Ama kweli mambo mengine huwa hayaelezeki.

Ama kweli mambo mengine huwa hayaelezeki.

Waterlemon

Senior Member
Joined
Sep 2, 2016
Posts
143
Reaction score
199
Nilienda kijijini kumtembelea mjomba wangu hukooo mikoani. Alikuwa ni mfugaji wa ng’ombe maarufu mkoani huko. Huwa akiuza ng’ombe wake pamoja hata na miradi ya kuuza maziwa kwenye viwanda vya kutengeneza maziwa pamoja na rasili nyengine nyengine zitokanazo na mifugo. Shambani huko alikuwa akikaa na mkewe...

Kwanza niacheni niseme, maana msema kweli ni mpenzi wa mungu…. Inachekesha haswa kumuita mke wa mjomba wangu “shangazi“ maana alikuwa ni msichana wa umri wangu tena ambae hatukupishana sana na tulishazoeana hata kabla hajamuoa. Tena nikiri kabisa, shangazi alikuwa kaumbika yaani masihara pembeni. Kwa kweli shangazi alikuwa mbichiii… kitoto chuma haswa…. yaani mpaka mie matembezi kwa mjomba nayatilia wasi wasi. Maana ibilisi hachezi mbali. Lakini heshma kwa mjomba…. Umaluuni huo sina!!


Basi katika matembezi na makazi yangu shambani kwa mjomba, asubuhi moja naamka naona nyumba kimyaaa. Nilipotoka nje namuona mjomba yupo kakaa kwenye kizingiti cha mlango kashika kichwa machozi yakimtoka.

“Vipi mjomba salama?” Nikamuuliza huku nikichuchumaa pembeni yake kwa wasiwasi mwingi kujua lipi lililomkuta. Mjomba akatingisha kichwa na kujibu kwa huzuni “Ama kweli mambo mengine huwa hayaelezeki.”


“Ni nini kilichotokea mjomba ambacho kimekutia huzuni namna hii?” nikamuuliza mjomba kwa kumuwekea mkono begani kumliwaza kwa huruma na kumsihi anieleze lililomkuta.

“Jana nilipapurana na anti yako, tukalala tumehamakiana kila mmoja upande wake wa kitanda. Tukalala wakavu wakavu. Leo asubuhi niliamka asubuhi na mapeka nikaenda kwenye banda la ng’ombe kukamua maziwa ya ng’ombe. Nilipokaribia kujaza bakuli la maziwa, yule ng’ombe akalipiga teke bakuli kwa mguu wa kulia maziwa yote yakamwagika”… huku mjomba akiendelea kutingisha kichwa … “Ama kweli mambo mengine huwa hayaelezeki.”

“Okay, lakini mjomba hilo si suala kubwa mno la kusikitisha”… nikamueleza kwa kumliwaza huku nikijieka pembeni yake… “Lipi zaidi lililotokea?”.. nikazidi kudadisi.

“mambo mengine huwa hayaelezeki.”.. .mjomba akaendelea.. “nikachukua kamba na kuufunga mgu wa kulia katika nguzo ya upande ule wa kulia”

“Halafu?”

“Nikakaa tena chini kumkamua ng’ombe maziwa. Nilipokaribia kujaza tena bakuli, ng’ombe akainua mguu wa kushoto na kulipiga tena teke bakuli, maziwa yote wakamwagika”

“Kalipiga tena teke?”.. Nikauliza… “Ama kweli mambo mengine huwa hayaelezeki.”.. arudia tena kauli mjomba huku akitingisha kichwa.

“That’s still not so bad uncle, lipi tena lililoendelea?”

Mjomba akaendelea… “nikachukua kamba na kuufunga mguu wa kushoto katika nguzo ya upande ule wa kushoto”

“Enhe?”… nikauliza maana najua ule sio mwisho wa tukio lile…

“Baada ya kukaa na kumkamua tena ng’ombe maziwa karibia bakuli kujaa, the stupid cow akalipindua tena bakuli la maziwa kwa mkia wake”

Nikabanwa na kicheko… “Hhhm”……. nikidadisi huku nikijizuia kucheka..... “ukafanya nini tena?”

“Well,” … akaendelea mjomba… “”Sikuwa na kamba nyengine ya kutumia, hivyo nikavua mkanda wangu wa suruali na na kuufunga mkia kwenye nguzo ya juu la banda. Wakati niko nyuma ya ng’ombe nimenyoosha mikono juu kuuinua mkia wa ng’ombe kuufunga juu ya nguzo ya banda, suruali yangu ikanipwaya na kunianguka chini. Muda huo huo mke wangu akaingia bandani…”

Shangazi kafunga mizigo yake huyooo kwao!..

Machozi yakim miminika zaidi… “Ama kweli mambo mengine huwa hayaelezeki.”

Hapo tena nikashindwa kujizuia. Niliporomoa kicheko kile cha kutapatapa na kubiringia... :'D

I was in stitches... "Pole mjomba!"
 
Back
Top Bottom