Ally Bananga: Nipo tayari kurudi CCM kama mtanionesha waliomuua Alphonce Mawazo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,896
Diwani wa (CHADEMA), Kata ya Sombetini, Ally Bananga Binamu Bananga amesema yupo tayari kurudi (CCM) ikiwa viongozi wa chama hicho ambao wanataka kumnunua ikiwa watamuonyesha watu waliowatuma kumuua Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.

Banaga.jpg

Mbunge wa jimbo la Kibamba, John Mnyika (kushoto) Diwani wa Sombetini Ally Banaga (Katikati) akiwa na Mstahiki Meya wa Ubungo Mhe. Boniface Jacob (Kulia).

Ally Banaga amedai kuwa yeye yupo tayari kurudi CCM kama viongozi hao watatimiza jambo hilo na kusema hiyo ndiyo itakuwa gharama yake kurudi CCM na siyo fedha au mali kama ambavyo wengine wanadaiwa kupewa.

"Ma CCM wanaotaka kuninunua, leo nataja gharama za kurudi CCM. Nionyesheni mliowatuma kumuuwa Mawazo, nitajiunga nanyi siku hiyo hiyo" alindika Ally Banaga

Aidha Banaga ameonyesha masikitiko yake makubwa kwa watu ambao wanakisaliti chama hicho na kusema kuwa wamesahau kuna watu kama kina Mawazo ambao wamekufa wakikipigania chama hicho.

"Nilishika jeneza lako nikikuangalia mwamba umelala. Ndipo nilipoamini kuwa sio stori, mwanaume wa kweli uliyefia vitani ukikitetea chama ambacho kuna Mambwa Koko yanakisaliti, yanakichezea yanakinajisi bila kuhisi maumivu yako ulipotoka roho kukipigania. Nilikuita kwangu Dar es Salaam tupumzike baada ya uchaguzi mkuu ambao CCM walikupora kwa nguvu ushindi wako, kaka ukakataa kwa neno moja " Nikiondoka Makanda watakufa moyo, ngoja niwape tafu, Tukutane Dodoma.....dah! Tukakutania Mwanza kwenye jeneza" alisema Banaga

Mawazo%202.jpg


Novemba 14, 2015 aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Busanda kupitia CHADEMA na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita aliuawa kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana na kupelekea kifo chake.
 
Hii aina mpya ya rushwa, basi na Tundulissu aweke bei yake kwamba wakikamata waliomshambulia anarudi ccm.
 
Back
Top Bottom