MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Wahenga walishawahi kunena kua "Uongo hufika kwa njia ya mkato lakini huishi kwa muda mfupi" na "Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele"
Leo asubuhi akihojiwa na kituo cha StarTV kwenye mjadala unaohusu hali ya kisiasa kwa ujumla nchinj DC wakinondoni ndugu Alli Hapi ametoa tafsiri ya neno Demokrasia kua ni "Ni kuwapatia wananchi huduma muhimu kama Maji,Afya,Elimu,barabara nk." Kwakweli nikaamini kua kuna watu hufanya makusudi kabisa kuuweka pembeni ukweli na kuamua kuongea tu ilimradi watu flani flani waridhike.
Hivi kweli ndugu Alli akikutana na mtoto wa darasa la tatu akamuuliza "Neno demokrasia lina maana gani? halafu huyu mtoto akajibiwa jibu kama hili ataelewa nini? hivi demokrasia ni kutimiza ahadi ulizoahidi kwa wananchi kweli? Kupeleka Umeme kijijini ni demokrasia? Demokrasia ina maana gani hasa?Abraham Lincoln ailiposema kua demokrasia ni utawala wa watu kwa ajili ya watu nkwa watu alimaanisha nini? Inamaana hata hili hulielewi kaka?
Hata Marehemu Muamar Gadafi wa Libya na Sadam Husein wa Iraq nao walikua wakiwapatia wananchi wao huduma zote tena kwa 100% mpaka mwingine aliwasaidia hata vijana kuona na kuwalipa pesa za matumizi wasiokua na kazi.Lakini wananchi hawa walikua wakilia kila siku kua hakuna Demokrasia, walilia kua hakuna Uhuru wa kufanya siasa,walilia kua hakuna Uhuru wa kuongea ama kukosoa serikali yao, walioonekana kupinga serikali waliitwa wachochezi na wengine kuitwa wahaini, wengine waliopinga serikali waliuawa,waliteswa,walifungwa na wengine walikimbilia uhamishoni.
Unachokiona Libya na Iraq kwa sasa ni kwa sababu wananchi walitaka Demokrasia na sio huduma za kijamii,kwa sababu walipatiwa kila walichotaka ispokua demokrasia tu.
Kiufupi ndugu yangu Alli Hapi wewe ni msomi mzuri sana na mjenga hoja mzuri, simamia ukweli huwezi kufukuzwa kazi kwa sababu ya kuusema. Kwa nafasi uliyonayo kwa sasa you are supposed to be focused and distinguished person na sio kuogopa kuusema ukweli.Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele na Uongo hufika kwa haraka ila huishi kwa muda mfupi.