Alphonce Lusako: Nina haki na mimi kusoma chuo

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE DHIDI YA SAKATA ENDELEVU LA UONEZI JUU YANGU KATIKA KUTIMIZA NDOTO ZANGU KIELIMU.
-------------------------------------

Na: Alphonse Lusako

Kabla ya kueleza, undani wa sakata la kufukuzwa kwa mara ya pili Chuo Kikuu cha Dar es Watanzania, jueni kwamba ninaonewa, ni takribani miaka sita sasa, napambana kuitafuta haki yangu ya kusoma bila mafanikio, nimezunguka nchi hii, kuomba, Viongozi wenye mamlaka na Elimu, wanipatie haki yangu ya kusoma, bila ya mafanikio.

Kwa mara ya kwanza nilijiunga na chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM) mwaka 2009 na kudahiliwa kusoma Shahada ya Biashara katika Uhasibu ( Bcom Account). Lakini mwaka 2011 mimi na wanafunzi wenzangu kadhaa tulifukuzwa UDSM na Kufutwa katika Mfumo wa Elimu nchini.

Sababu kuu ya kufukuzwa UDSM, ni kuratibu Mgomo wa Wanafunzi UDSM wa kupinga kurudishwa kwa Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza waliokwisha wasili vyuo vikuu vya umma nchini, kurudishwa nyumbani kwa hoja hafifi kwamba bajeti haitoshi. WANA-UDSM, tulihoji, uwepo wa mikopo hewa ambayo ilikuwa inaliwa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu.

Tuliiomba Serikali, Mikopo hewa yote ielekezwe kuwadhamini baadhi ya Wanafunzi. Mnakumbuka, Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako, kuanzia August 17, 2016, alivitaka vyuo vikuu takribani 31 kati ya 81, kurejesha fedha walizozipokea ambazo ni za wanafunzi hewa. Haya yote ni matokeo ya uhojaji wetu tangu miaka ya 2011 (Rejeeni ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali “CAG” za miaka 4 iliyopita).

Tunashukuru, Mwenyezi Mungu, sisi tukatolewa mbuzi wa kafara lakini baada ya siku mbili tu Serikali kupitia Bodi ya Mikopo (HESLB) iliwadhamini mikopo wanafunzi wengi ndani ya vyuo vikuu vya umma nchini, kitakwimu, upande UDSM, Wanafunzi zaidi 144 walipewa mikopo.

Ifahamike kwamba, vuguvugu la migomo Vyuo Vikuu nchini, kwa kiasi kikubwa, ni zao la ubidhaishaji wa Sekta ya Elimu, ulioanza miaka ya 1990’s baada ya Serikali kuanzisha Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya juu (Cost sharing Policy). Hii ni sera pekee, iliyoleta matabaka makubwa sasa kati ya Walionacho na Wasionacho katika Mfumo wa Elimu nchini.

Kihistoria(Hatua Tulizozichukua)
Tulianza kufanya hatua za ndani ya Chuo, tukakata rufaa dhidi ya maamuzi ya kutufukuza na kutufuta katika mfumo wa elimu, Tukiomba baraza la Chuo (UDSM) Lirejee maamuzi husika yenye lengo la kupoka haki yetu ya kusoma katika vyuo vya umma nchini. Baraza la chuo lilikataa maombi yetu.
Tulishitakiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu (Criminal case No. 270 ya 2011). kwa makosa makuu mawili, mosi, Kufanya Mkusanyiko usio halali, pili kukaidi amri ya polisi iliyotutaka tutawanyike.

Mnamo tar. 30.08.2012, Tulishinda kesi hii kwa Mahakama kutupilia mbali shitaka husika. Tuliporudi Chuoni, Wanafunzi takribani 12 kati ya 51 tukabaguliwa bila sababu za msingi na hatukurudishwa.
Tukaanza njia za kidiplomasia tena, tulizunguka nchi hii kwa kila kiongozi mwenye mamlaka na sekta ya Elimu, tukiomba huruma yao ya kuturudisha Chuoni tumalize shahada zetu.

Tuliandika barua kwa Mkurugenzi wa Vyuo vikuu, Waziri wa Elimu, Mh. Shukuru Kawambwa kwa wakati huo, Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Nahodha vuai kwa wakati huo ambaye tulimuomba atusaidie suala letu la kesi mahakamani. Tuliomba Tume ya Utawala bora na haki za Binadamu iingilie kati, Tuliomba Bunge La jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kamati maalumu iliyokuwa inaongozwa na Mh. Magreth Sitta, kuingilia kati. Hatua zote hizi hazikuleta suluhisho.

Baada ya hatua zote hizo kushindikana, tuliona kutafuta haki yetu Mahakamani ndio njia pekee. Tuliomba msaada katika taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) na Tanganyika Law Sociaty (TLS), tukapatiwa mawakili ambao wamepambana miaka yote kututea (takribani miaka 5) mahakamani ili tupate haki yetu ya kusoma bila mafanikio, tulianza Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, tukakata rufaa mahakama kuu, tukakata rufaa mahakama ya Rufaa (Appeal Court of Tanzania). Ilipofika mwaka 2016, nikaona niachane na masuala ya kesi kwani ni muda mrefu nipo mahakamani. Nikatoa faili langu mahakamani.
Nikaamua kuingia katika diplomasia tena. tukamuandikia Mh. Raisi (John Pombe Makufuli) kuomba aingilie kati mgogoro huu ili tupate haki yetu ya kusoma nchini.

Tuliamini na bado ninaamini kwamba, Mtu mwenye mamlaka makubwa kwenye nchi yoyote ile duniani, baada ya Mwenyezi Mungu, Ni Rais. Tukashukuru Mungu, Wasaidizi wa Mh. Raisi katika masuala ya Elimu na Sheria walionyesha Ushirikiano, tumekaa vikao mara kadhaa Ikulu, wakamshirikisha Mkurugenzi wa Vyuo vikuu, wakaishirikisha wizara ya Elimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Vyuo vikuu (TCU), wakati huo akiwa ni Prof. Yunus Mgaya.

Mnamo tar 12. 02. 2016, TCU waliwaandikia barua rasmi Chuo (UDSM) kwamba kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu [Universities reguration 43(1) GN 226 ya mwaka 2013, Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo kwa masuala ya kinidhamu anaruhusiwa kuomba Chuo kwa mara nyingine tena baada ya miaka miwili kupita, katika chuo hicho hicho au vyuo vingine tangu kufukuzwa kwake (Barua imeambatanishwa), hivyo akakiomba Chuo kitupe Ushirikiano.

Kutokana na Ushauri husika, mwaka 2016 nikaomba udahili katika Vyuo vikuu vitatu ikiwemo UDSM. TCU wakanichagua nisome UDSM shahada ya Uchumi (Economics) kipaumbele changu cha pili baada ya Sheria, kwa kuwa ndoto yangu ni kusoma shahada ya Sheria, nikaanza hatua za kubadilisha kozi kuelekea Shahada ya Sheria, Utawala wa UDSM, Ulinipa Ushirikiano kwa kugonga mihuri ya kukubali kubadilisha kozi yangu, hadi DVC Undergraduate UDSM, alithibitisha hamisho langu.

Hakuna Mtawala ambaye hajui kwamba Alphonce Lusako, hasomi Chuo kikuu cha Dar es Salaam. ni miezi minne sasa imepita tangu nianze masomo yangu chuoni, katika hali ya sintofahamu mnamo tar 30.01.2017 nikiwa katika ratiba yangu ya mtihani nikapewa barua ya kusimamishwa uanafunzi wangu (nimeambatanisha) kwa kile kinachodaiwa kwamba nimedahiliwa kimakosa na hivyo kusimamishwa rasmi masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Sio siri, nilishtushwa, niliumizwa, kibinadamu iliniwia ngumu sana.

Kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Vyuo vikuu (TCU)
Kwa kuwa nilikuwa katika ratiba ya mitihani yangu (UE), Haraka iwezekanavyo, nikakikimbilia Tume ya Vyuo vikuu(TCU) kuonana na Mkurugenzi Mtendaji wa TCU, Kuomba aingilie kati dhuluma hii nifanye mitihani yangu.

Niliandika barua rasmi kwa mujibu wa Sheria za vyuo vikuu (Universities Regulation) ili TCU inisaidie haraka iwezekanavyo niendelee na mitihani, kwani . Mkurugenzi akasema niache barua atakaa na wanasheria wake kisha nitapewa mrejesho, nimeshinda TCU siku zote tatu bila ya majibu ya barua yangu.

Nilipofanya marejeo ya Maamuzi ya Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya tar.13 desember 2011 yaliyoelekeza Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kutufuta katika Mfumo wa Elimu nchini. Huenda haya yote yanayotokea sasa ni utekelezaji wa maazimio husika.
Watanzania, ifahamike kwamba ninaonewa, niliwahi muambia Prof. Rwekaza Mkandala kwamba, “Kumnyima mtoto wa masikini elimu, ni sawa na kumpiga risasi afe katika nchi yake.” Hakuna dhambi kuu niliyoitenda nchi hii, nikastahili adhabu ya kupokwa haki yangu ya kusoma ndani ya nchi hii milele.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ni chuo kikuu cha umma, ni chuo kilichojengwa na kodi za watanzania, ni chuo kilichojengwa na jasho la kila mtanzania. Hivyo kila mtanzania mwenye sifa kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria, anapaswa kusoma katika chuo hiki bila kubaguliwa.

Kuongoza Vyuo Vikuu kwa misingi ya Sheria
Mpaka sasa ninamifano ya Wanafunzi walioikimbia nchi hii na kuenda kusoma nje ya nchi kwa sababu ya ukiukwaji mkubwa wa Sheria ndani ya vyuo vikuu nchini. Natamani kuona nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii. Tukiendelea kuongoza vyuo vikuu , kwa visasi, kwa chuki binafsi, neno la mtu likawa sheria, watawala wa vyuo vikuu wakawa juu ya sheria, tutaliingiza taifa hili katika gharama za machafuko.

Hitimisho.
Nimetafakari sana, na kujiuliza maswali mengi watanzania, ninachokishuhudia katika maisha yangu ni kwamba; hawapambani na binadamu anayeitwa Alphonce Lusako, wanapambana na Elimu atayoipata Alphonce. Fimbo yao kuu, ni umasikini wangu na wazazi wangu, Kibinadamu masuala haya ni magumu sana, nimeona nimuache Mwenyezi Mungu apambane mwenyewe.

Aidha, niwashukuru viongozi wote wa dini walionipigia simu kutoka mikoa mbalimbali, wakinifariji, nachelea kusema, waliombee taifa kwani kunavijana wengi katika vyuo vikuu hutendwa kama ninavyotendwa. Niwashukuru wazazi wangu watambue kwamba haya ni mapito na yatapita, Niwashukuru Wanafunzi wenzangu wa UDSM, niseme neno moja tu (KWAHERINI), Niwashukuru wanasheria, ndugu na marafiki zangu walioshikamana name katika wakati huu, nachotaka niseme kwao ni kwamba, hatma ya maisha ya mwanadamu ipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu.
 
Daaaah 2009 bado unapigana kuendelea na first degree wakati walioingia chuo 2013 Sasa hivi wamemaliza na wanafanya kazi"

Nashauri vijana wenzetu hasa kutoka familia masikini waende vyuoni kusoma tu ndio kazi inayowapeleka huko siasa na migomo waachieni wanasiasa..............

Siasa na migomo havilipi bila kuwa na pesa utabaki kutanga tanga tu mtaani mpaka unazeeka............

Mtafute Mbatia atakupa somo la kutosha kuhusu shida yako..........
 
UNALETA HARAKATI WAKATI ELIMU YAKO DUNI?
Hiyo kazi si ungewaachia kina profesa Lipumba? Sasa urudi kijijini ukalime kenge weee unayetaka kushindana na ulimwengu. You should have known that this World is not fair...
Sasa utakula jeuri yako. Kama uliwashinda wazazi wako, sio kwamba utamshinda kila mtu. Wenzako tumesoma UDSM kwa shida shida hivyo hivyo, majoho tumevaa na sasa sisi ndio vigogo wa mashirika na taasisi nyeti...
Hatuko hapa kutetea ujinga, hata kama hatuishabikii sisis em, hili la kwako la kufukuzwa chuo ni la kipuuuzi...
 
mkuu yule mama aliyelia juzi mbele ya rais amenimaliza kabisa somalia ilikuwa na amani kama tanzania wanachochea tu bado kidogo
 
Kuna wakati unashindwa kuwaelewa baadhi ya watu waliopewa mamlaka kuwa nao ni binadamu au wanyama?
Hawa vijana nawakumbuka sana kwenye hili sakata, kwanza walitimuliwa kipindi kigumu sana na walijitahidi sana hata kuomba hili jambo liishe lakini kwa kiburi cha baadhi ya watendaji wa chuo waliwakomalia wakiwatuhumu kutumwa na chama cha siasa.
Kosa wanalotaka kuwanyanyasa nalo ni dogo mno, mgomo ule ulikuwa wa kawaida sana na haukuleta madhara yoyote yale, na wanafunzi wale walichokidai serikali baadae ilitekeleza baada ya kuona mantiki ya madai yao, sasa hapo nani anastahili adhabu?
Ifikie hatua taasisi zetu zijiepushe na siasa za kitoto namna hii.
Ni aibu kubwa chuo kama UDSM kimdahili mwanafunzi halafu baada ya miezi kadhaa kilete sababu za kitoto eti wamemdahili kimakosa, hapa wanataka tuamini kuwa TCU wakishirikiana na UDSM wanadahili wanafunzi wasiokuwa na sifa.
Wapeni haki hawa vijana wasome , makosa yao ni madogo ukilinganisha na nyinyi mwenye mamlaka madhambi mliyowafanyia Watanzania huenda nyinyi mlistahili kunyongwa kabisa.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE DHIDI YA SAKATA ENDELEVU LA UONEZI JUU YANGU KATIKA KUTIMIZA NDOTO ZANGU KIELIMU.
-------------------------------------

Na: Alphonse Lusako

TCU wakanichagua nisome UDSM shahada ya Uchumi (Economics) kipaumbele changu cha pili baada ya Sheria, kwa kuwa ndoto yangu ni kusoma shahada ya Sheria, nikaanza hatua za kubadilisha kozi kuelekea Shahada ya Sheria, Utawala wa UDSM, Ulinipa Ushirikiano kwa kugonga mihuri ya kukubali kubadilisha kozi yangu, hadi DVC Undergraduate UDSM, alithibitisha hamisho langu.

Hakuna Mtawala ambaye hajui kwamba Alphonce Lusako, hasomi Chuo kikuu cha Dar es Salaam. ni miezi minne sasa imepita tangu nianze masomo yangu chuoni, katika hali ya sintofahamu mnamo tar 30.01.2017 nikiwa katika ratiba yangu ya mtihani nikapewa barua ya kusimamishwa uanafunzi wangu (nimeambatanisha) kwa kile kinachodaiwa kwamba nimedahiliwa kimakosa na hivyo kusimamishwa rasmi masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kwanza Lusako apewe pole kwa maswahibu yaliyomkuta.
Pia siungi mkono uanaharakati wowote vyuoni, hivyo naamini he has learned his lessons, na huku kuzuiliwa kufanya EU isije kuwa amerudia harakati kichinichini!.

Concern yangu japo alitamani kusoma Sheria lakini TCU wakamdahili kwenye Economics, ningependa kujua Credits zake za kuingia Chuo kama zilikidhi vigezo vya kusoma Sheria? .

Angeiweka hiyo barua ya kunzuia kufanya EU na tukazijua sababu, tutakuwa in a better position ku coment.

Hivyo naomba credits zake na hiyo barua tumsaidie kijana asome.
Ila katika ku Google ili kuangalia credits zake, nikakutana na haya makitu.

Waraka: Alphonce Lusako alias Emekha Ikhe kwako prof. Rwekaza Mkandala

https://www.google.com/url?sa=t&source=web&rct=j&url=http://mambodaima.blogspot.com/2016/10/king-of-morocco-received-for-leo-here-in.html?m=1&ved=0ahUKEwih_MzN_vbRAhVDSBQKHbVRAk8QFgg0MAk&usg=AFQjCNHNkPSl3QwmPlS6aE55ogvenJLh0w&sig2=1ntT6VrYF0DotWFENb5sig

Ushauri wangu kwa Alifonsi ni kuamua kushika moja kati ya kushika masomo au kuendelea na uanaharakati.

Akiamua kusoma asome na harakati awake pembeni. Akiamua kuendelea na harakati, masomo awake pembeni.
Paskali
 
UNALETA HARAKATI WAKATI ELIMU YAKO DUNI?
Hiyo kazi si ungewaachia kina profesa Lipumba? Sasa urudi kijijini ukalime kenge weee unayetaka kushindana na ulimwengu. You should have known that this World is not fair...
Sasa utakula jeuri yako. Kama uliwashinda wazazi wako, sio kwamba utamshinda kila mtu. Wenzako tumesoma UDSM kwa shida shida hivyo hivyo, majoho tumevaa na sasa sisi ndio vigogo wa mashirika na taasisi nyeti...
Hatuko hapa kutetea ujinga, hata kama hatuishabikii sisis em, hili la kwako la kufukuzwa chuo ni la kipuuuzi...
Kama wewe kweli ni kigogo wa shirika lolote hapa nchini basi hii nchi imelaaniwa na nitamuunga mkono Rais aendelee kuwatumbua kwani wewe ulistahili kuwa watu wa mwanzo kutimuliwa.
Unataka kutuambia hata wale walioliona hili na kuamua kuwarudisha na hawana akili yaani hata Rais aliyeruhusu watu wake wawasikikize naye hakuwa ni mwenye kujua?
 
Hii naitumia na nawashauri vijana wengi sana juu la hili.

Siasa za vyuoni hazitufikishi popote. 2009-2016 ni miaka 7. Waliokuwa naye wanamaliza PhD au wanafanya kazi na hela wanazo.

Tusipotezee nafasi zetu za kielimu kwa sababu ya kutaka kuwa wanasiasa.

Hatuwezi kugoma kwenda kazini utarajie mshahara utapata. CHezea mshahara, usichezea kazi.
Nashauri vijana hasa kutoka familia masikini waende vyuoni kusoma tu ndio kazi inayowapeleka huko siasa na migomo waachieni wanasiasa..............

We have long way to go.......
 
Nothing is endless under the righteous judgment will come on your side. Keep on believing in God
 
Nisaidieni kwa nini dogo ameanzisha hii hoja yake kwenye jukwaa la siasa? is it coincidence au ndio....????
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE DHIDI YA SAKATA ENDELEVU LA UONEZI JUU YANGU KATIKA KUTIMIZA NDOTO ZANGU KIELIMU.
-------------------------------------

Na: Alphonse Lusako

Kabla ya kueleza, undani wa sakata la kufukuzwa kwa mara ya pili Chuo Kikuu cha Dar es Watanzania, jueni kwamba ninaonewa, ni takribani miaka sita sasa, napambana kuitafuta haki yangu ya kusoma bila mafanikio, nimezunguka nchi hii, kuomba, Viongozi wenye mamlaka na Elimu, wanipatie haki yangu ya kusoma, bila ya mafanikio.

Kwa mara ya kwanza nilijiunga na chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM) mwaka 2009 na kudahiliwa kusoma Shahada ya Biashara katika Uhasibu ( Bcom Account). Lakini mwaka 2011 mimi na wanafunzi wenzangu kadhaa tulifukuzwa UDSM na Kufutwa katika Mfumo wa Elimu nchini.

Sababu kuu ya kufukuzwa UDSM, ni kuratibu Mgomo wa Wanafunzi UDSM wa kupinga kurudishwa kwa Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza waliokwisha wasili vyuo vikuu vya umma nchini, kurudishwa nyumbani kwa hoja hafifi kwamba bajeti haitoshi. WANA-UDSM, tulihoji, uwepo wa mikopo hewa ambayo ilikuwa inaliwa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu.

Tuliiomba Serikali, Mikopo hewa yote ielekezwe kuwadhamini baadhi ya Wanafunzi. Mnakumbuka, Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako, kuanzia August 17, 2016, alivitaka vyuo vikuu takribani 31 kati ya 81, kurejesha fedha walizozipokea ambazo ni za wanafunzi hewa. Haya yote ni matokeo ya uhojaji wetu tangu miaka ya 2011 (Rejeeni ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali “CAG” za miaka 4 iliyopita).

Tunashukuru, Mwenyezi Mungu, sisi tukatolewa mbuzi wa kafara lakini baada ya siku mbili tu Serikali kupitia Bodi ya Mikopo (HESLB) iliwadhamini mikopo wanafunzi wengi ndani ya vyuo vikuu vya umma nchini, kitakwimu, upande UDSM, Wanafunzi zaidi 144 walipewa mikopo.

Ifahamike kwamba, vuguvugu la migomo Vyuo Vikuu nchini, kwa kiasi kikubwa, ni zao la ubidhaishaji wa Sekta ya Elimu, ulioanza miaka ya 1990’s baada ya Serikali kuanzisha Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya juu (Cost sharing Policy). Hii ni sera pekee, iliyoleta matabaka makubwa sasa kati ya Walionacho na Wasionacho katika Mfumo wa Elimu nchini.

Kihistoria(Hatua Tulizozichukua)
Tulianza kufanya hatua za ndani ya Chuo, tukakata rufaa dhidi ya maamuzi ya kutufukuza na kutufuta katika mfumo wa elimu, Tukiomba baraza la Chuo (UDSM) Lirejee maamuzi husika yenye lengo la kupoka haki yetu ya kusoma katika vyuo vya umma nchini. Baraza la chuo lilikataa maombi yetu.
Tulishitakiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu (Criminal case No. 270 ya 2011). kwa makosa makuu mawili, mosi, Kufanya Mkusanyiko usio halali, pili kukaidi amri ya polisi iliyotutaka tutawanyike.

Mnamo tar. 30.08.2012, Tulishinda kesi hii kwa Mahakama kutupilia mbali shitaka husika. Tuliporudi Chuoni, Wanafunzi takribani 12 kati ya 51 tukabaguliwa bila sababu za msingi na hatukurudishwa.
Tukaanza njia za kidiplomasia tena, tulizunguka nchi hii kwa kila kiongozi mwenye mamlaka na sekta ya Elimu, tukiomba huruma yao ya kuturudisha Chuoni tumalize shahada zetu.

Tuliandika barua kwa Mkurugenzi wa Vyuo vikuu, Waziri wa Elimu, Mh. Shukuru Kawambwa kwa wakati huo, Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Nahodha vuai kwa wakati huo ambaye tulimuomba atusaidie suala letu la kesi mahakamani. Tuliomba Tume ya Utawala bora na haki za Binadamu iingilie kati, Tuliomba Bunge La jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kamati maalumu iliyokuwa inaongozwa na Mh. Magreth Sitta, kuingilia kati. Hatua zote hizi hazikuleta suluhisho.

Baada ya hatua zote hizo kushindikana, tuliona kutafuta haki yetu Mahakamani ndio njia pekee. Tuliomba msaada katika taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) na Tanganyika Law Sociaty (TLS), tukapatiwa mawakili ambao wamepambana miaka yote kututea (takribani miaka 5) mahakamani ili tupate haki yetu ya kusoma bila mafanikio, tulianza Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, tukakata rufaa mahakama kuu, tukakata rufaa mahakama ya Rufaa (Appeal Court of Tanzania). Ilipofika mwaka 2016, nikaona niachane na masuala ya kesi kwani ni muda mrefu nipo mahakamani. Nikatoa faili langu mahakamani.
Nikaamua kuingia katika diplomasia tena. tukamuandikia Mh. Raisi (John Pombe Makufuli) kuomba aingilie kati mgogoro huu ili tupate haki yetu ya kusoma nchini.

Tuliamini na bado ninaamini kwamba, Mtu mwenye mamlaka makubwa kwenye nchi yoyote ile duniani, baada ya Mwenyezi Mungu, Ni Rais. Tukashukuru Mungu, Wasaidizi wa Mh. Raisi katika masuala ya Elimu na Sheria walionyesha Ushirikiano, tumekaa vikao mara kadhaa Ikulu, wakamshirikisha Mkurugenzi wa Vyuo vikuu, wakaishirikisha wizara ya Elimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Vyuo vikuu (TCU), wakati huo akiwa ni Prof. Yunus Mgaya.

Mnamo tar 12. 02. 2016, TCU waliwaandikia barua rasmi Chuo (UDSM) kwamba kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu [Universities reguration 43(1) GN 226 ya mwaka 2013, Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo kwa masuala ya kinidhamu anaruhusiwa kuomba Chuo kwa mara nyingine tena baada ya miaka miwili kupita, katika chuo hicho hicho au vyuo vingine tangu kufukuzwa kwake (Barua imeambatanishwa), hivyo akakiomba Chuo kitupe Ushirikiano.

Kutokana na Ushauri husika, mwaka 2016 nikaomba udahili katika Vyuo vikuu vitatu ikiwemo UDSM. TCU wakanichagua nisome UDSM shahada ya Uchumi (Economics) kipaumbele changu cha pili baada ya Sheria, kwa kuwa ndoto yangu ni kusoma shahada ya Sheria, nikaanza hatua za kubadilisha kozi kuelekea Shahada ya Sheria, Utawala wa UDSM, Ulinipa Ushirikiano kwa kugonga mihuri ya kukubali kubadilisha kozi yangu, hadi DVC Undergraduate UDSM, alithibitisha hamisho langu.

Hakuna Mtawala ambaye hajui kwamba Alphonce Lusako, hasomi Chuo kikuu cha Dar es Salaam. ni miezi minne sasa imepita tangu nianze masomo yangu chuoni, katika hali ya sintofahamu mnamo tar 30.01.2017 nikiwa katika ratiba yangu ya mtihani nikapewa barua ya kusimamishwa uanafunzi wangu (nimeambatanisha) kwa kile kinachodaiwa kwamba nimedahiliwa kimakosa na hivyo kusimamishwa rasmi masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Sio siri, nilishtushwa, niliumizwa, kibinadamu iliniwia ngumu sana.

Kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Vyuo vikuu (TCU)
Kwa kuwa nilikuwa katika ratiba ya mitihani yangu (UE), Haraka iwezekanavyo, nikakikimbilia Tume ya Vyuo vikuu(TCU) kuonana na Mkurugenzi Mtendaji wa TCU, Kuomba aingilie kati dhuluma hii nifanye mitihani yangu.

Niliandika barua rasmi kwa mujibu wa Sheria za vyuo vikuu (Universities Regulation) ili TCU inisaidie haraka iwezekanavyo niendelee na mitihani, kwani . Mkurugenzi akasema niache barua atakaa na wanasheria wake kisha nitapewa mrejesho, nimeshinda TCU siku zote tatu bila ya majibu ya barua yangu.

Nilipofanya marejeo ya Maamuzi ya Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya tar.13 desember 2011 yaliyoelekeza Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kutufuta katika Mfumo wa Elimu nchini. Huenda haya yote yanayotokea sasa ni utekelezaji wa maazimio husika.
Watanzania, ifahamike kwamba ninaonewa, niliwahi muambia Prof. Rwekaza Mkandala kwamba, “Kumnyima mtoto wa masikini elimu, ni sawa na kumpiga risasi afe katika nchi yake.” Hakuna dhambi kuu niliyoitenda nchi hii, nikastahili adhabu ya kupokwa haki yangu ya kusoma ndani ya nchi hii milele.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ni chuo kikuu cha umma, ni chuo kilichojengwa na kodi za watanzania, ni chuo kilichojengwa na jasho la kila mtanzania. Hivyo kila mtanzania mwenye sifa kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria, anapaswa kusoma katika chuo hiki bila kubaguliwa.

Kuongoza Vyuo Vikuu kwa misingi ya Sheria
Mpaka sasa ninamifano ya Wanafunzi walioikimbia nchi hii na kuenda kusoma nje ya nchi kwa sababu ya ukiukwaji mkubwa wa Sheria ndani ya vyuo vikuu nchini. Natamani kuona nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii. Tukiendelea kuongoza vyuo vikuu , kwa visasi, kwa chuki binafsi, neno la mtu likawa sheria, watawala wa vyuo vikuu wakawa juu ya sheria, tutaliingiza taifa hili katika gharama za machafuko.

Hitimisho.
Nimetafakari sana, na kujiuliza maswali mengi watanzania, ninachokishuhudia katika maisha yangu ni kwamba; hawapambani na binadamu anayeitwa Alphonce Lusako, wanapambana na Elimu atayoipata Alphonce. Fimbo yao kuu, ni umasikini wangu na wazazi wangu, Kibinadamu masuala haya ni magumu sana, nimeona nimuache Mwenyezi Mungu apambane mwenyewe.

Aidha, niwashukuru viongozi wote wa dini walionipigia simu kutoka mikoa mbalimbali, wakinifariji, nachelea kusema, waliombee taifa kwani kunavijana wengi katika vyuo vikuu hutendwa kama ninavyotendwa. Niwashukuru wazazi wangu watambue kwamba haya ni mapito na yatapita, Niwashukuru Wanafunzi wenzangu wa UDSM, niseme neno moja tu (KWAHERINI), Niwashukuru wanasheria, ndugu na marafiki zangu walioshikamana name katika wakati huu, nachotaka niseme kwao ni kwamba, hatma ya maisha ya mwanadamu ipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu.
Matokeo ya kutumika kama ngazi. Mikopo wanyimwe wengine kugoma ukagome wewe. Haya ndio matatizo ya kutumika kama ngazi kwa ujira kiduchu. Waliokutuma uratibu hiyo migomo wako bungeni wewe unasaga lami umetumika kama taulo la gesti.

Vijana fikirieni future zenu na maendeleo yenu na familia zenu kwanza na pia fikirieni unachotaka kufanya kina impact gani katika maisha yenu ya sasa na baadae. Ona sasa kusoma husomi na maisha yamekupiga kisa siasa Pumbavu
 
Jitu limekiri kuratibu migomo vyuoni.Hilo limaonekana ni likorofi kweli.Chadema wangemlipia akaenda kusoma India,sio lazima asome UDSM.Mbona chadema wanamlipia lema mawakaili wanashindwa kumlipia shule huyo mbavicha aliekuwa akitekeleza kwa vitendo sera ya migomo?
 
Daaaah 2009 bado unapigana kuendelea na first degree wakati walioingia chuo 2013 Sasa hivi wamemaliza na wanafanya kazi"

Ila nashauri siasa isifanyike kwenye elimu walionyamaza wakapita chuo sio wajinga ......

Nchi yetu bado ina mfumo mbovu wa utawala wa Mwenye nguvu mpishe............

Nashauri vijana hasa kutoka familia masikini waende vyuoni kusoma tu ndio kazi inayowapeleka huko siasa na migomo waachieni wanasiasa..............

We have long way to go.......
Nakumbuka Baba yangu alinisindika siju nareport chuo, wosia wake ilikuwa nikifukuzwa kwa ajili ya kushiriki kugoma nisirudi nyumbani kwake
 
Back
Top Bottom