Alpha High School, je hamjui kuna bei elekezi?

Alpha High School, je hamjui kuna bei elekezi?

Hatutaki kuona tena foleni za mabasi na magari madogo toka Tanzania yakipeleka watoto Kenya na Uganda ili wakasome. Shule nzuri na elimu nzuri vinapatikana hapa Tanzania sasa, kwa gharama zinazolingana na kupeleka hao watoto Nairobi au Kampala. Lipi bora: wasome hapa kwa gharama kubwa au tupate aibu ya kuwasomba kila muhula kuwapeleka Kenya au Uganda wakasome kwa ghrama kubwa vile vile? Maana lazima wasome shule nzuri. Ni hiari yao, na kama hupendi hizo shule hulazimishwi.
 
Mtoa uzi,achana na huo uzi,labda kama mwanao hutak afaulu mtihan ila apate maarifa mengine,acha na mambo ya serikali kama mwanao anataka vyeti vyake vina A na Bs,wewe chagua shule inayofundisha vizur co kwa kutegemea bei elekez.Ada elekez labda shule za vichochoron,walimu wa masomo wanabadilishwa kila baada ya mwez mmoja.
 
Mwenye nyumba ukiona anakusumbua hama au jenga ya kwako.
 
Ni sawa na kung'ang'ania kununua kilo cha sukari elfu 10 kwenye maduka binafsi wakati maduka ya serikali ni elfu 2 na malalamiko ambayo siyo ya lazima unayapeleka serikalini
 
Hiyo ada ni kidogo sana kulinganisha na hii Dar international academy ambapo ada kwa sekondari ni zaidi ya 33m (USD 16000). Mtoa mada waache wenye misuli yao wasomeshe watoto wao hapo.
 
jk

Jk mtoto wake alisoma Kibaha boys usiongee kitu usichokijua
Hapo sijamtaja JK nimesema Magu,mtoto wake amepelekwa Feza.Soma ndugu uekewe usikurupuke.Mimi sijapinga wao kupeleka watoto wao kokote point ni kuwa wafanye/tufanye juhudi kuakikisha shule za serekali zinatoa elimu katika ubora wa hali ya juu
 
Unajua kampuni za soda zimetoa matangazo kila sehemu kuwa pepsi/coke ya chupa ni Tsh. 500/- tu, lakini ukienda Serena na kwingineko soda hiyo hiyo inauzwa Tsh. 3,000/- na hakuna anayelalamika!?
Ifike mahali Watz tujifunze na kuelewa maana ya thamani ya unachonunua (value for money) na haki ya mnunuzi badala ya kulialia.
 
Mheshimiwa waziri wa Elimu na Tamisemi je mnajua Gharama tunazotakiwa wazazi kulipa kama ada na michango mingine kwenye shule ya binafsi ya Alpha sekondari School iliyopo Mikocheni Dar es Salaam

Ada ziko juu sana ..ada ya mtoto anaetaka kukaa Bweni ni shs milini tano na laki sita...bado michango mingine mingine

Rais wetu mpendwa njoo utusaidie wananchi wako tunaimia sana pamoja na kuwa elimu ni haki ya kila mtanzania
Bei elekezi serikali si wameshalipinga suala hilo mkuu
 
Tofauti ni kuwa shule za serikali hazinunui mitihani ya necta na mwanafunzi anafaulu kwa akili na jitihada zake,no spoon feeding
Hizi ndo roho za kimasikini tunazosema.... mtu kama huna uwezo wa kulipia usipondee tena kwa kugeneralize, mbali na kumpeleka mtoto private schools kwa kigezo cha performance lakini private zenye kueleweka ukichanganya na malezi ya nyumbani mtoto anakua na vitu vingi special kuanzia kujiamini, talents, exposure N.k... elimu ni zaidi ya makaratasi ya vyeti. Mtu kama una uwezo kwa bora elimu iliyopo public schools peleka tu mtoto private especially elimu ya msingi ukijaaliwa unamaliza mpaka six na chuo unamtafutia scholarship nchi ya kueleweka akirudi nyumbani anakuja kuendeleza business za maana sio kukimbizana na take home za 450K
Money is b'ful... I am a very big fan of what money can do.
 
Bei elekezi serikali si wameshalipinga suala hilo mkuu
Ndo maana serikali ikaja na shule zake za kata ni uamuzi wako kumpeleka mtoto shule zenu za kujua kiingereza na milioni tano au kumpeleka kwenye shule za kata na nauli yake na sh 100 ya kula andazi mwisho wa siku mtihani ni mmoja ...chukua hatua
 
Hizi ndo roho za kimasikini tunazosema.... mtu kama huna uwezo wa kulipia usipondee tena kwa kugeneralize, mbali na kumpeleka mtoto private schools kwa kigezo cha performance lakini private zenye kueleweka ukichanganya na malezi ya nyumbani mtoto anakua na vitu vingi special kuanzia kujiamini, talents, exposure N.k... elimu ni zaidi ya makaratasi ya vyeti. Mtu kama una uwezo kwa bora elimu iliyopo public schools peleka tu mtoto private especially elimu ya msingi ukijaaliwa unamaliza mpaka six na chuo unamtafutia scholarship nchi ya kueleweka akirudi nyumbani anakuja kuendeleza business za maana sio kukimbizana na take home za 450K
Money is b'ful... I am a very big fan of what money can do.
Unamtafutia scholarship ya nini?Pambana kama mwanaume umsomeshe mtoto wako nje ya nchi huko.
 
Unamtafutia scholarship ya nini?Pambana kama mwanaume umsomeshe mtoto wako nje ya nchi huko.
Scholarships zipo ili zitumike.... tumia akili sio nguvu, kama mtoto ana uwezo why asipate scholarship??? Ikikosekana unapambana unalipa. But katika kila hatua kama kuna upenyo wa mwanangu kusoma comfortably @ good quality why not hustling for a scholarship?????
Kila mtu apambane na hali yake....
 
Back
Top Bottom