Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,490
- 32,193
Watu wengi wakisikia neno Almasi, wanawaza pesa, madini yale ya thamani magumu kabisa. Na watu wengi hawajui kwamba nyundo inaweza kupasuapasua vipande vipande almasi. Diamond is the hardess material but not the strongest. Yani ugumu wa diamond uko kwenye msuguano, hachubuki wala kuishiria haraka pale unapoitumia kusugua vitu. Lakini ukiongelea strength kwa kiswahili sijui ni nini, diamond inazidiwa hata na chuma. Ngoja twende kwenye mada yangu.
Teknolojia imekua sana kiasi kwamba binadamu anaweza kuzalisha almasi kwenye maabara. Kwa kawaida almasi huzalishwa chini ya ardhi pale inapotokea mgandamizomkubwa wa miamba na ikiwa kwenye mazingira ya joto kali. Ila binadamu sasa anaweza kuzalisha almasi kwa kutumia mashini maalum ambazo hutengeneza hali ya namna hiyo.
Mwanadada Maghan Markle, nadhani nyote mnafahamu, alionekana akiwa kavaa heleni za almasi wakati akikatiza mitaa ya London, Januari 2019. Almasi hizo zilikuwa ni za kuotesha na ilichukua siku tao tu kuziotesha.
Kampuni ya Kimai iliyoko huko Antwerp inatengeneza Almasi. Lakini swali ni je hizi Almasi ni za kweli ziko sawa kama almasi za kuchimba?
Jibu ni ndiyo hizi ni almasi kweli. Sifa zake za kikemia, muonekano wake ni sawa kabisa na almasi za kuchimbwa. Njia mbili hutumika katika kuotesha almasi. Na zote zinahusisha mgandamizo na joto kubwa.
Kutokana na maendeleo ya teknolojia, inagharimu $300 mpaka $500 kuzalisha carat moja ya almasi wakati mwaka 2008, iligharimu $4,000. Wataalam wa mambo wanasema wanaweza zitofautisha hizi aina mbili kwa uzoefu ila kwa mtu wa kawaida hawezi zitofautisha. Pia bei sokoni ya almasi ya kuchibwa ni kubwa sana kuliko ya kuzalishwa maabara.
Mimi ninasubiri teknolojia ya kutengeneza dhahabu niruke nayo.