PreGE2025 Ally Hapi: Vijana zungumzeni mazuri yaliyofanywa na Serikali

PreGE2025 Ally Hapi: Vijana zungumzeni mazuri yaliyofanywa na Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi, Ally Hapi, ameutaka Mtandao wa vijana wa Kesho Yetu, Uzalendo Wetu na Utaifa (TK Movement), kutokatishwa tamaa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya serikali, badala yake wasonge mbele kulisemea taifa kwenye mambo mazuri linayofanya.

1747031379612.png
Hapi amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya vijana zaidi ya 600 wa mtandao wa TK Movement kutoka mikoa yote hapa nchini kujifunza kuhusu masuala ya ushiriki wa uchaguzi Mkuu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema, vijana hao wasikubali kurudishwa nyuma katika kile ambacho wanakifanya ili kuhakikisha serikali inasikika kwa wananchi, kwa sababu hakuna jambo zuri linalofanywa bila ya kupata kikwazo kutoka kwa wengine.
 
Vijana 600 wasiojitambua watatumika kisiasa na kupewa mkate halafu baada ya uchaguzi wanatoswa.
 
Huyu angekuwa na akili timamu na uzalendo wa kweli angewaasa vijana waeleze yote yaliyofanywa na Serikali, mabaya na mazuri:


Wazungumze jinsi serikali ilivyoteka na kuua wakosoaji na wanaopinga rasilimali za nchi kuporwa na kugawiwa waarabu, waeleze pia miradi ambayo Serikali imefanikiwa kuitekeleza.

Halafu watu wapime mema vs mabaya.
 
Back
Top Bottom