kwa mkupuo?. Je serikali ina "excess" ya fedha ambazo baada ya kusanywa kwa muda zinaweza kusaidia kwenye ulipaji wa madeni?