Almanusura niolewe hotelini, mke wa mtu sumu

Tatizo ulikutana na mabaunsa wa chipsi yai na maji ya kiroba...... Ungekutana na mabaunsa poti sijui kama ungesimulia.....Ila ulipenda dezo mno huku kulipiwa lipiwa ujue na kuvaa shela mura....Japo vijana wamejifunza kitu.
 
mimi sina huruma na mwanamume anayetembea na mke wa mtu, halikadhalika mwanamke anayetembea na mume wa mtu, dawa yenu nyie ni kuliwa tu.
 
how can we proof kama kweli hawajakuoa?

Kwa kweli hakuna namna ya Ku proof kama huamini, isipokua Nina hoja chache tu

(1)nisingekua hata na kifua cha kuja hapa kusimulia huu mkasa kama ningelawitiwa,

(2) hata hapa kazini sina hakika sana kama ningekuwepo, ila nipo, jamaa ndie alimuachisha mkewe kazi kwa aibu, hiyo ni baada ya kushindwa kunifukuzisha kazi, na baadae nilifungua kesi ya kunitishia maisha kama nilivyoshauriwa na uongozi
Hiyo yote ni baada ya kushindwa kunilawiti kama alivyopanga

(3) wakurya huwa hatuna uoga wa kuogopa kifo, huwezi kujikunyata watu wakufire kisa unaogopa kufa, you have to fight, humu mjini watu wanainua vyuma mapambo ili kuvutia wanawake kimuonekano lakini nguvu kama nguvu hawana, nilijionea mwenyewe siku ya tukio, mmoja alienipiga roba nilimngangania kwa kumdandia hadi kuniachia, sasa baunsa wa ukweli huwezi kuitoa roba yake
Wawili kati ya mabaunsa wanne walikua wamejichubua uso kama wakongo, sasa kuna baunsa hapo, nilipata hofu mwanzo lakini nilipoanzisha mtiti wakalainika wenyewe na bahati nzuri msaada wa walinzi ukaja

(4) sikutahiriwa hospital
Nilitahiriwa porini bila ganzi, wakati ngariba anakata lile govi, huku anakuimbia wimbo wa kikurya kwamba ulizaliwa siku moja na utakufa siku moja, uoga wako ndio kifo chako,

Na kwa manufaa ya wengi mnaouliza hivi wanatoa wapi ushujaa!! Basi jibu lake ni hii tohara ya bila ganzi, tena hairuhusiwi kutahiriwa mtoto, ni kuanzia miaka 18+ ili usikie Yale maumivu na hupaswi kulia, ukilia tu unatangazwa kijiji kizima, wanawake wote wanaambiwa ulilia, huhesabiki kama umetahiriwa

Hata msaada wa walinzi usingekuja, nilikua tayari kupigana hadi mwisho hivyo hivyo huku wakinipiga, shida yao kubwa ilikua ni kunidhibiti, hicho ndicho walishindwa, nilikua tayari waje wabebe maiti yangu na sio kudhalilika
 
Pole sana,
ndo ujifunze kusoma alama ujue unasetiwa. Pia uwe unabadili hoteli mara kwa mara
Ungekuwa na manati ya mzungu hao mabaunsa unawaambia muoeni bosi wenu au nawapiga risasi maana nyie majambazi mmenivamia

ila mabausa wanne umewazidi nguvu..... labda kelele zilisaidia
 
Naona ume-edit baadhi ya maeneo

1. walikuvua boxer ila walipotaka kukupaka mafuta ukapata nguvu za ajabu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom