Aliyewafungia Wanafunzi 14 banda la nguruwe atetewa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,257
2,000
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nkasi mkoani Rukwa, Missana Kwangura amekiri kushindwa kumsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Matala, Revocatus Tinga, anayetuhumiwa kuwafungia wanafunzi watoro 14 kwenye chumba kimoja na nguruwe.

Alisema sababu ya kutomsimamisha kazi Ofisa Mtendaji huyo ni kukwepa kukiuka Kanuni za Utumishi wa Umma badala yake atamuhamisha kituo cha kazi.

Septemba mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda alimwagiza Kwangura kumsimamisha kazi Tinga mara moja na kuhakikisha nafasi yake inazibwa haraka kwa kumpeleka ofisa mtendaji mwingine.

Akizungumza na wanahabari mjini Sumbawanga alisema baada ya agizo hilo, aliunda timu ya wataalamu ambayo inaonesha kuwa ni kweli Tinga aliwafungia wanafunzi 14 ambao tisa kati yao ni wavulana na watano ni wasichana katika jengo wanalofugwa nguruwe.

"Ofisa Mtendaji huyo alifanya msako usiku na kuwakamata wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Matala wakiwa kwenye vibanda umiza wakiangalia video.

“Walikuwa wanafunzi 14 na aliwaadhibu kwa kuwafungia kwenye jengo la nyumba ambamo chumba kimoja walifungiwa wao na chumba kingine kilikuwa na nguruwe,” alisema

Alisema katika mazingira hayo hakutenda kosa kwa sababu aliwafungia wanafunzi kwenye chumba kimoja huku nguruwe wakiwa kwenye chumba kingine ndani ya jengo moja.

Akafafanua: “Kosa alilolifanya ni kuwafungia wanafunzi wa kike na wa kiume kwenye chumba kimoja usiku kucha. Sitamfukuza kazi ila nitamuhamishia kituo kingine cha kazi.”

Mtanda alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Swahilla kilichopo jirani na Kijiji cha Matala ambapo wananchi walimweleza kuwa adhabu hiyo ni ya kikatili.

"Adhabu aliyowapatia wanafunzi hao haikubaliki, nimeagiza asimamishwe kazi mara moja kisha akabidhiwe kwa maofisa wa polisi kwa uchunguzi na ikibainika kuwa amewatendea wanafunzi hao unyama huo, ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria,"alisisitiza.

Mtanda aliongeza: "Ni jambo lisilokubalika kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji ambaye ni mlinzi wa amani katika kijiji anafanya udhalimu huo, sisi kama serikali lazima tuchukue hatua stahiki."

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili Ofisa Mifugo Mwandamizi Mkoa wa Rukwa, Respisius Mayengo, alisema kama nguruwe hao wangekuwa na homa ya nguruwe, wanafunzi hao wangekuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa.

"Bahati nzuri mkoani kwetu hakuna ugonjwa wa homa ya nguruwe. Kitendo alichokifanya ofisa huyo hakikubaliki hata kama angewafungia kwenye banda la kuku au zizi la ngombe au wanyama wengine," alisema.
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,608
2,000
Hivi ni nani huwa anawapa Watanzania haki ya kuadhibu mtoto asiye wake ? Mini siku mtu akigusa mtoto wangu namchapa risasi, huu ujinga, ...
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
2,752
2,000
Mtendaji alifanya jambo zuri la kudhibiti nidhamu ya watoto ila ndio hivyo tena "mambo yame-back fire".

Vijijini kuna changamoto sana. Hapo alitegemea kupandishwa cheo ila anakwenda kushushwa.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,684
2,000
Yaani huyo apewe ukuu wa wilaya huyo ana uchungu anataka watoto wasome ebu fikiria usiku muda ambao sio wa kazi anajitolea kufanya msako bure wa wanafunzi watoro wakati hana cha kulipwa overtime wala Nini.Ana uchungu na watoto kuharibikka na kutaka wasome

Raisi Magufuli mpe ukuu wa hiyo wilaya huyo atainua kiwango cha elimu hapo
 

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
2,015
2,000
Mtendaji amefanya jukumu ambalo wazazi walipaswa kufanya..anapaswa kupongezwa na si kuadhibiwa
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,791
2,000
Habari inajichanganya, mara hatafukuzwa kazi, atahamishwa, Huku nukuu inasema kinyume, kafanya kitengo cha kinyama asimamishwe kazi.

WaTz tunatuliza akili zetu katika mambo gani?
 

Baba vinka

Member
Nov 28, 2020
8
45
Hapa najiuliza kitu ila jibu lake silipati, ikiwa hao wanafunzi angewaacha yaani asipitishe msako siku ile and let say kuna jambo baya limewapata usiku huo hapo kibandani walikokuwa hao wanafunzi asubuhi angelaumiwa nani?

Kama si yeye kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya kijiji ila kwa kuwa kadhibiti hii hali, Leo anaonekana mbaya. Mimi nampongeza sana kwa kazi aliyoifanya, Huo ni uwajibikaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom