Allergy Ya Manukato

camily

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
255
609
Habari wakuu..

Naombeni msaada naona nina allergy na manukato (perfumes & body spray), zinanipa mafua makali sana..

Na hii sio nikipulizia mimi tuu hapana, hata nikikaa na mtu alojipulizia basi ni tafrani, mafua hayaishi..

Sasa ofisini plus mitaani humu kwenye vikao vya bia ni ngumu sana kukaa sehemu watu hawanukii, msaada dawa gani ya kumaliza hii shida
 
Kuna uwezekano ikawa ni allergic rhinitis. Na kama ilivyo kwa allergy zote, unapogundua chanzo unapaswa kukiepuka, maana yake ukae mbali na visababishi, ambavyo kwa upande wako ni hizo perfumes, body spray na hata deodorants.

Kisha muda wote uwe na dawa za mafua, utumie unapohitaji.. Sasa dawa nyingi za mafua huwa zinalevya, hasa za 1st generation, hivyo kwa kuwa wewe unafanya kazi na unahitaji full concentration kazini, ni bora ukatumia dawa za 2nd generation. Mfano mzuri ni Loratadine na Cetrizine, although Cetrizine kuna baadhi ya watu wanasema zinaleta usingizi pia ila Loratadine hazina sedation.
 
Shukrani sana
 
Mkuu hapo kwenye kuepuka chanzo, sawa mimi sipakai au sijipulizii..Haya shughuli zetu hizi tunachangamana na watu tofauti kwenye mikusanyiko hapa na pale au kibaruani, kwenye usafiri, sokoni, ibadani

unachomokaje
 
Kuna uwezekano ikawa ni allergic rhinitis. Na kama ilivyo kwa allergy zote, unapogundua chanzo unapaswa kukiepuka, maana yake ukae mbali na visababishi, ambavyo kwa upande wako ni hizo perfumes, body spray na hata deodorants.

Kisha muda wote uwe na dawa za mafua, utumie unapohitaji.. Sasa dawa nyingi za mafua huwa zinalevya, hasa za 1st generation, hivyo kwa kuwa wewe unafanya kazi na unahitaji full concentration kazini, ni bora ukatumia dawa za 2nd generation. Mfano mzuri ni Loratadine na Cetrizine, although Cetrizine kuna baadhi ya watu wanasema zinaleta usingizi pia ila Loratadine hazina sedation.
Mkuu umenena vyema sana. Naona una uelewa juu ya issue za allergy natumaini unaweza kunishauri mimi pia. Kwa kifupi nami mwanzo nilikuwa nakohoa sana na kupata mafua makali mazizo mazito yale. Kwa eneo nililopo nilishindwa kupata msaada. Nipo Tunduma nilitembelea vituo vyote vya afya vya huku lakini hali ilizidi kuwa mbaya. Mwanzo niliambiwa nina gas nyingi tumboni kwahiyo inakuwa inaflow na inasababisha kukohoa na mafua nikapewa dawa lakini hazikusaidia kitu. Baadae nikashauriwa kukata kilimi lakini nayo haikusaidia. Nilienda hospitali ya rufaa mbeya nikafanyiwa vipimo vya kifua nikaambiwa niko salama nikaambiwa niende tu nyumbani sina shida yoyote. Hali ilizidi kuwa mbaya sana maana niliendelea kukohoa mwanzo mwisho na mafua makali na wakati huo nilikuwa sipati maumivu yoyote wala kudhoofika mwili. Kuna siku katika pita pita zangu jamii forum nkakutana na uzi unaeleza issue kama yangu katika kupitia pitia nikakutana na jamaa anadai alishapata solution. Nkamcheki akaniambia yeye kwake alipima akakutwa na allergy na alishauriwa awe anatumia rolatadine na nosal spray na baada ya kuanza kutumia hivyo huwa anajiskia vizuri nami nkajaribu hizo kiukweli zilinisaidia sana kwa kiasi kikubwa nakuwa safi nikitumia ila sasa ndo nikiacha tu ile hali inarejea tena. Concern yangu kubwa ni kwamba nina mwanangu ana umri kama mwaka na miezi nane nae naona ameanza kupata dalili kama zangu kikohozi na mafua hayaishi na dawa ameshatumia sana na kikohozi chetu kina tabia zinazoendana mara nyingi tunakohoa usiku tukiwa tumelala alfu kinakuwa pale unaposhituka usingizini na ukiwa umelala kwa kuangalia chali. Mimi nilishapima allergy nikaambiwa ninayo ila bado sijapima vipimo vya kujua ni allergy ya nini naomba kujua je kuna dawa permanent ya kutibu allergy na je allergy inaweza kuambukiza?
 
Sorry for late response.

Kwenye familia/ukoo wenu kuna tatizo la pumu (asthma)?

Nasema hivyo kwa sababu asthma nayo ina tabia hiyo, ni aina ya allergy, inazalisha IgE ambayo inapelekea mast cell zizalishe mediators i.e. histamines, prostaglandins na other cytokines, ndio maana ulipotumia loratadine ambayo ni antihistamine ilikusaidia.

Ok, kwa ninavyoelewa asthma (au tatizo lolote la allergy) huwa linazunguka ndani ya familia, kwa maana inarithishwa through generations, though urithishwaji wake ni complex, haiwezi kuelezewa by simple laws of inheritance like Mendelian's.
Tabia mojawapo ya asthma, mcharuko wake hutokea usiku kwa sababu kwanza, hewa ya usiku huwa imepoa (cold air), na cold air inakosa unyevu hivyo kupelekea irritation (bronchial spasm & hyperactivity) na kuzalisha makohozi kwa wingi (mucus production). Pili, kulala chali ni kichocheo pia cha kupelekea shambulio.

Sasa unaweza ukawa umerithi asthma isionyeshe dalili au ikaonyesha dalili kidogo endapo tu utapata chanzo cha kuichochea kwa mfano ukifanya mazoezi makali, moshi wa sigara n.k. ambayo hiyo inachukuliwa kama ni mild asthma.
Ila kuna nyengine kama moderate, severe na very severe ambazo hizo huhitaji kuambiwa kama ni pumu ili kujua.

Kipimo kama X-Ray kwenye asthma hakisaidii kitu, kwa sababu hawataweza kuona hiyo bronchial hyperactivity.
Kwa kuwa ushacheki na ukagundulika kuwa una allergy, unatakiwa kufanya lung function test ili kujua kama ni asthma au la. Hospitali huwa wanafanya spirometry na PEFR tests, those tests may be decisive.

Kwa sasa kama utapata/atapata dalili kama hizo tena, unaweza kutumia dawa ya salbutamol ya kunywa kwa mtoto au vidonge kwa wewe mtu mzima, mpaka utakajua tatizo ni nini ila usiendelee kukaa na mtoto nyumbani kwenye hali hiyo, mpeleke hospitali.

Najua kuna sehemu nimetumia maneno ya kitaalamu na unaweza usielewe ila nisamehe tu sikuwa na namna nyengine ya kufikisha ujumbe.
 
Asante sana mkuu hii salbutamol haina naiweza kuitumia kama ninavyotumia tolatadine yaani haina effects? Ili nitumie kwa kipindi hiki mpaka pale ntakapo fanya vipimo sababu hali inanirudia na rolatadine nakunywa sana naona kama zimeshazoea mwili hazifunction kama mwanzo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom