Angalizo kwa wizara ya ardhi, mipango miji na wadau wake

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Naomba nitumie fursa hii kuwatahadharisha ninyi watu wa mipango miji na wizara husika ya makazi na uendelezwaji wa miji na makazi ya raia kwa ujumla.

Kumekuwa na kasi ya ununuzi wa viwanja, ujenzi wa makazi kiholela na umilikishwaji wa maeneo kibiashara unaofanywa na makampuni binafsi kuwauzia raia kwa kutumia ramani ambazo kwa baaadae italeta shida sana na changamoto za kimakazi.

Katika ununuzi wa viwanja kiholela, raia wanauziana viwanja bila hata kuzingatia mahitaji ya nafasi ambazo zinahitajika kuachwa kwaajiri ya miundo mbinu ya maji taka, umeme, njia kwaajiri ya barabara za dharula na mengineyo, matokeo yake ni kuwa na makazi ambayo hayaeleweki utadhani ni makazi ya wanyama na sio binadamu.

Hizi kampuni ambazo naziita uchwara, zinapima maeneo huko nje ya miji, kama kigamboni, bagamoyo, kiluvya na kwengineko na kuuza kwa bei ya juu kwa square metres kwa wananchi wa kipato cha chini au kawaida kabisa ambao wanaweza vimudu kwa shida sana hivi viwanja. Na mbaya zaidi hivi viwanja vimewekwa kwa mpangilio ambao mimi binafsi ninaona unakinzana na sifa za makazi bora ya binadamu.

Unakuta kwanza viwanja katika mchoro vimebananishwa kama makabati ya kuwekea kuku wa mayai na hakuna sehemu inaonyesha nafasi ya miundo mbinu muhimu kama maji taka, umeme, njia katika ya nyumba na nyumba, kitu ambacho kitakuja kushusha hadhi ya maeneo hayo muda makazi hayo yakishajazwa na wakazi. Naongea haya kwa kutazama tu changamoto tunazokutana nazo sisi wakazi wa maeneo ya makazi ambayo yameshajaa kama huku tabata segerea, tabata kimanga, kinyerezi na kwengineko ambapo kama serikali na mamlaka zake mlifanya uzembe wa hali ya juu na mlitakiwa kupewa adhabu kubwa sana kwa kutosimamia hili viwango vya kimataifa vya makazi.

Haya ni mapendekezo yangu baada ya kukaa na wadau ambao tulipata muda wa kulijadili hili swala kwa kina.

1. Serikali kupitia wizara ya ardhi na mipango miji, kwa haraka sana bila kuchelewa wasitishe shughuli zote za upimaji na uendelezaji wa miji unaoendelea kwa sasa kwasababu unafanyika kwa dosari nyingi sana especially gharama na pia mpangilio wa hizo plot ambazo nimeshasema kuwa haijazingatia viwango vya ubora na makazi kwa kutolipa kipa umbele swala la uwepo wa uhitaji wa nafasi za kuweka miundo mbinu ya maji taka, umeme, nafasi kati ya plot na plot ili kuruhusu nafasi ya hewa kwa muda ujao makazi yatapojaaa, drainage system kwa maana ya njia kubwa ya maji yanayopita hasa hasa nyakati za mvua kubwa, na vinginevyo.

2. Serikali kwa kupitia wataalamu ambao sio tu watafanya kazi kwa kufuata maoni yao binafsi na kujikuta ni wajuaji kupitilizia kutolea majibu vitu ambavyo kwa utashi wao wanahisi wapo sahihi na kumbe hakuna wajualo ila watatafiti mahitaji halisi ya wananchi ambao kwa sasa hawajaridhishwa sana na shughuli za muendelezo wa makazi mapya unaoendelea kwenye maeneo mapya ili waweze kuoutline vigezo sahihi kwasababu ramani za michoro ya plots zinalenga zaidi kuwanufaisha wamiliki wa hizi kampuni binafsi zinazopima na kuuza viwanja kwa bei ya juu na ya kibinafsi ambayo kwa raia wa kawaida mwenye kipato cha biashara ya vitumbua na maandazi hataweza mudu.

3. Serikali watambue hiki ninachokizungumza hapa kama kitapuuzwa kama yale maoni ya miaka ya nyuma ya kuwa na mji ambao haujapangiliwa kimkakati, matokeo yake ni hizi gharama za kipuuzi za bomoa bomoa ambazo huishia kuwatia hasara wananchi ambao mimi nasema pamoja na kuwa wanakuwa kweli wamefanya makosa ambayo ni kuwa kinyume na sheria na taratibu za makazi ila wanakuwa hawana hatia ya kupewa adhabu ya kubomolewa nyumba walizojenga kwa shida na viwanja hivi wanavyovipata kwa shida.

Hivyo basi, nawakumbusha serikali na mamlaka yake kuwa gharama na usumbufu mnaokwepa leo huwa haipotei vitazidi tu hizo siku za mbeleni, ingawa kawaida yenu ni kutumia mabavu na ubabe wa kimamlaka kuwanyanyasa hawa raia ambao hivi sasa mnawatazama tu wanavyopelekeshwa na hawa wachumia tumbo wanaojiita kampuni za kuuza viwanja vilivyopimwa. Hebu simamieni hili gharama ya kesho ya ubomoaji na kulipwa fidia kwa wananchi ndio mnaanza kuitengeneza taratibu hapa.


4. Katika mataifa yalitoendelea, hata tusiende mbali, hata hapo zimbabwe tu ambapo ni taifa lilikaliwa na wazungu na walipangilia vizuri sana upimaji wa maeneo ya makazi na kilimo, ni ngumu kukuta mtu anaishi kiwanja cha 20 by 20 meters eti kama sehemu ya makazi.

Huu ni udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za raia katika nchi yao wa hali ya juu. Yote hii ni kwasababu serikali kupitia watendaji wake wanaishi kwa mawazo na fikra za kumdharau sana mtanzania wa kawaida na kumuona ana hadi ya kutopata makazi mazuri yenye nafasi.

Wewe kweli unajenga eneo la mita za mraba 20 kwa 20, hiyo itakuwa ni sehemu ya makazi kweli?! Hapo si hata ukiachia ushuzi huko ndani majirani wanajua bwana fulani amepumua sasa hivi, au unampa wife ukuni huko ndani majirani si watasikia kila kitu, yote sababu ya kuwapo kaeneo kadogo tena vilivyo bananishwa.

Mapendekezo yaliyotokana na ushauri wa wadau wenzangu ni kwamba viwanja kwaajiri ya makazi ya nyumba ya kawaida yaani ndogo ya kipato cha chini kipimo cha chini kabisa kianzie robo heka na kuwe na bei fixed kutoka wizarani na serikalini maana kwa mujibu wa sheria na hata katiba ya nchi, ardhi si bidhaa ya mtu binafsi kama gari kusema kila mtu apange bei anayotaka katika manunuzi ya awali kwa ardhi ambayo haikuwahi tumika kabisa na haina title.

Ardhi inatakiwa bei ya matumizi yake ndio itofautiane na sio manunuzi ya hiyo ardhi yenyewe. Mfano mimi nikijenga nyumba bei ya kodi nitapanga mwenyewe na nitabargain na mpangaji, au nikipanda mazao, bei ya mazao ndio nitapanga mwenyewe. Ila sio mtu ananunua viwanja kwa lengo la kuwauzia wengine kwa bei za kufirika ambazo ukiambiwa utulezee umezikokotoaje utagindua ni tamaa za kidalali tu za kutaka kuwanyonya wengine kwa kitu ambacho ni mali ya uma hadi unaiuza kana kamba unauza nyumba, gari, au jengo ama mali yoyote iliyopatikana juu ya matumizi ya hiyo ardhi.

5. Usitishwaji wa haraka sana wa hizi shughuli za mauziano ya viwanja kati ya kampuni na badala yake serikali ishirikiane na hizi kampuni kwa kuzipa vipimo upya na wao kama serikali kutoa bei mpya elekezi na kutoruhusu watu kuvinunua viwanja hivi kwa malengo ya kuvihodhi kwa matumizi ya baadae au kuja kuwauzia wengine siku za usoni. Hii inatengeneza presha kwa wanachi wasio na kipato na wanajiona kuwa hawana haki wala hadhi ya umiliki wa ardhi katika taifa lao na hii imewapa mwanya raia wachache kununua ardhi na kuihodhi kitu ambacho ni kinyume na sheria.

Katazo lizingatie usitishwaji wa shughuli zinazoendelea za kupima na kuuza viwanja bila kuzingatia standard za makazi ya kisasa mara moja, bei sahihi ambayo inaendana na hali ya maisha na vipato vya watu pamoja madhumuni ya kuitaka ardhi kwa makazi.

Lakini muhimu zaidi katazo hili lilenge kurekebisha biashara hii ambayo mimi naweza ita haramu ya kugeuza ardhi ni bidhaa kama nyinginezo na kuachia kundi fulani la watu au watendaji wahodhi mamlaka na taratibu za kuitumia.

Hivyo basi bei elekezi itolewe ili kutoa mwanya kwa raia wa kipato cha kawaida waweze kupata makazi na wao kuondokana na mizigo ya kodi.

Waziri wangu mzee Lukuvi, najua hii kitu utaisoma, na hata usipoisoma basi ujumbe utakufikia bila shaka.

Naomba muandikie sheria mpya juu ya manunuzi na matumizi ya ardhi mpya ambayo haina hati ya umiliki.

Ardhi ni mali ya serikali kwann matumizi yake yapo kiholela kiasi kwamba vijana wadogo ambao wamekubali kupambana kujitafutia maisha wanapata wakati mgumu sana kuweza kuiaccess sababu tu kuna watu wachache wanaigeuza kuwa bidhaa huria na kuitumia kujipatia faida kama biashara ya karanga na hatimaye kuchelewesha maendeleo ya raia wengine sababu tu ya ubinafsi uliopitiliza?!

Tafadhali mkuu hii habari ya kuuuza kiwanja kwa sijui square meter inauzwa 10,000/, au 15,000/=, au 20,000/ au 25,000/ na kuendelea kwa mtu ambaye anashida ya kujipatia eneo la kujenga nyumba ya kuishi, sio ya kupangisha wala ya kufanyia biashara yoyote inasababisha raia wengi tena wa kipato cha chini kushindwa kumudu hiyo gharama na kuishia kujiona wapweke katika taifa lao.

Naomba tafadhali ndugu waziri hii kitu uifanyie kazi na kama utataka nikuandikie proposal ya utaratibu wa kulinda masilahi ya raia wote katika matumizi sahihi ya ardhi bila uonevu au ubaguzi wowote, then naomba uniruhusu nitaiandika na wadau waichangie mawazo na kuiboresha kisha uwe mswaada kamili.

Lakini pia, jambo la msingi ningependa kuligusia ni umuhimu wa shirika la nyumba la taifa NHC kujitafakari upya kuwa linamalengo gani kwa miaka ijayo, je wataendelea na uwekezaji wa ujenzi wa nyumba hizi za miradi kikoloni ambayo unashangaa unasema nyumba ya kiasi cha chini kabisa ni milioni 40 na wakati unaambiwa huku mtaani kuna mafundi wanawajengea watendaji wa serikalini na watu binafsi nyumba za kipato cha chini ambazo hazivuki milioni 30 na muda mwingine hata milioni 25.

Kwann sasa bei iwe kubwa hivyo kwa shirika ambalo limpewa dhamana ya kuwajengea raia makazi nafuu?!

Na kwann mnahangaika kujenga nyumba za kuuza badala ya kujenga majengo ya kupangisha ambayo wanavyumba Viwili tu mbona kuna mama pale Moshi amejenga kaghorofa ka kuishi kaya nane.

Juu nne na chini nne. Ambayo hiyo ghorofa ina sebule ambayo imeunga na dining hapo hapo sebuleni, halafu chumba kimoja cheye choo ndani na mashelf ya nguo huko huko ndani. Yaani safi kabisa be mkubwa anakusanya mpunga wake wa 120,000=/ kwa mwezi kwa kila kaya hapo.

Hivyo zidisha 120,000 mara 8 kwa maana ya mwezi. Halafu jibu lake zidisha mara sita uone hilo ni ghorofa moja.

Sasa hawa NHC wakezana kujenga majumba yao ambayo wanaishia kuleta masharti katika kuyauza na wateja wanaoweza kumudu ni wachache, wakati kama wangewekeza katika ujenzi wa makazi nafuu ya kupanga kwa kodi ili vijana wengi hususani huku mijini wangeweza pata nyumba kwa urahisi na madalali walale njaa kidogo maana hii tabia yao ya kutaka kodi ya mwezi mmoja ni ujinga usio na kipimo.
 
Kuna hadi chuo cha archi. Hawa jamaa naona ni viazi sana. Ama labda taratibu zao sijui zipoje ama sijui wanapima nini? Ama wanasiasa wetu(ccm) ndio wapumbavu labda.

Kwa sababu inawezekanaje mji usiwe na plan ya miaka hata 50 ijayo . Ili hata mtu akijenga gorofa kama lile la ubungo awe anajua.

Nyumba nyingi wanazobomoa hazina hata miaka 25.
Pumbavu.
 
Halmashauri za miji hazina uwezo wa kupima ardhi mijini, sasa watu waishi wapi wakati nyumba za kupanga hazitoshi na ni ghali. Jibu tagadhali
 
Wizara husika walushashindwa siku nyingi kufanya upimaji wa viwanja....ndomana wakawapa makampuni binafsi....
Siku zote serikali haiwezi kuendesha mambo

Ova
 
Halmashauri za miji hazina uwezo wa kupima ardhi mijini, sasa watu waishi wapi wakati nyumba za kupanga hazitoshi na ni ghali. Jibu tagadhali
Haujanipata vema.....

Sijasema serikali kupitia halimashauri wao ndio wafanye zoezi, la hasha. Nimemaanisha kwa namna zoezi linavyokwenda kwa sasa linahitaji kufanyiwa marekebisho. Inamaana serikali waweke utaratibu wa vipimo ambavyo vinakidhi ubora na mazingira ya kisasa.

Mfano, unakuta viwanja ishirini vimebananishwa kama makreti ya soda. Haieleweki ni wapi utapita mtaro wa maji taka ya kila nyumba, hakuna space kati ya mpaka na mpaka wa plot na mbaya zaidi bei ni kubwa sana na ni ya kibepari kwa square meter, na mbaya zaidi viwanja vinakadiliwa ukubwa kwa hadhi ya skwata.

Yaani viwanja ukisema ujenge nyumba ya ubora ya ramani ya kisasa inamaliza nafasi yote hapo haujaweka nafasi ya makaro ya choo, bado haujaweka karo kwaajiri ya maji ya kupeleka kwenye tanki kwaajiri ya maji, bado nafasi ya parking na banda la store ya nje. Sasa kwann wanaachia watu wanapima viwanja kwa kubana hivi?!

Ndio nikasuggest wawasitishe kwanza, then watoe vipimo vipya na sahihi, kwa wastani kiwanja chenye hadhi ya kukaa binadamu na kuishi kwa utu kinatakiwa kuwa ni robo heka, na hapo auziwe kwa bei ya jumla sio habari za square meters, na bei iwe chini na affordable kwa mtu ambaye atajaza taarifa kuwa ni ujenzi kwaajiri ya makazi yake ya kudumu sio nyumba ya kupangisha kwa biashara, kujengea lodge, shule, bar, pub, gereji bubu, au sijui nini hapana. Ni kwa ajili ya makazi ya households tu.
 
Wizara husika walushashindwa siku nyingi kufanya upimaji wa viwanja....ndomana wakawapa makampuni binafsi....
Siku zote serikali haiwezi kuendesha mambo

Ova
Na hilo lipo wazwazi kuwa hawawezi sasa baso hizi kampuni wanazoziachia kufanya hii kazi basi zizingatie ubora na standards maana isiwe tunapima viwanja vya kujengea mabanda ya kuku. Sasa wewe kiwanja cha mita 20 kwa 20 kina hadhi ya kukaa binadamu kweli kama sio kukiuka haki za binadamu.
 
Kuna hadi chuo cha archi. Hawa jamaa naona ni viazi sana. Ama labda taratibu zao sijui zipoje ama sijui wanapima nini? Ama wanasiasa wetu(ccm) ndio wapumbavu labda.

Kwa sababu inawezekanaje mji usiwe na plan ya miaka hata 50 ijayo . Ili hata mtu akijenga gorofa kama lile la ubungo awe anajua.

Nyumba nyingi wanazobomoa hazina hata miaka 25.
Pumbavu.
Eti bwana. Yaani ni mambo ya kijinga ujue haya
 
Na hilo lipo wazwazi kuwa hawawezi sasa baso hizi kampuni wanazoziachia kufanya hii kazi basi zizingatie ubora na standards maana isiwe tunapima viwanja vya kujengea mabanda ya kuku. Sasa wewe kiwanja cha mita 20 kwa 20 kina hadhi ya kukaa binadamu kweli kama sio kukiuka haki za binadamu.
Inategemea na makampuni yanayojihusisha na upimaji wa viwanja na kuuza!
Makampuni mengine wanapima kuanzia sqmt 1000 and above,wanaweka hadi mhindi mbinu Kama barabara etc
Ukiona wanapima viwanja vya mbanano ujue wamewalenga watu wa hali ya chini

Ova
 
Inategemea na makampuni yanayojihusisha na upimaji wa viwanja na kuuza!
Makampuni mengine wanapima kuanzia sqmt 1000 and above,wanaweka hadi mhindi mbinu Kama barabara etc
Ukiona wanapima viwanja vya mbanano ujue wamewalenga watu wa hali ya chini

Ova
Then hii ni mbaya sana
 
Wizara husika walushashindwa siku nyingi kufanya upimaji wa viwanja....ndomana wakawapa makampuni binafsi....
Siku zote serikali haiwezi kuendesha mambo

Ova


Hi kali, sasa wale maafisa ardhi kwenye hizo halmashauri wanafanya kazi gani, au ulikuwa ujanja wa watu fulani kuisingizia serikali kuwa imeshindwa kama yule aliyekuja na sera ya ubinafsishaji kumbe anataka kujimilikisha mgodi
 
Nimeshangaa kule Mikumi wamepima viwanja eneo ambalo wanyama pori wanapita kuelekea kunywa maji, siku moja tulikwenda kutazama viwanja tukashangaa wanyama wanakatiza kwenye eneo tunakoambiwa viwanja vimepimwa
 
Hi kali, sasa wale maafisa ardhi kwenye hizo halmashauri wanafanya kazi gani, au ulikuwa ujanja wa watu fulani kuisingizia serikali kuwa imeshindwa kama yule aliyekuja na sera ya ubinafsishaji kumbe anataka kujimilikisha mgodi
Hao Hao maafisa wa ardhi pamoja na maafisa wa ardhi ambao wa kujitegemea wanafanya kazi hizo.....
Tena bora private Kuliko wa ardhi wa ardhi pale pasua tu wakati mwingine

Ova
 
Na hilo lipo wazwazi kuwa hawawezi sasa baso hizi kampuni wanazoziachia kufanya hii kazi basi zizingatie ubora na standards maana isiwe tunapima viwanja vya kujengea mabanda ya kuku. Sasa wewe kiwanja cha mita 20 kwa 20 kina hadhi ya kukaa binadamu kweli kama sio kukiuka haki za binadamu.
Acha dharau mkuu Kiwanja cha mita 20×20 unakiita ni cha kujengea banda la kuku? Ni watanzania wangapi wenye huo uwezo wa kumiliki viwanja vya 60×60
 
Acha dharau mkuu Kiwanja cha mita 20×20 unakiita ni cha kujengea banda la kuku? Ni watanzania wangapi wenye huo uwezo wa kumiliki viwanja vya 60×60
Sasa kama umeelewa maudhui ya huu uzi utajua kuwa nimelenga kuwakomboa watanzania waweze kuaccess viwanja vya hadhi nzuri yaani vikubwa na sio viwanja vidogo kama hivyo
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Back
Top Bottom