Miiku
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 3,835
- 2,630
Pichani ni Ally Hemed Kijana mwenye Siasa zenye weledi mkubwa sana. Kijana huyu ndiye anayemfanya Lowassa kuonekana kama alivyo.
Mikakati mingi ya Siasa anazofanya Lowassa zinaanzia kwenye kichwa cha Hemed. Mpaka mwaka 2015 alikuwa bado yupo CCM alihama na Baba yake Lowassa na ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kila sehemu ambayo Lowassa alikuwa anaenda kufanya mkutano.
Kwenye kampeni za 2015 ndiye aliyekuwa anaiongoza taasisi yake ya 4U Movement. Taasisi hii ilifanya kazi kubwa sana kuliko BAVICHA na UVCCM. Katika kura za Lowasaa milioni Sita nusu zilipatikana kwa kutumia kichwa hiki.
Ni mhitimu wa IFM na Aliwahi kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi IFM. Ndiye huyu anayeonekana kuwa karibu sana na Lissu kule Nairobi kwa sasa.
Kwa sasa ndiye Head Of Department ya Propaganda pale Chadema. Vijana wengi wa CHADEMA hawamjui vizuri Hemed Ally.
KWANINI NAMZUNGUMZIA ALLY HEMED?
Kuna Movement imeanza ndani ya Chadema ya vijana ambayo inapinga Falsafa za watu wanaohamia na kupewa majukumu ya moja kwa moja.
Vijana wengi wa Chadema wanamuangakia Hemed kama mtu ambaye anaweza kuwageuka siku za Usoni na kurudi CCM.
Kupitia Kitabu cha Yericko Nyerere cha Ujasusi wa kiuchumi na Kidola kijana Malisa Gj ametumia scenario ya mauaji ya Mwanausalama wa Rwanda aliyeasi (Patrick Gareya) anapinga kitendo cha mtu kutoka chama fulani na kuaminiwa kwa kupewa madaraka muda mfupi bila kujiridhisha kama kweli ni Kamanda mwenzao.
Hoja hii inawezekana imejengwa juu ya misingi ya kutokumuamini Mtu anayetoka CCM kama Nyalandu. Aidha andiko la Malisa Gj linatahadharisha viongozi wa Chadema kuwa makini na watu wanahamia kutoka CCM.
Aidha andiko hilo linajenga hoja kutokuthaminiwa vijana wa BAVICHA kama kina Malisa kutokupewa nafasi na Chama. Wapo vijana wengi sana Pale Bavicha wanafanya kazi kubwa. Yericko aliwahi kusema alikimbia kwa mguu toka Kigamboni hadi Dar Kukimbia asikamatwe hadi leo anaenda pale Kisutu kwa kesi ya kukitetea Chama.
Kuna Vita ya Chini chini inayoendelea ndani ya taasisi hii ya vijana ya Chadema. Mbowe anapaswa kulitazama hili kwa Jicho la kipekee na kuruhusu vijana waliokipigania chama kwa Muda mrefu kama kina Malisa kupewa nafasi zinazochukuliwa na makada wa CCM.
TATIZO HILI NI LA VYAMA VYOTE.
Tatizo hili halipo CHADEMA tu lipo kwa vyama vyote na hata kwenye chama chetu CCM lipo. Mfano pale UVCCM kuna watu wanazeekea pale na wanakipigania chama usiku na mchana ila kuna watu wanakuja toka Upinzania na kupita juu ya vichwa vyao na kupanda ngazi za Kiuongozi.
Jambo hili limekuwa likikatisha tamaa sana vijana waliopo kwenye Taasisi hizo.
Siwezi Kupingana na falsafa inayotumika kuwapatia vyeo ila utumike mfumo wa kuwashindanisha ili waliokutwa kama watashindwa basi roho zao zitulie.... na wakubali kuwa wameshindwa.
unaweza kunielewa unavyotaka........