• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Ama kweli mapenzi kizungumkuti

bongompya

bongompya

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2015
Messages
224
Points
195
bongompya

bongompya

JF-Expert Member
Joined May 10, 2015
224 195
"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng?ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.

Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.

Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga lakini aliipinga sana.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.

Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi.

Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.

Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.

Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulishanyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.

Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia baruahii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu.

Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyikanakufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie vibayamaana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!

Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako-
AMENITENDA HIVI!!!
LIKE & SHARE
 
just-imagine

just-imagine

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Messages
355
Points
500
just-imagine

just-imagine

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2015
355 500
.....so sad😪😪😞😞😫😫
 
habari ya hapa

habari ya hapa

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
12,828
Points
2,000
habari ya hapa

habari ya hapa

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
12,828 2,000
Aiseeee du, mabaya sana
 
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Messages
3,965
Points
2,000
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2013
3,965 2,000
hii issue ya mapenzi ni jipu lingine la kutumbuliwa na mheshimiwa!
 
G

Gojaga Nize

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Messages
2,764
Points
2,000
G

Gojaga Nize

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2015
2,764 2,000
Hivi hii sijawahi iona sehemu kweli....
 
Lmntrix

Lmntrix

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2014
Messages
574
Points
500
Lmntrix

Lmntrix

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2014
574 500
Inamaana in whatever cases ulitoa mimba mara nyingi,so ikawa kawaida yako kunyofoa mpaka kizazi kikawa easily uprooted, enhe enhe kwahyo generation yako imefikia kikomo pole, sasa utajajibu nini siku ya hukumu ume uwa kiasi gani kwa kukosa akili.. Pole...usha haribu...
Ahsante kwa utunzi anyway
 
S

simple B mgendi

New Member
Joined
Nov 27, 2015
Messages
3
Points
45
S

simple B mgendi

New Member
Joined Nov 27, 2015
3 45
Mmh love love love .............,.,
 
A

aaamuk

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2015
Messages
709
Points
0
A

aaamuk

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2015
709 0
Watu wana maumivu yao...ukisimuliwa visa vya mapenzi ...unaweza weka kisa chako kwenye shelf
..anyway pole
 
Forensic Anthropologist

Forensic Anthropologist

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2015
Messages
2,219
Points
2,000
Forensic Anthropologist

Forensic Anthropologist

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2015
2,219 2,000
Usijali baby kama watoto tutafanya adoption
 
Typical

Typical

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
338
Points
250
Typical

Typical

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
338 250
Unapataje mimba ukiwa kwenye siku zako..!!!?
 
Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2012
Messages
28,529
Points
2,000
Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2012
28,529 2,000
Ni zaidi ya unyama
 
blogger

blogger

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2012
Messages
2,937
Points
2,000
blogger

blogger

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2012
2,937 2,000
Chuo gani ? Cha ujinga..! Muwe mnavitaja.
 

Forum statistics

Threads 1,403,909
Members 531,427
Posts 34,438,875
Top