Almanusura niolewe hotelini, mke wa mtu sumu

john baptiste

Member
Nov 26, 2015
12
4
Wana jamvi nawasalim,

Mwaka 2013 nilitokea kumpenda Dada mmoja hapa kazini kwetu, alikua ni kiongozi ktk moja ya idara za hili shirika letu, hatukua tunafahamiana personally isipokua kwa kupishana Mara kwa Mara hapa mjengoni, yy flour ya 4 mm ya 6.

Uzuri wake hauna maelezo ya kawaida, hakua akivaa Pete hivyo nilidhani hajaolewa, pia ni msichana mwenye kujisikia sana na hubadilisha magari Mara kwa mara, kumbe mumewe ni mtu mwenye pesa, nilifahamu baadae.

Nikaweka mkakati kumnasa, wanaume wengi walimuogopa hasa jinsi ya kumuingia maana haongeai na wala hana ukaribu wa kijinga na wanaume, ila mm nikajitia kichaa nikajilipua, nikapokelewa kwa mikono miwili, hakutaka guest za kipumbavu, Mara zote tulienda hotelini na alilipa yy gharama zote, kula kunywa na mengineyo.

On that fateful day, huyu Dada hakuja kazini kwa siku tatu, wed, Thurs, and Friday, nilishtuka maana kila nikipiga simu hapokei ana jibu kwa sms tu kwa hizo siku tatu zote, ila Jumapili asubuhi ikaingia sms kuwa tuonane kule kule hotelini tunakoendaga mchana wa saa Tisa, nilipomuuliza mbona hupokei simu akajibu hakua anajisikia vizuri isitoshe mumewe alikua karibu.

Saa Nane na nusu akanipigia kuniuliza kama nimefika maeneo ya hotelini nikajibu ndio ila nipo nje nakusubiri, maana mlipaji siku zote huwa ni yy, nilishangaa alikua na sauti ya unyonge sana inayokatika katika, akafika akalipa akaingia room akaniita nami nikaingia.Alikua na michubuko mkononi na pia kama vile uso umekua mwekundu, akadai walikua na matatizo kidogo na mumewe nisijali sana.

Kila nikimwambia tuvue nguo sasa tuanze zoezi ananiuliza una haraka gani? Huku akiwa busy kuchati, muda kidogo, mlango unasukumwa watu nisiowafaham wanaingia chumbani na kufunga mlango, kumbe yule Dada huenda aliufungua kwa maksudi wakati nimeingia chooni, walikua watu wanne wenye muonekano wa kuinua vyuma na mmoja mwembamba ambae ndie Mume wa mpenzi wangu.

Walinivaa na kunikamata kwa nguvu na kunibana kiasi cha kushindwa kutikisa hata kichwa, yule Mume aliniambia tumekuja humu kukuoa, lazima tukukojolee na wewe, umeniumiza moyo kwa kipindi kirefu Leo ni zamu yako, mtoeni hiyo boxer mpakeni mafuta mumuoe watu wasije wakashtuka huko nje.

Baada ya Maneno hayo sikuwahi kuingiwa na nguvu kama siku hiyo, na sijui zilitoka wapi, nilikumbuka neno moja la baba yangu wakati natairiwa 1999 kule nyumbani musoma, nanukuu, nilitahiriwa ukubwani.

"" Leo mwanangu umetahiriwa na kisu bila ganzi na hukutoa machozi, umevuka kigezo cha ujasiri kwa mila zetu, lishinde lolote linalokuja mbele yako kama ulivyoyashinda maumivu ya kutahiriwa na kisu bila ganzi""

Nilimkamata jamaa alienipiga roba na kumdandia hadi kuniachia, niliwang'ata kwa meno kila alieleta mkono, nilirusha mateke hovyo bila mpangilio, tulisumbuana mle ndani kona moja hadi nyingine, nikaanza kupiga kelele weziii wezii kwa nguvu kubwa hadi walinzi na staff wa hotel na hotel manager wakaja na kugonga baada ya kusikia zile purukushani na kelele za weziii
Wakaweka chini ya ulinzi kwa kuleta fujo, nikaambiwa nivae, tulikua tunavuja damu wote na TV ikiwa vipande vipande, hali ya mule haikua inatamanika, walikua wamenidunda sana ingawa walishindwa kunithibiti, kumbe huwa ni woga tu unaofanya watu kulawitiwa, sikuogopa kabisa vitisho vya kuniua, niliwajibu nipo tayari kufa kuliko kuolewa.

Tukasombwa wote hadi polisi, kwa uharibifu wa Mali, yule jamaa baadae akatoa kiasi cha pesa kwa mhindi, watu wa hotel wakaondoka baada kuchukuliwa maelezo, baadae tukaachiwa wote na kuambiwa turudi pale Jumatatu asubuhi, OCD akasema huyu abaki kwa usalama wake, nikatoka Jumatatu, tukafanya mazungumzo pande zote, jamaa alikua akilia kwa hasira muda wote, akisema atanipata tu, vitisho vile vikachukuliwa kama ushahidi na akaonywa kwamba nikidhurika tu ni yy, akakataa kwenda mahakamani kwa ajili ugoni kama alivyoshauriwa.

Yaliendelea mengi sana baadae kwenye sakata hilo ambalo lilifika hadi kazini, lakini mwisho wa yote mungu alinishindia, nipo kazini hadi sasa, yule dada alizuiwa na mumewe kufanya kazi, sijui wanaendeleaje hadi sasa.

Hadi sasa najiuliza kwanini yule Dada aliamua kunisaliti na kunilengesha kiasi kile, akisahau mapenzi yote niliyompa aliyodai kakosa kwa mmewe, isitoshe mwanzo yeye mwenyewe alidai hajaolewa baadae ndipo akasema ukweli, na kwamba wao wasabato huwa hawavai Pete ndio maana sikuiona.

Naomba mjifunze mke wa mtu sumu.
 
huyo mungu kweli ni mungu na ndo maana unaandika mungu

back to the issue, we kweli muraaa, ungeolewa kama ungejirahisi, big up sana, kastori ni katamu
 
Ni story nzuri kwa wale wanaoingia kwenye game.

Kwani hawakuwa na communication codes? Anyway we learn through trials and errors with millions of miscalculations.
 
Hongera sana kaka kwa kuuvuka huo msala,ila nionavyo mim wanaume huwa tunafanya makosa sana mara tuonapo wake zetu na kukimbilia kwenda kushika ugoni bila kujiuliza kwa kina kuwa mim kama mwanaume nimesababishaje kutokee kwa usaliti ambao hapo awali haukuwepo.
Kwa upande mwingine wadada na akina mama ni wajibu wenu kukataa kujihusisha na mpenzi mwingine ili hari una mme anakupenda na kukuhudumia kila kitu,kama kuna mapungufu ndani ya ndoa tafteni ufumbuzi wa tatizo hilo kuliko kukimbilia kuisaliti ndoa.
 
Stori hii ni ndefu kama iliyoletwa jana lakini watu tumeisoma yote mpaka mwisho, jana kila mtu ndefu, ndefu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom