Ally Bananga akamatwa na polisi kwa agizo la CCM

MWENGE OHOOO MWENGE.....MWENGE TUNAUKIMBIZA..........haina faida yoyote,uonevu,upendeleo kama kawa tz,si wauzime tu
 
Wananchi hatujawapuuza chadema, tafadhali tunaomba usitusemee. Tabia hizi hata wabunge wenu wanazo sana. Utasikia wakisema eti 'wananchi wa jimboni kwangu wamenituma'' wakati jimboni
ana miaka miwili hajakanyaga. Ongea na nafsi yako na si wananchi, kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe mbele za Mungu.

Hasa viti maalumu was chadema
 
Lizaboniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Wakati mwingine pima hoja kwanza.
  1. Bananga alikuwa safarini?
  2. Bananga alikutana na mbio za Mwenge?
  3. Bananga alikutana wapi na mbio za mwenge?

Bananga jambazi tu kama masour
 
attachment.php


Hii n Land Rover Puma inakimbia balaa kama wanaCCM walikuwa na Land Cruiser au Land Rover Tdi 300 hakika wasingeweza kuikamata wangebaki kusoma namba.
 
Teh teh teh naona umeamua kukiweka uchi Saccoss yenu mkuu!
1. Ufisadi muulize Dj na nyumba na NHC pia Padri na nyumba na NHC hela ya ruzuku analipa deni
2.Magaidi muulize Lwakatare Ben Saa8, Mallya
3.Manafiki muulize Tundu Lisu
4.Majuha ni kuulize wewe

Unatia Huruma Aisee,kama Mbowe fisadi na kuna magaidi cdm,tunaposema hii serikali ni dhaifu kwa nini hamtuelewi? Au unataka kutuaminisha kuwa mbowe ni zaidi ya hii serikali dhaifu ya chama chakavu hadi ishindwe kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria? SERIKALI INAYOSHINDWA KUMUWAJIBISHA MBOWE,BEN NA LWAKATARE ITAWEZA VITA YA UJANGILI NA MADAWA YA KULEVYA KWELI? TUNAPOSEMA HII SERIKALI NI DHAIFU MTUELEWE,TUIPUMZISHE KWANI IMECHAKAA IPO TAABANI
 
Khaa!! Mibongo mingine mijinga sana hasa ikiwa mianasiasa. Haijui taratibu zilivyo kazi kupiga kelele na kutoa mipovu tu. Askari wa trafik kazi yake ni kukutajia kosa lako la barabarani na kiasi cha faini unayotakiwa kulipa kama unahisi umeonewa basi unaenda kutafuta haki mahakamani. Sasa wewe yote hutaki unatoa povu tu kwanini usitulizwe na rungu la kichwa kwa kumzuia askari kufanya kazi yake ya halali aliyotumwa na jamhuri?? Mengine tunajitakia kwa ujinga wetu
 
Mungi, Usiwafundishe polisi kazi wewe!!! Unajua taratibu za mhalifu akikamatwa zikoje?/
Hedaru pana kituo kidogo cha polisi, hivyo ni lazima apelekwe Same kwanza!! Then Jumatatu au
jnne atapelekwa Korogwe mahakamani.

Tulieni hivyo hivyo, Mwenge ni TUNU ya Taifa una taratibu na kanuni zake, acha kuleta maneno ya khanga hapa.
 
Kila wanachokifanya CCM lazima kitawarudi soon... Tuendelee ku-document ujinga wao...
Wakuu,

Siku zote tunatambua kwamba tunaongozwa kwa sheria na kanuni katika maeneo yote yanayohusu maisha ya kila siku

Zipo sheria ambazo zimewekwa mfano sheria za barabarani (traffic regulation act) za nchi yetu, ambayo kimsingi ikithibitika zimevunjwa moja kwa moja anayeingia hatiani ni mtumiaji wa chombo yaani Dereva, na wala siyo abiria.

Kwa wasiojua leo kulikuwa na msafara wa mbio za mwenge Korogwe, kamanda Ally Bananga naye alikuwa Korogwe, wakati anatoka Korogwe na gari lake lililokuwa linaendeshwa na Dereva Daudi Kilo, walikutana na msafara wa Mwenge wakaupisha mpaka ukaisha, wakaendelea na safari yao kama kawaida baada ya kuruhusiwa na traffic.

Chakushangaza magari mawili ya ccm yakawa yanawakimbiza kwa nyuma, hawakujua sababu ya wao kuwakimbiza, na kwakuwa waliwaona wao walichokifanya ni kuongeza kasi, maana walijua kuwa kwakuwa gari lao lina mabendera ya chadema itakuwa imewaumiza roho ccm wanaosumbuliwa na homa kali ya UKAWA, wakajua wanataka kuwadhuru kwa tindikali au ugaidi wa aina yoyote ile.

Baada ya magari ya ccm kushindwa kuwakamata akina Ally Bananga, ccm wakaaamua kupiga simu polisi wawakamate Bananga na Dereva wake kwa kuingilia msafara wa Mwenge. Kilichotokea ni kwamba gari la Bananga lilizuiwa na polisi Hedaru, wakafunguliwa kesi ya kuingilia msafara wa Mwenge. Wakati wanaendelea kushangaa kilichotokea, ghafla maccm yakaingizana Hedaru,vwakawaamrisha polisi kuwaweka ndani Bananga na Dereva wake Daudi Kilo kwa kosa la barabarani (traffic offense), na wamenyimwa dhamana. Hivi ninavyoandika hapa, kinacholeta utata zaidi ni kwamba kuna mawasiliano yanafanyika ya kipolisi wakishirikiana na ccm kuwapeleka Bananga na Kilo Same badala ya kuwapeleka Korogwe ambapo wanapodai ndiyo kosa limefanyika.

Tukio la kukamatwa Bananga limethibitishwa na kamanda wa polisi kilimanjaro Robert Boaz

Tunajiuliza: hata kama kungelikuwa na kosa, Bananga anaingiaje wakati yeye alikuwa haendeshi?

Tunajiuliza: Kama kosa lilufanyika Korogwe kwanini wanapelekwa Same kulikoni?

CCM watambue tunawafahamu kuanzia kuchani mpaka unywele, hatutarudi nyuma hata muwatumie dola kwa hila ya namna gani, mapambano yataendelea mpaka kieleweke.

Tunajua hivi sasa maccm yanahaha na kuihofu chadema kuliko hata homa ya ebola, kwakuwa tu chadema imekubalika na watanzania nchi nzima.

Tutaendelea kuwajuza kila kitakachojiri......
 
Hata mwehu hawezi andika pumba kama hizi. Kiumbe gani wewe huna hata chembe ya aibu? Kama huwezi kujibu kwa hoja, kaa kimya. Mwehu!.

Teh teh teh naona umeamua kukiweka uchi Saccoss yenu mkuu!
1. Ufisadi muulize Dj na nyumba na NHC pia Padri na nyumba na NHC hela ya ruzuku analipa deni
2.Magaidi muulize Lwakatare Ben Saa8, Mallya
3.Manafiki muulize Tundu Lisu
4.Majuha ni kuulize wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom