hili nalo neno !ngoja nianze mambo yangu yalee si wajua mi ndo event organizer humu ndani!
tuyaache hayo mamduchu!
ila umenigusa sna uliposema kuna kitu kimekufanya ukose raha mpka ukaona uende kwa baba padri!
Nimejaribu kujihoji mimi mwenyewe ni lini niliwahi kufikia hatua hii ya kujikana!?
UMENICHALLENGE i see!
Yeye kama padri anajua kuwa Mungu aliiweka ndoa kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora yeye mbona hakuoa ili atii maagizo ya Mungu
Acha woga mdadaa maisha ni hayahaya hakuna mengine. Au unataka mpaka ukutane nae Sellena Hotel, Beach au Mlimani City. Muda ni huu. We hata hakuna haraka ya kunijibu. kaa ufikirie then urudi. Kama vp una watu unawaogopa ni PM.
mh chezeya sister maria salome wa Asizi wewe!ahahahahhahaa kama sio weye vile!kweli leo tunapata upako!LOLsi wote wameitiwa wito wa ndoa...hata paulo alisema hayo..
baada ya kumaliza kunitibu kiroho, basi baba padri akanichapa swali, akaniuliza binti una umri gani??? nikamtajia magunia ya chumvi niliyokula, then akanitundika swali lingine, akaniuliza, je una mpango gani na swala la ndoa?? (nikajisemea moyoni loh huu mwaka wa kupewa ujumbe wa ndoa) nikamjibu baba padri wajua vijana wa sikuhizi hawapendi kuingia kwenye ndoa, kwani kwao ni jukumu kubwa na miye sitaki kuuvaa mkenge so bado nasoma mazingira.Basi baba padri akaanza kutiririka ,akanambia unajua kijana wa kiume aweza kutana na binti kwenye daladala na wakifika mwisho wa safari wanaishia gesti...limekuwa jambo la kawaida kwa vijana wa sasa kwani maisha wanayachukulia kiteknolojia zaidi.wasichana wanaangalia nani mwenye qualifications za kumwezesha kufikia malengo yake hivyo ni rahisi kwao kubadili wapenzi mara kwa mara, hivyo swala la mahusiano na ndoa wengi wanayachukulia kama ajira, na mwenye vigezo ndo anapewa nafasi.swala la upendo wa dhati halipewi kipaumbele kwenye mahusiano ya siku hizi na ndo sababu ndoa nyingi hazidumu.Ila hayo(huku akinitazama usoni) yasikufanye uepuke sakramenti ya ndoa, Mungu aliiweka kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora.Akahitimisha kwa sala nami nikaaga na kurudi kwangu.Huu ni ujumbe wa baba padri kwa vijana wote so muusome na muufanyie kazi.
hahahahah sina haraka miye ingawa sauti za kunihimiza zinazidi lol....
hahahahah sina haraka miye ingawa sauti za kunihimiza zinazidi lol....
si wote wameitiwa wito wa ndoa...hata paulo alisema hayo..
Mmmh, hiyo statement ina ujumbe uliojificha ndani yake. Ndiyo maana hujataka kuyaandika mengine. Bila shaka anataka uzae na yeye. Na kwa kuwa ushasema vijana wa siku hizi hawaeleweki, basi baba paroko anaweza kuwa ni chaguo zuri kwako au vipi? Si hana mke?hahahahahah kweli asee, baba padri amenigusa sana na maongezi yake..alinambia mengi sana ambayo hata sijayaandika hapa
Uwe mwangalifu na huyu baba padri wako. Bottom line ni kwamba wao pia ni binadamu wa kiume kama wanaume wengine. anaweza akageuza somo wakati wowote, na akaishia kumsingizia shetani