Ama kweli Pesa ni kilainishi

Boss la DP World

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
1,997
7,551
Habari wakuu,
Ninayo furaha ya pekee sana jioni ya leo baada ya kutunukiwa mwili na binti mrembo niliyemtafuta kwa miaka mingi sana bila mafanikio, sana sana niliambulia matusi mpaka nikawa najisikia vibaya.

Iko hivi, huyu mdada tulifahamiana miaka zaidi ya 10 iliyopita mimi nikiwa mwaka wa mwisho wa masomo yangu chuoni, yeye akiwa mwaka wa kwanza, nilimpenda nikaamini nikimtongoza hata kataa, niliamini tutaoana na nikaamini tutajenga familia. Siku ikawadia nikakutana naye face to face nikaomba appointment, akakubali kukutana na mimi siku iliyofuata na kweli alifika kwa wakati sehemu tuliyo kubaliana, basi baada ya salamu nikaanza kujieleza, hata kabla sijamalizia, akasimama akaniambia nilidhani una jambo la maana kumbe ni huo ujinga, hapa umepotea njia. (hiyo sentensi niliyo bold ilinikatisha tamaa sana,)

Pia sikupenda jinsi alivyo ondoka, nibora angetumia lugha nzuri kiasi, basi mimi nikaacha kabisa kumtafuta tena ila nilikuwa nampenda sana tu, siku ya mahafali yangu nikaomba kupiga naye picha akaniuliza hivi unanionaje? sikujibu kitu nikawa namwangalia tu, akaondoka. Sikuweza hata kuomba namba yake maana ningeogelea matusi.

Baada ya kumaliza chuo nilikuwa namtafuta bila mafanikio maana niligundua account zake za mitandao ya kijamii hazikuwa active. Mwezi wa 3 mwaka jana nikaona account mpya ya mtandao mmoja wa kijamii yenye jina lake na picha zake, nikam request urafiki, nikamjulia hali hakujibu chochote ila alisoma sms yangu.

Sasa from no where juzijuzi akanitext kuomba namba yangu, nikahisi account yake imedukuliwa maana najua yeye hawezi kufanya hivyo, nikamjibu naomba yakwako nikupigie, akanitumia namba 2, nikaangalia usajili jina ni lilelile, nikampigia nikamsalimia kama vile hakuna kitu, ila kichwani ile statement yake ilikuwa inajirudia, baada ya muda akaniambia amepata changamoto X na hajui atafanyaje, basi nikaona sio kesi nikafanya muamala mnono, akashukuru tukaagana.

Baada ya dakika chache akanitumia ujumbe whatsapp wa kushukuru, nikamwambia sawa. Sasa tangu jana amekuja kwenye kikao cha kazini kwao, kinafanyika mji niliyopo, alivyonipigia kuniambia nipo kwenu, nikamkaribisha, ila kwakuwa nilikuwa mbali nilimwambia tutaonana leo, nikamuuliza atakuwa confortable kufika kwangu ili aone pia familia yangu na kufahamu ninapoishi? Maana niliogopa kutaja habari za lodge.

Akaniambia hayuko confortable, nikamwambia basi ngoja nitafute sehem tulivu tukutane akasema sawa. Saa 11 nimemaliza mambo yangu nikamuuliza alipo, akaniambia nikampitia tukaenda lodge ya mafichoni, yaani nimeshangaa maana hata hakukuwa na ugumu tukajikuta tu tumeshiriki tendo, akaniambia kuwa siku ile ya mahafali hata yeye alinihurumia alivyotafakari ila ndiyo hivyo ni mambo yaliyopita.

Nilichofurahi ni kuwa nime enjoy sana kutimiza ndoto yangu. Nimeona nisilale bila kutoa ushuhuda, kama yuko humu basi ajue nampenda.
 
Mkuu yan ulikua unataka kumpeleka nyumbani akamsalimie mkeo?
Isinge wezekana mkuu nilijua hatakuwa na ujasiri huo, ila nilikwepa kumtajia lodge kama option yakwanza, nilikwepa kutaja restaurant maana baada ya kutoka kwenye restaurant ingekuwa ngumu kumshawishi kwenda kutiana. Ni mambo ya cuba haya.
 
Wewe ndiyo umelainishwa! Huyu maisha yake (hasa ya kimahusiano) hayajamwendea vyema. She is now above 30 and likely desperate....

Maana baada ya miaka 10 ya kukutreat kama mbwa...

Ghafla kaibuka from nowhere...akiwa na shida....

Nawe kwa uboya wako ukapeleka muamala mnono. Utu wako ni huo muamala ama? Bila huo muamala ungeweza kumpata au ungeendelea kutukanwa kama mbwa?

Kama umelala naye sababu ya huo muamala, itakuwa ni makosa kusema kuwa umeuziwa hiyo mbususu?

Na si ajabu umeuza mechi...huku, kama ulivyosema, una familia....

Ni nani aliyelainishwa hapo? Una tofauti gani na wanaonunua machangu barabarani?

A man without principles is like a ship without an anchor. Ni kusukwa sukwa tu na mawimbi huku na huko...na mwishowe hata kugoteshwa kwenye miamba au mangrove swamps.

Screenshot_20230519_131717_Chrome.jpg

Sad!
 
A man without principles is like a ship without an anchor. Ni kusukwa sukwa na mawimbi tu kila mahali...na mwishowe hata kugoteshwa kwenye miamba au mangrove swamps.

Pole!
You did hit the nail on the head.
Na Kama huyu bwege ataendelea na huyu Dem, atakuja umizwa mbeleni Kama Dem ata reconcile na aliyekua anamtindua.
 
Bei Elekezi
Nimegundua mambo machache kwako:

1. Vijana wengi approach yenu mbovu....tengeneza mazingira na huhitaji nguvu nyingi kutongoza ujue

2. Huwezi day one sio sahihi sana kutongoza
3. Kuna wanawake ukionyesha uchu mkubwa umemkosa
..............................

4. Inasikitisha wanaume wengi hatujui thamani yetu...ke akikutaka yeye unapatikana 24/7/12
Huu ni ujinga mzito.

5. Nilivyo na dharau ningempa hiyo pesa kama ninavyosaidia yatima lkn simgusi kwa kutaka kwake hadi nimtake mimi.

6. Umeliwa kimasihara bro ooooh🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Shimba ya Buyenze
 
Wewe ndiyo umelainishwa! Huyu maisha yake (hasa ya kimahusiano) hayajamwendea vyema. She is now above 30 and likely desperate....

Maana baada ya miaka 10 ya kukutreat kama mbwa...

Ghafla kaibuka from nowhere...akiwa na shida....

Nawe kwa uboya wako ukapeleka muamala mnono. Utu wako ni huo muamala ama? Bila huo muamala ungeweza kumpata au ungeendelea kutukanwa kama mbwa?

Kama umelala naye sababu ya huo muamala, itakuwa ni makosa kusema kuwa umeuziwa hiyo mbususu?

Na si ajabu umeuza mechi...huku, kama ulivyosema, una familia....

Ni nani aliyelainishwa hapo? Una tofauti gani na wanaonunua machangu barabarani?

A man without principles is like a ship without an anchor. Ni kusukwa sukwa tu na mawimbi huku na huko...na mwishowe hata kugoteshwa kwenye miamba au mangrove swamps.

Sad!
Umeboneza vizuri mzee mwenzangu ngoja nikuite kwa post yangu
 
Dah umepigwa pakubwa Sana!ukiona miaka 10 umekataliwa ndio umekuja kukubaliwa ghafla yaani wewe ni last option kwenye Maisha yake,huyo ana mawili,
La kwanza kakwama kwa mtu anayempenda na bado hajapata mbadala wa kuziba pengo,

la pili kaamua kukuweka wewe Kama chanzo chake cha mapato.
Matusi makubwa sana.
Miaka 10 si anabugia mavi ya kale?
Huwa sirudi nyuma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom