Taarifa nilizozipata muda si mrefu zinasema kwamba mwanamuziki mwimbaji maarufu wa muziki wa dansi Ally Pugi amefariki dunia usiku wa kuamkia jana (12/6/2010) huko Morogoro alikokuwa amekwenda kusalimia ndugu zake. Marehemu Ally ambaye mpaka wakati kifo kinamkuta alikuwa mwimbaji wa bendi ya BRC (Bendi ambayo uwa inatumbuiza pale Port View siku ya Ijumaa) alikuwa akifanya shughuli za Muziki huko nchini Botswana kabla ya kujiunga na BRC January 2009. Marehemu Ally tayari amezikwa huko huko Morogoro.
Kwa sisi tuliopata nafasi ya kuwa naye karibu, kwa kweli alikuwa ni muimbaji mahiri. Mimi nilimpenda sana na hasa alipokuwa anaimba wimbo wa "Kinyonga". Ilikuwa ni lazima nikamtuze. Anyway yeye katangulia na wengine tunafuata!!!!

pole na wewe pia Bw Tiba kwa kuondokewa na mtu wako wa karibu
na mimi huyo jamaa alikuwa wa karibu sana, nilianza kumfahamu alipokuwa pale Knondoni Mkoko alipokuwa anapiga na Bantu group, niliishi nae pia pale Gaborone akiwa na Marehemu Abdalah "Dogodogo", Shaban "Wanted", Gregory, Maliki Star na baadae Kupaza na nilikuwa nae mwezi wa tatu this yr hapo Dar Pale maeneo ya MAwenzi Tabata walikuwa wanapiga pale,