Ally Kiba ni Messi, Diamond Ronaldo

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Nani mkali, Ali Kiba au Diamond?

Kuna mashabiki vindakindaki ukiwachokoza kwenye mada hiyo, wanaweza kurusha ngumi kwa kubishana. Wasanii hao wawili wameweza kutengeneza Simba na Yanga yao. Ni jambo jema sana kibiashara na maendeleo ya muziki.

Ukweli ni kwamba wote ni bora lakini nani zaidi? Kila mmoja ana ufundi wake, ni upi? Hapa nawachambua Ali Kiba na Diamond katika muktadha mpana ili kuonesha nani anashika nafasi ipi kwenye medani ya muziki Tanzania, Afrika na dunia kwa jumla.

Lionel Messi ni mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona ya Hispania, vilevile Timu ya Taifa ya Argentina. Cristiano Ronaldo anakipiga Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno. Kila mmoja ana ubora wake. Ni mafundi uwanjani na ni tegemeo la timu zao na ulimwengu mzima wa wapenda soka.

Kwa zama hizi ni wao tu! Awamu za akina Ronaldo de Lima &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];The Phenomeno', Zinedine Zidane, David Beckham, Rivaldo, Ronaldinho Gaucho, Thierry Henry na wengine zilishapita katika vipindi tofauti. Ni kama ambavyo George Weah alivyofuata baada ya Maradona, Gabriel Batistuta ambao walitanguliwa na akina Eusébio, Garrincha, Pele na wengine wengi.

Ni kama ambavyo wakati Gerd Müller wa Ujerumani akitisha kwa magoli, hakuna kizazi cha sasa aliyekuwepo uwanjani anacheza. Kwa kifupi ni mpango wa kupokezana vijiti. Kwa maana hiyo, huu ni wakati wa Messi na Ronaldo. Wapo wengi wakali wanaotikisa kwa sasa, ila pale juu wanaonekana wao zaidi.

Vivyo hivyo kwa Bongo Flava, wapo wakali wanaotikisa. Heshima yao ni kubwa na muziki wao ni mzuri, ila imetokea kuwepo kwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];uspesho' fulani kwa Diamond na Ali Kiba. Hivyo basi, nao watapita siku jioni yao ikiwadia na kijiti hicho kitapokelewa na wengine.

Zilishakuwepo zama ambazo muziki wa Tanzania utaongea nini mbele ya Inspector Haroun. Ukaja muda ambao soko lote la Bongo Flava lilihamia kwa Juma Nature. Ni yeye ndiye aliyejaza kumbi za burudani, utaongea nini?

Usisahau kuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, Juma Nature na Inspector Haroun walikuwa kama Simba na Yanga kutokana na upinzani wao. Ni kama ambavyo baada ya Profesa Jay kung'ara akiwa na Kundi la Hard Blasterz Crew (HBC) hasa alipoanza kufanya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];project' binafsi, watu wakaanza kumshindanisha na mkongwe Sugu &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Mr. II'. Kushindanisha haikwepeki!

Watawala kibao walishapita kwenye huu muziki wa Bongo Flava. Ilikuwa zaidi ya shida Mr. Nice aliposhika mpini. Zama za Dully Sykes utaongea nini wewe? Walishatawala akina Q Chillah, TID, MB Dog, Ferouz, Daz Baba (Daz Nundaz), Matonya, Joslin, Dudubaya, Solid Ground Family, Mandojo na Domokaya, Wagosi wa Kaya na wengine wengi ambao jioni yao iliwadia.

DIAMOND NI NAMBA MOJA BONGO?

Ni ukweli kwamba Diamond ameshapiga hatua na amekuwa bora sana katika kutumia fursa ili kufika mbali zaidi (anastahili pongezi za kipekee). Ila inaposemwa kuwa yeye ni namba moja nchini, hiyo haiwezi kuwa sahihi.

Ubora wa mwanamuziki hauwezi kutafsiriwa kwa kupanda sana ndege kwenda Ulaya, Marekani, Asia na kwingineko. Vilevile haupimwi kwa kufanya shoo nyingi na kulipwa pesa nyingi. Ubora wa mwanamuziki ni utunzi na uimbaji wa nyimbo zinazoishi ndani ya watu pamoja na kutengeneza mashabiki damu.

Juma Nature alitisha kwa mashabiki lakini hakuwahi kuwa msanii mkubwa kwa Profesa Jay au Sugu. Ja Rule alipoliteka soko la Hip Hop Marekani hakuwa mkubwa kwa DMX, vilevile Mase pamoja na kung'ara kibiashara lakini hakutambulika kama mkubwa kwa P Diddy, vivyo hivyo 50 Cent kwa Snoop au kinara wa mauzo ya Hip Hop duniani, Eminem mbele ya Jay Z.

Hapa pia nifafanue kuwa ukongwe hauna maana ya ukubwa kimuziki. Inawezekana umri wako ni mkubwa au umeanza fani muda mfupi lakini kazi yako ni ndogo, kwa hiyo wewe siyo msanii mkubwa.

Kadhalika, inawezekana ukawa msanii mdogo kiumri lakini kazi unayofanya ni kubwa, hapo utaitwa msanii mkubwa. Michael Jackson alipoitwa Mfalme wa Pop, kulikuwa na watangulizi wake wenye umri mkubwa lakini kikazi MJ aliwafunika.

Tupac Shakur na Notorious BIG walikuwa wadogo na walikufa wakiwa na umri mdogo lakini mapinduzi waliyoyafanya kwenye muziki wa Hip Hop hasa kibiashara, leo hii wanapotajwa, moja kwa moja unakuwa unazungumzia wasanii wakubwa sana kuwahi kutokea. Ni kazi tu!

Tukirejea kwa muktadha wetu ni kwamba hata aina ya wanamuziki ambao Diamond ameshashirikiana nao kimataifa, hawampi hadhi kwamba yeye ni namba moja. Anayo kazi ya kuendelea kufanya ili nyakati zije kumtambulisha kwa vigezo stahili. Umri au uchanga kazini siyo kitu, kazi yake ikiwa kubwa itampendelea na kumpa hadhi anayotaka!

Hivi karibuni, Diamond alihojiwa kuhusu uhusiano wake na Ali Kiba, nilishangazwa sana na tamko la Diamond lililokosa woga kuwa yupo tayari kumsaidia Ali Kiba kwa kufanya naye &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];kolabo' kwa vile yeye ameshapiga hatua.

Swali; Hiyo hatua aliyopiga Diamond ni kumzidi Ali Kiba? Inaonekana Diamond anamchukulia Ali Kiba kama akina Rich Mavoko, Barnaba, Shetta, Ben Pol na wengine ambao wanahitaji nguvu ya wasanii wa nje kuchomoza nje ya mipaka ya Tanzania.

Diamond ameshafanya kazi na Davido, Iyanya, Tiwa Savage na Mafikizolo. Wote hao kwa kiwango cha kimataifa, bado wanahangaikia ukubwa katika fani kwa sababu bado wadogo sana ukilinganisha na wakubwa wengi ambao sisi tunawajua.

Ali Kiba kupitia &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];project' ya One8, aliweza kurekodi na wasanii wengi wakubwa Afrika na dunia kwa jumla. Diamond anashindwa kuheshimu nafasi ya Ali Kiba kurekodi wimbo na Mfalme wa R&B asiyepingika duniani, R. Kelly.

Wasanii waliofanya kazi na Diamond, hata mmoja hafikii daraja la 2Face na Fally Ipupa. Kwa hapo utakuwa na nafasi ya kuwaza, Diamond amsaidie Ali Kiba kumpeleka wapi, ikiwa kama nafasi ya kufanya kazi hamfikii.

Jawabu la Diamond likanifanya nibaini kuwa kumbe &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];bwa mdogo' anajiona namba moja Tanzania. Hapohapo nikajiuliza, hivi Diamond anajua kuwa Lady Jaydee alishaimba na Oliver Mtukudzi? Je, Diamond anajua ukubwa wa Mtukudzi? Anaweza kumlinganisha na akina Iyanya na Davido au Mafikizolo?

Je, Diamond anajua kuwa AY ameshafanya kazi na Lil Romeo na Sean Kingston. Anatambua uwezo wa watu hao katika soko la muziki Marekani na duniani kwa nyakati zao?

ALI KIBA NA DIAMOND, NANI NI NANI?

Turejee kwa Ronaldo na Messi. Ni kwamba wote ni bora lakini kwa kuwatazama tu aina ya uhusika wao uwanjani, Messi ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, yaani alizaliwa awe staa wa soka, misingi na mazoezi yamemfikisha pakubwa sana.

Ronaldo vilevile ana kipaji lakini hakifikii kile cha Messi. Ronaldo ana bidii kubwa kwenye mafunzo na mazoezi. Wanasema "hard work pays off", yaani bidii inalipa. Juhudi ya Ronaldo inamfanya kuwa mwanasoka bora sana.

Hata ukiutazama mwili wa Messi, hauna miraba ya mazoezi kama ilivyo kwa Ronaldo. Ni mastaa wakubwa wawili wa soka duniani, mmoja anatamba kwa sababu ya kipaji kikubwa alichojaliwa na Mungu, mwenzake anatembea kifua mbele kutokana na bidii yake ya mazoezi.

Ali Kiba ni Messi. Ana kipaji kikubwa, amejaliwa sauti nzuri ambayo kama asingechagua muziki, sijui angeifanyia nini. Kwa mantiki hiyo, kinachombeba ni kipaji zaidi kuliko jitihada za kujitangaza.

Ali Kiba kwa muda mrefu aliamini katika kuandika mashairi, kutengeneza sauti inayovutia kisha mashabiki watapenda tu kazi. Kipaji chake kikamfanya akubalike na kufika alipofika.

Diamond ni Ronaldo. Alipoanza muziki akaamua kujiongeza kwamba bidii yake inaweza kumfikisha pazuri. Alihangaika mno kujitangaza, akawa anafanya kazi sana, mazoezi ya kuhakikisha shoo zake zinakuwa bora.

Diamond akawa mtundu wa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];kucheza' na media. Wanasema juhudi huvuta bahati, bidii yake ikamfanya awe msanii anayependwa sana, akaoneshwa njia nyingi akazifikia, akawa anacheza na vyombo vya habari, mwisho akawa Platnumz kweli!

MAKOSA:

Ali Kiba alipokuwa anang'ara sana, alisahau msingi wake kuwa ni Watanzania. Akawa anapanda sana ndege kwenda kufanya ziara nje, akaharibu soko lake la nyumbani. Hata kwenye vyombo vya habari akawa hapatikani. Waandishi wakimsaka kwa ajili ya mahojiano, anakuwa mgumu kutoa ushirikiano.

Si kweli kwamba Ali Kiba aliwahi kukaa kimya kwa miaka mitatu eti ndiyo Diamond akatamba. Januari mwaka juzi (2012), alitoa Single Boy akimshirikisha Lady Jaydee. Novemba 2012, alitoa My Everything baadaye akafanya project na mdogo wake, Abdu Kiba, ila hakuweza kukaa vizuri sokoni.

Mwana imemrudisha sokoni na Watanzania wameamua kumpa nafasi nyingine ya kutamba. Alipoangukia Ali Kiba ndipo Diamond alipojikwaa. Baada ya kufanya kolabo na akina Davido na kushiriki tuzo za BET na MTV, amesahau soko la nyumbani.

Mbwembwe zikawa nyingi, kila siku &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];anabodi' kwenda nje kupiga shoo mshenzi, nyingine anaishia kupigwa mawe, Watanzania waliomuweka pale juu hawamuoni shoo za nyumbani. Mapromota wa nyumbani waliomuwezesha kuwa alipo, walipomtafuta anawaringia.

Diamond aliyekubalika na kupendwa na watu ni mnyenyekevu, mtu wa watu, ila wa sasa ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];bwana misifa' kuliko Dully, utadhani watu wataacha kumzomea? Ni hoja dhaifu kusema wazomeaji walitengenezwa.

Huko nyuma, kuna vikundi vilishapanga kumzomea Diamond kwenye shoo zake lakini vilizidiwa nguvu na umati mkubwa uliokuwa unamshangilia. Rejea mwaka jana Maisha Club hali ilivyokuwa, jiulize kwa nini kwenye Fiesta wazomeaji waliwazidi washangiliaji?

Ali Kiba na Diamond wote ni wadogo zangu. Ali Kiba kwa ujio wake asafishe makosa. Aheshimu vyombo vya habari na mashabiki wake. Huu ni muda wa kutengeneza fedha. Diamond azinduke mapema, akiamini alizomewa kwa mipango, atazidi kufeli. Agutuke mapema na kusahihisha makosa.

See: original version from Luqman Maloto
 
Nimependa sana ufafanuzi wako.Na hata diamond kipindi anafanya interview na sporah alisema anaamini hard work ndio imemfikisha hapo na kuwa yeye haamini mambo ya talent and same applied kwa kiba yeye naona anaamini kwenye talent ila hard work hana.Kiukweli wote wanaimba vizuri na wote wana mapungufu yao ambayo management zao inatakiwa iyatatue.
 
kweli kabisa aunty
ila ngoja wale ffffffff uone!!
 
Nani mkali, Ali Kiba au Diamond?

Kuna mashabiki vindakindaki ukiwachokoza kwenye mada hiyo, wanaweza kurusha ngumi kwa kubishana. Wasanii hao wawili wameweza kutengeneza Simba na Yanga yao. Ni jambo jema sana kibiashara na maendeleo ya muziki.

Ukweli ni kwamba wote ni bora lakini nani zaidi? Kila mmoja ana ufundi wake, ni upi? Hapa nawachambua Ali Kiba na Diamond katika muktadha mpana ili kuonesha nani anashika nafasi ipi kwenye medani ya muziki Tanzania, Afrika na dunia kwa jumla.

Lionel Messi ni mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona ya Hispania, vilevile Timu ya Taifa ya Argentina. Cristiano Ronaldo anakipiga Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno. Kila mmoja ana ubora wake. Ni mafundi uwanjani na ni tegemeo la timu zao na ulimwengu mzima wa wapenda soka.

Kwa zama hizi ni wao tu! Awamu za akina Ronaldo de Lima ‘The Phenomeno’, Zinedine Zidane, David Beckham, Rivaldo, Ronaldinho Gaucho, Thierry Henry na wengine zilishapita katika vipindi tofauti. Ni kama ambavyo George Weah alivyofuata baada ya Maradona, Gabriel Batistuta ambao walitanguliwa na akina Eusébio, Garrincha, Pele na wengine wengi.

Ni kama ambavyo wakati Gerd Müller wa Ujerumani akitisha kwa magoli, hakuna kizazi cha sasa aliyekuwepo uwanjani anacheza. Kwa kifupi ni mpango wa kupokezana vijiti. Kwa maana hiyo, huu ni wakati wa Messi na Ronaldo. Wapo wengi wakali wanaotikisa kwa sasa, ila pale juu wanaonekana wao zaidi.
Vivyo hivyo kwa Bongo Flava, wapo wakali wanaotikisa. Heshima yao ni kubwa na muziki wao ni mzuri, ila imetokea kuwepo kwa ‘uspesho’ fulani kwa Diamond na Ali Kiba. Hivyo basi, nao watapita siku jioni yao ikiwadia na kijiti hicho kitapokelewa na wengine.

Zilishakuwepo zama ambazo muziki wa Tanzania utaongea nini mbele ya Inspector Haroun. Ukaja muda ambao soko lote la Bongo Flava lilihamia kwa Juma Nature. Ni yeye ndiye aliyejaza kumbi za burudani, utaongea nini?

Usisahau kuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, Juma Nature na Inspector Haroun walikuwa kama Simba na Yanga kutokana na upinzani wao. Ni kama ambavyo baada ya Profesa Jay kung’ara akiwa na Kundi la Hard Blasterz Crew (HBC) hasa alipoanza kufanya ‘project’ binafsi, watu wakaanza kumshindanisha na mkongwe Sugu ‘Mr. II’. Kushindanisha haikwepeki!

Watawala kibao walishapita kwenye huu muziki wa Bongo Flava. Ilikuwa zaidi ya shida Mr. Nice aliposhika mpini. Zama za Dully Sykes utaongea nini wewe? Walishatawala akina Q Chillah, TID, MB Dog, Ferouz, Daz Baba (Daz Nundaz), Matonya, Joslin, Dudubaya, Solid Ground Family, Mandojo na Domokaya, Wagosi wa Kaya na wengine wengi ambao jioni yao iliwadia.

DIAMOND NI NAMBA MOJA BONGO?

Ni ukweli kwamba Diamond ameshapiga hatua na amekuwa bora sana katika kutumia fursa ili kufika mbali zaidi (anastahili pongezi za kipekee). Ila inaposemwa kuwa yeye ni namba moja nchini, hiyo haiwezi kuwa sahihi.
Ubora wa mwanamuziki hauwezi kutafsiriwa kwa kupanda sana ndege kwenda Ulaya, Marekani, Asia na kwingineko. Vilevile haupimwi kwa kufanya shoo nyingi na kulipwa pesa nyingi. Ubora wa mwanamuziki ni utunzi na uimbaji wa nyimbo zinazoishi ndani ya watu pamoja na kutengeneza mashabiki damu.

Juma Nature alitisha kwa mashabiki lakini hakuwahi kuwa msanii mkubwa kwa Profesa Jay au Sugu. Ja Rule alipoliteka soko la Hip Hop Marekani hakuwa mkubwa kwa DMX, vilevile Mase pamoja na kung’ara kibiashara lakini hakutambulika kama mkubwa kwa P Diddy, vivyo hivyo 50 Cent kwa Snoop au kinara wa mauzo ya Hip Hop duniani, Eminem mbele ya Jay Z.

Hapa pia nifafanue kuwa ukongwe hauna maana ya ukubwa kimuziki. Inawezekana umri wako ni mkubwa au umeanza fani muda mfupi lakini kazi yako ni ndogo, kwa hiyo wewe siyo msanii mkubwa.
Kadhalika, inawezekana ukawa msanii mdogo kiumri lakini kazi unayofanya ni kubwa, hapo utaitwa msanii mkubwa. Michael Jackson alipoitwa Mfalme wa Pop, kulikuwa na watangulizi wake wenye umri mkubwa lakini kikazi MJ aliwafunika.

Tupac Shakur na Notorious BIG walikuwa wadogo na walikufa wakiwa na umri mdogo lakini mapinduzi waliyoyafanya kwenye muziki wa Hip Hop hasa kibiashara, leo hii wanapotajwa, moja kwa moja unakuwa unazungumzia wasanii wakubwa sana kuwahi kutokea. Ni kazi tu!

Tukirejea kwa muktadha wetu ni kwamba hata aina ya wanamuziki ambao Diamond ameshashirikiana nao kimataifa, hawampi hadhi kwamba yeye ni namba moja. Anayo kazi ya kuendelea kufanya ili nyakati zije kumtambulisha kwa vigezo stahili. Umri au uchanga kazini siyo kitu, kazi yake ikiwa kubwa itampendelea na kumpa hadhi anayotaka!

Hivi karibuni, Diamond alihojiwa kuhusu uhusiano wake na Ali Kiba, nilishangazwa sana na tamko la Diamond lililokosa woga kuwa yupo tayari kumsaidia Ali Kiba kwa kufanya naye ‘kolabo’ kwa vile yeye ameshapiga hatua.
Swali; Hiyo hatua aliyopiga Diamond ni kumzidi Ali Kiba? Inaonekana Diamond anamchukulia Ali Kiba kama akina Rich Mavoko, Barnaba, Shetta, Ben Pol na wengine ambao wanahitaji nguvu ya wasanii wa nje kuchomoza nje ya mipaka ya Tanzania.

Diamond ameshafanya kazi na Davido, Iyanya, Tiwa Savage na Mafikizolo. Wote hao kwa kiwango cha kimataifa, bado wanahangaikia ukubwa katika fani kwa sababu bado wadogo sana ukilinganisha na wakubwa wengi ambao sisi tunawajua.

Ali Kiba kupitia ‘project’ ya One8, aliweza kurekodi na wasanii wengi wakubwa Afrika na dunia kwa jumla. Diamond anashindwa kuheshimu nafasi ya Ali Kiba kurekodi wimbo na Mfalme wa R&B asiyepingika duniani, R. Kelly.

Wasanii waliofanya kazi na Diamond, hata mmoja hafikii daraja la 2Face na Fally Ipupa. Kwa hapo utakuwa na nafasi ya kuwaza, Diamond amsaidie Ali Kiba kumpeleka wapi, ikiwa kama nafasi ya kufanya kazi hamfikii.
Jawabu la Diamond likanifanya nibaini kuwa kumbe ‘bwa mdogo’ anajiona namba moja Tanzania. Hapohapo nikajiuliza, hivi Diamond anajua kuwa Lady Jaydee alishaimba na Oliver Mtukudzi? Je, Diamond anajua ukubwa wa Mtukudzi? Anaweza kumlinganisha na akina Iyanya na Davido au Mafikizolo?

Je, Diamond anajua kuwa AY ameshafanya kazi na Lil Romeo na Sean Kingston. Atambua uwezo wa watu hao katika soko la muziki Marekani na duniani kwa nyakati zao?

ALI KIBA NA DIAMOND, NANI NI NANI?

Turejee kwa Ronaldo na Messi. Ni kwamba wote ni bora lakini kwa kuwatazama tu aina ya uhusika wao uwanjani, Messi ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, yaani alizaliwa awe staa wa soka, misingi na mazoezi yamemfikisha pakubwa sana.

Ronaldo vilevile ana kipaji lakini hakifikii kile cha Messi. Ronaldo ana bidii kubwa kwenye mafunzo na mazoezi. Wanasema “hard work pays off”, yaani bidii inalipa. Juhudi ya Ronaldo inamfanya kuwa mwanasoka bora sana.
Hata ukiutazama mwili wa Messi, hauna miraba ya mazoezi kama ilivyo kwa Ronaldo. Ni mastaa wakubwa wawili wa soka duniani, mmoja anatamba kwa sababu ya kipaji kikubwa alichojaliwa na Mungu, mwenzake anatembea kifua mbele kutokana na bidii yake ya mazoezi.

Ali Kiba ni Messi. Ana kipaji kikubwa, amejaliwa sauti nzuri ambayo kama asingechagua muziki, sijui angeifanyia nini. Kwa mantiki hiyo, kinachombeba ni kipaji zaidi kuliko jitihada za kujitangaza.
Ali Kiba kwa muda mrefu aliamini katika kuandika mashairi, kutengeneza sauti inayovutia kisha mashabiki watapenda tu kazi. Kipaji chake kikamfanya akubalike na kufika alipofika.

Diamond ni Ronaldo. Alipoanza muziki akaamua kujiongeza kwamba bidii yake inaweza kumfikisha pazuri. Alihangaika mno kujitangaza, akawa anafanya kazi sana, mazoezi ya kuhakikisha shoo zake zinakuwa bora.
Diamond akawa mtundu wa ‘kucheza’ na media. Wanasema juhudi huvuta bahati, bidii yake ikamfanya awe msanii anayependwa sana, akaoneshwa njia nyingi akazifikia, akawa anacheza na vyombo vya habari, mwisho akawa Platnumz kweli!

MAKOSA:

Ali Kiba alipokuwa anang’ara sana, alisahau msingi wake kuwa ni Watanzania. Akawa anapanda sana ndege kwenda kufanya ziara nje, akaharibu soko lake la nyumbani. Hata kwenye vyombo vya habari akawa hapatikani. Waandishi wakimsaka kwa ajili ya mahojiano, anakuwa mgumu kutoa ushirikiano.

Si kweli kwamba Ali Kiba aliwahi kukaa kimya kwa miaka mitatu eti ndiyo Diamond akatamba. Januari mwaka juzi (2012), alitoa Single Boy akimshirikisha Lady Jaydee. Novemba 2012, alitoa My Everything baadaye akafanya project na mdogo wake, Abdu Kiba, ila hakuweza kukaa vizuri sokoni.

Mwana imemrudisha sokoni na Watanzania wameamua kumpa nafasi nyingine ya kutamba. Alipoangukia Ali Kiba ndipo Diamond alipojikwaa. Baada ya kufanya kolabo na akina Davido na kushiriki tuzo za BET na MTV, amesahau soko la nyumbani.

Mbwembwe zikawa nyingi, kila siku ‘anabodi’ kwenda nje kupiga shoo mshenzi, nyingine anaishia kupigwa mawe, Watanzania waliomuweka pale juu hawamuoni shoo za nyumbani. Mapromota wa nyumbani waliomuwezesha kuwa alipo, walipomtafuta anawaringia.

Diamond aliyekubalika na kupendwa na watu ni mnyenyekevu, mtu wa watu, ila wa sasa ni ‘bwana misifa’ kuliko Dully, utadhani watu wataacha kumzomea? Ni hoja dhaifu kusema wazomeaji walitengenezwa.

Huko nyuma, kuna vikundi vilishapanga kumzomea Diamond kwenye shoo zake lakini vilizidiwa nguvu na umati mkubwa uliokuwa unamshangilia. Rejea mwaka jana Maisha Club hali ilivyokuwa, jiulize kwa nini kwenye Fiesta wazomeaji waliwazidi washangiliaji?

Ali Kiba na Diamond wote ni wadogo zangu. Ali Kiba kwa ujio wake asafishe makosa. Aheshimu vyombo vya habari na mashabiki wake. Huu ni muda wa kutengeneza fedha. Diamond azinduke mapema, akiamini alizomewa kwa mipango, atazidi kufeli. Agutuke mapema na kusahihisha makosa.

great analysis
 
Nani mkali, Ali Kiba au Diamond?

Kuna mashabiki vindakindaki ukiwachokoza kwenye mada hiyo, wanaweza kurusha ngumi kwa kubishana. Wasanii hao wawili wameweza kutengeneza Simba na Yanga yao. Ni jambo jema sana kibiashara na maendeleo ya muziki.

Ukweli ni kwamba wote ni bora lakini nani zaidi? Kila mmoja ana ufundi wake, ni upi? Hapa nawachambua Ali Kiba na Diamond katika muktadha mpana ili kuonesha nani anashika nafasi ipi kwenye medani ya muziki Tanzania, Afrika na dunia kwa jumla.

Lionel Messi ni mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona ya Hispania, vilevile Timu ya Taifa ya Argentina. Cristiano Ronaldo anakipiga Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno. Kila mmoja ana ubora wake. Ni mafundi uwanjani na ni tegemeo la timu zao na ulimwengu mzima wa wapenda soka.

Kwa zama hizi ni wao tu! Awamu za akina Ronaldo de Lima ‘The Phenomeno', Zinedine Zidane, David Beckham, Rivaldo, Ronaldinho Gaucho, Thierry Henry na wengine zilishapita katika vipindi tofauti. Ni kama ambavyo George Weah alivyofuata baada ya Maradona, Gabriel Batistuta ambao walitanguliwa na akina Eusébio, Garrincha, Pele na wengine wengi.

Ni kama ambavyo wakati Gerd Müller wa Ujerumani akitisha kwa magoli, hakuna kizazi cha sasa aliyekuwepo uwanjani anacheza. Kwa kifupi ni mpango wa kupokezana vijiti. Kwa maana hiyo, huu ni wakati wa Messi na Ronaldo. Wapo wengi wakali wanaotikisa kwa sasa, ila pale juu wanaonekana wao zaidi.
Vivyo hivyo kwa Bongo Flava, wapo wakali wanaotikisa. Heshima yao ni kubwa na muziki wao ni mzuri, ila imetokea kuwepo kwa ‘uspesho' fulani kwa Diamond na Ali Kiba. Hivyo basi, nao watapita siku jioni yao ikiwadia na kijiti hicho kitapokelewa na wengine.

Zilishakuwepo zama ambazo muziki wa Tanzania utaongea nini mbele ya Inspector Haroun. Ukaja muda ambao soko lote la Bongo Flava lilihamia kwa Juma Nature. Ni yeye ndiye aliyejaza kumbi za burudani, utaongea nini?

Usisahau kuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, Juma Nature na Inspector Haroun walikuwa kama Simba na Yanga kutokana na upinzani wao. Ni kama ambavyo baada ya Profesa Jay kung'ara akiwa na Kundi la Hard Blasterz Crew (HBC) hasa alipoanza kufanya ‘project' binafsi, watu wakaanza kumshindanisha na mkongwe Sugu ‘Mr. II'. Kushindanisha haikwepeki!

Watawala kibao walishapita kwenye huu muziki wa Bongo Flava. Ilikuwa zaidi ya shida Mr. Nice aliposhika mpini. Zama za Dully Sykes utaongea nini wewe? Walishatawala akina Q Chillah, TID, MB Dog, Ferouz, Daz Baba (Daz Nundaz), Matonya, Joslin, Dudubaya, Solid Ground Family, Mandojo na Domokaya, Wagosi wa Kaya na wengine wengi ambao jioni yao iliwadia.

DIAMOND NI NAMBA MOJA BONGO?

Ni ukweli kwamba Diamond ameshapiga hatua na amekuwa bora sana katika kutumia fursa ili kufika mbali zaidi (anastahili pongezi za kipekee). Ila inaposemwa kuwa yeye ni namba moja nchini, hiyo haiwezi kuwa sahihi.
Ubora wa mwanamuziki hauwezi kutafsiriwa kwa kupanda sana ndege kwenda Ulaya, Marekani, Asia na kwingineko. Vilevile haupimwi kwa kufanya shoo nyingi na kulipwa pesa nyingi. Ubora wa mwanamuziki ni utunzi na uimbaji wa nyimbo zinazoishi ndani ya watu pamoja na kutengeneza mashabiki damu.

Juma Nature alitisha kwa mashabiki lakini hakuwahi kuwa msanii mkubwa kwa Profesa Jay au Sugu. Ja Rule alipoliteka soko la Hip Hop Marekani hakuwa mkubwa kwa DMX, vilevile Mase pamoja na kung'ara kibiashara lakini hakutambulika kama mkubwa kwa P Diddy, vivyo hivyo 50 Cent kwa Snoop au kinara wa mauzo ya Hip Hop duniani, Eminem mbele ya Jay Z.

Hapa pia nifafanue kuwa ukongwe hauna maana ya ukubwa kimuziki. Inawezekana umri wako ni mkubwa au umeanza fani muda mfupi lakini kazi yako ni ndogo, kwa hiyo wewe siyo msanii mkubwa.
Kadhalika, inawezekana ukawa msanii mdogo kiumri lakini kazi unayofanya ni kubwa, hapo utaitwa msanii mkubwa. Michael Jackson alipoitwa Mfalme wa Pop, kulikuwa na watangulizi wake wenye umri mkubwa lakini kikazi MJ aliwafunika.

Tupac Shakur na Notorious BIG walikuwa wadogo na walikufa wakiwa na umri mdogo lakini mapinduzi waliyoyafanya kwenye muziki wa Hip Hop hasa kibiashara, leo hii wanapotajwa, moja kwa moja unakuwa unazungumzia wasanii wakubwa sana kuwahi kutokea. Ni kazi tu!

Tukirejea kwa muktadha wetu ni kwamba hata aina ya wanamuziki ambao Diamond ameshashirikiana nao kimataifa, hawampi hadhi kwamba yeye ni namba moja. Anayo kazi ya kuendelea kufanya ili nyakati zije kumtambulisha kwa vigezo stahili. Umri au uchanga kazini siyo kitu, kazi yake ikiwa kubwa itampendelea na kumpa hadhi anayotaka!

Hivi karibuni, Diamond alihojiwa kuhusu uhusiano wake na Ali Kiba, nilishangazwa sana na tamko la Diamond lililokosa woga kuwa yupo tayari kumsaidia Ali Kiba kwa kufanya naye ‘kolabo' kwa vile yeye ameshapiga hatua.
Swali; Hiyo hatua aliyopiga Diamond ni kumzidi Ali Kiba? Inaonekana Diamond anamchukulia Ali Kiba kama akina Rich Mavoko, Barnaba, Shetta, Ben Pol na wengine ambao wanahitaji nguvu ya wasanii wa nje kuchomoza nje ya mipaka ya Tanzania.

Diamond ameshafanya kazi na Davido, Iyanya, Tiwa Savage na Mafikizolo. Wote hao kwa kiwango cha kimataifa, bado wanahangaikia ukubwa katika fani kwa sababu bado wadogo sana ukilinganisha na wakubwa wengi ambao sisi tunawajua.

Ali Kiba kupitia ‘project' ya One8, aliweza kurekodi na wasanii wengi wakubwa Afrika na dunia kwa jumla. Diamond anashindwa kuheshimu nafasi ya Ali Kiba kurekodi wimbo na Mfalme wa R&B asiyepingika duniani, R. Kelly.

Wasanii waliofanya kazi na Diamond, hata mmoja hafikii daraja la 2Face na Fally Ipupa. Kwa hapo utakuwa na nafasi ya kuwaza, Diamond amsaidie Ali Kiba kumpeleka wapi, ikiwa kama nafasi ya kufanya kazi hamfikii.
Jawabu la Diamond likanifanya nibaini kuwa kumbe ‘bwa mdogo' anajiona namba moja Tanzania. Hapohapo nikajiuliza, hivi Diamond anajua kuwa Lady Jaydee alishaimba na Oliver Mtukudzi? Je, Diamond anajua ukubwa wa Mtukudzi? Anaweza kumlinganisha na akina Iyanya na Davido au Mafikizolo?

Je, Diamond anajua kuwa AY ameshafanya kazi na Lil Romeo na Sean Kingston. Atambua uwezo wa watu hao katika soko la muziki Marekani na duniani kwa nyakati zao?

ALI KIBA NA DIAMOND, NANI NI NANI?

Turejee kwa Ronaldo na Messi. Ni kwamba wote ni bora lakini kwa kuwatazama tu aina ya uhusika wao uwanjani, Messi ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, yaani alizaliwa awe staa wa soka, misingi na mazoezi yamemfikisha pakubwa sana.

Ronaldo vilevile ana kipaji lakini hakifikii kile cha Messi. Ronaldo ana bidii kubwa kwenye mafunzo na mazoezi. Wanasema "hard work pays off", yaani bidii inalipa. Juhudi ya Ronaldo inamfanya kuwa mwanasoka bora sana.
Hata ukiutazama mwili wa Messi, hauna miraba ya mazoezi kama ilivyo kwa Ronaldo. Ni mastaa wakubwa wawili wa soka duniani, mmoja anatamba kwa sababu ya kipaji kikubwa alichojaliwa na Mungu, mwenzake anatembea kifua mbele kutokana na bidii yake ya mazoezi.

Ali Kiba ni Messi. Ana kipaji kikubwa, amejaliwa sauti nzuri ambayo kama asingechagua muziki, sijui angeifanyia nini. Kwa mantiki hiyo, kinachombeba ni kipaji zaidi kuliko jitihada za kujitangaza.
Ali Kiba kwa muda mrefu aliamini katika kuandika mashairi, kutengeneza sauti inayovutia kisha mashabiki watapenda tu kazi. Kipaji chake kikamfanya akubalike na kufika alipofika.

Diamond ni Ronaldo. Alipoanza muziki akaamua kujiongeza kwamba bidii yake inaweza kumfikisha pazuri. Alihangaika mno kujitangaza, akawa anafanya kazi sana, mazoezi ya kuhakikisha shoo zake zinakuwa bora.
Diamond akawa mtundu wa ‘kucheza' na media. Wanasema juhudi huvuta bahati, bidii yake ikamfanya awe msanii anayependwa sana, akaoneshwa njia nyingi akazifikia, akawa anacheza na vyombo vya habari, mwisho akawa Platnumz kweli!

MAKOSA:

Ali Kiba alipokuwa anang'ara sana, alisahau msingi wake kuwa ni Watanzania. Akawa anapanda sana ndege kwenda kufanya ziara nje, akaharibu soko lake la nyumbani. Hata kwenye vyombo vya habari akawa hapatikani. Waandishi wakimsaka kwa ajili ya mahojiano, anakuwa mgumu kutoa ushirikiano.

Si kweli kwamba Ali Kiba aliwahi kukaa kimya kwa miaka mitatu eti ndiyo Diamond akatamba. Januari mwaka juzi (2012), alitoa Single Boy akimshirikisha Lady Jaydee. Novemba 2012, alitoa My Everything baadaye akafanya project na mdogo wake, Abdu Kiba, ila hakuweza kukaa vizuri sokoni.

Mwana imemrudisha sokoni na Watanzania wameamua kumpa nafasi nyingine ya kutamba. Alipoangukia Ali Kiba ndipo Diamond alipojikwaa. Baada ya kufanya kolabo na akina Davido na kushiriki tuzo za BET na MTV, amesahau soko la nyumbani.

Mbwembwe zikawa nyingi, kila siku ‘anabodi' kwenda nje kupiga shoo mshenzi, nyingine anaishia kupigwa mawe, Watanzania waliomuweka pale juu hawamuoni shoo za nyumbani. Mapromota wa nyumbani waliomuwezesha kuwa alipo, walipomtafuta anawaringia.

Diamond aliyekubalika na kupendwa na watu ni mnyenyekevu, mtu wa watu, ila wa sasa ni ‘bwana misifa' kuliko Dully, utadhani watu wataacha kumzomea? Ni hoja dhaifu kusema wazomeaji walitengenezwa.

Huko nyuma, kuna vikundi vilishapanga kumzomea Diamond kwenye shoo zake lakini vilizidiwa nguvu na umati mkubwa uliokuwa unamshangilia. Rejea mwaka jana Maisha Club hali ilivyokuwa, jiulize kwa nini kwenye Fiesta wazomeaji waliwazidi washangiliaji?

Ali Kiba na Diamond wote ni wadogo zangu. Ali Kiba kwa ujio wake asafishe makosa. Aheshimu vyombo vya habari na mashabiki wake. Huu ni muda wa kutengeneza fedha. Diamond azinduke mapema, akiamini alizomewa kwa mipango, atazidi kufeli. Agutuke mapema na kusahihisha makosa.

unajitahidi kuelezea ila naona una chuki kwa dimond sema unazificha kwenye maneno kwa kumapka mafuta kwa mgongo wa chupa..

unatoa critiscism za kipuuzi kuwa Dimond ameacha shoo za nyumbani za watanzania waliompandisha?? hivi nikuulize unajua p square wapo wapi sasa??? kama hujui basi wanaishi zao atlanta wamehama kabisa nyumbani kwao Nigeria na bado wanafanya kazi nzuri sembuse huyu Dimond ambaye yupo sinza hapo,,,..

Dimond kwa level yake aliyofikia hapaswi kurudi nyuma kung'ang'ania shoo za uchwara kama Fiesta na zingine zenye mtonyo mdogo kwa kigezo cha eti watanzania walimpandisha, ushauri wako umejaa mawazo ya kimaskini...ni lini hapa bongo kuna promoter alimpa dimond hela anazotaka akakataa kupiga shoo?? kama anapiga shoo hadi kwenye birthday ya K Lyn we ulitaka aje akuimbie chumbani kwako mdogomdgo ndo ufurahie.........acha ujinga bwana
 
Back
Top Bottom