TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa TEC, Padre Raymond Saba afariki dunia

UTUKUFU KWA MUNGU JUU, Nakushukuru MUNGU kwa maisha ya Padri Raymond SABA kwa sababu yamenijenga kiimani, Nakumbuka alinifundisha kuwa Sala zangu zinisaidie kuingia katika mpango wa MUNGU na Sala sio njia ya kumuingiza MUNGU katika mpango wangu.
 
Mimi mwenyew namkumbuka sana katufundisha kigoma na ndoo alikuwa mkalimani kipindi barozi wa papa kaja kigoma kwenye sinodi ya kwanza jimbo la kigoma. Alikuwa anatafsili kila tini alikuwa nishida😥😥
 
akapate anachostahili…
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَمَاتُوا۟ وَهُمْ كُفَّارٌ أُو۟لَٰٓئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ ٱللَّهِ وَٱلْمَلَٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجْمَعِينَ

Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.
 
Umeanza upuuzi sasa
 
Mtesaji na mteswaji wote mwisho wao ni mmoja, tujifunze kutenda mema, pumzika kwa amani mtaalamu wa lugha saba za kanisa baba Raymond Saba, upokelewe mbinguni.
 
RIP Fr Saba..
Kanisa limepoteza mwl bora kabisa wa Biblia..
Wana Mivumoni tutakukumbuka daima.
Mwaka huu tumepoteza walimu 2 wazuri wa Biblia, Fr Mbiku wa pale UDSM na Fr Raymond. Kwangu mimi hawa wataendelea kudumu kama walimu bora kabisa wa neno la Mungu na ambao hutamani muda wa mahubiri uishe. Kweli dunia tunapita na siku zetu za kuwa hapa ni chache sana. Na aheri mwenye mwisho mwema kwa maana ataishi milele kwenye furaha na faraja.
Mwenyezi Mungu atufundishe kuzihesabu siku zetu.
 
Kweli kabisa Mkuu..

Fr Mbiku nae ni pigo kubwa ..
Nakumbuka alikuja Mwaka jana kutoa kipaimara pale Maria De Matias kijana wangu alikuwa anapata Kimapaira..

Kiukweli nilitarajia siku moja kumuona Fr Saba kuwa Askofu..nilimuona kwenye uelekeo huo. .

Mungu Ampe Pumziko la Milele.
 
akapate anachostahili…
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَمَاتُوا۟ وَهُمْ كُفَّارٌ أُو۟لَٰٓئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ ٱللَّهِ وَٱلْمَلَٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجْمَعِينَ

Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.
Imani yako isiwe sababu ya kuona wengine hawako sawa. Upo huru kusema chochote lakini heshimu hisia za watu hasa kwenye msiba. Mwenda zake alikuwa mtu mwema na aliyefundisha sana juu ya upendo kwa Mungu na jirani. Sidhani kama dini yako inafundisha tofauti na hivo viwili ukichukulia kiujumla mafundisho yake.
 
Kweli kabisa Mkuu..

Fr Mbiku nae ni pigo kubwa ..
Nakumbuka alikuja Mwaka jana kutoa kipaimara pale Maria De Matias kijana wangu alikuwa anapata Kimapaira..

Kiukweli nilitarajia siku moja kumuona Fr Saba kuwa Askofu..nilimuona kwenye uelekeo huo. .

Mungu Ampe Pumziko la Milele.
Kabisa
 
Askofu Joseph R. Mlola, ALCP/OSS, wa Jimbo Katoliki Kigoma anasikitika kuwajulisha kuwa ndugu yetu Padre Raymond Saba, ameitika sauti ya Mungu kutoka dunia hii leo kama saa mbili kasoro dakika ishirini hivi usiku.

Kama tulivyowajulisha, alikuwa akipatiwa Matibabu katika hospitali ya Rabininsia.

Tuzidi kuiombea roho yake pumziko la milele kwa Mungu.

Tuwaombee wazazi na jamaa zake wote. Tushikane mkono katika kipindi hiki kigumu kwa kuombeana.

Taarifa nyingine tutajulishwa baadaye.

Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani. Amina.

Fr Evarist Guzuye Chancellor
Kigoma, 3 Agosti 2021

NOTE: Huyu ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa TEC aliyenyang'anywa pasipoti baada ya kupata msukosuko kufuatia waraka wa Kwaresima mwaka 2018.

Poreni sana wafiwa.

Mkuu ni covid-19 iyo? Vijana wanapukutika sio muchezo
 
Back
Top Bottom