kunze
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 398
- 469
NHC yajichanganya
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limejichanganya katika kutatua mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 25 ukihusisha nyumba iliyopo kwenye kiwanja namba 221, mtaa wa Maweni, Upanga jijini Dar es Salaam.
Mgogoro huo unaomhusisha mtumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ismail Ally Osman na NHC ambao shirika hilo limeshindwa kutekeleza agizo lake la kumhamisha (Osman) kutoka kwenye nyumba ya msaidizi (servant quarter) iliyopo kwenye kiwanja 221,Upanga ambayo yeye ni mpangaji.
Kwa mujibu wa barua yenye kumbukumbu namba NHC/DSM/775/VOL 11/58/GG ya tarehe 27/07/2016 iliyotolewa na shirika hilo kwenda kwa mpangaji Ismail Ally Osman, inamtaka kuhama kutoka kwenye nyumba hiyo kwenda kwenye nyumba nyingine aliyojengewa na NHC.
Osman amegoma kuhama kwa madai kwamba yeye ndiye mwenye haki ya kubaki katika nyumba hiyo. “ Nihame niende wapi,” alihoji Osma alipongea na gazeti hili wiki iliyopita.
Barua hiyo kwa Osman inasema “Tunapenda kukufahamisha kuwa ofisi ya Waziri Mkuu ilipokea malalamiko ya upangaji ya msaidizi (servant quarter) ambayo wewe ni mpangaji. Kama unavyofahamu malalamiko na mgogoro huu ni wa miaka mingi na hivyo ofisi ya waziri mkuu ilitutaka kuangalia upya chimbuko la mgogoro huu na tutafute namna bora ya kupata ufumbuzi wa kudumu.”
Barua hiyo iliongeza kuwa katika kutimiza hilo, shirika liliazimia kupitia upya historia ya suala hili na mgogoro uliopo pamoja na taratibu nzima zilizotumika kupangisha nyumba ya msaidizi (servant quarter) na kuona namna gani linaweza kushughulikia ili kutoa suluhisho la kudumu la mgogoro unaoendelea.
Shirika hilo limedai kuwa baada ya kupitia upya historia wamebaini kuwa Bi Imelda Abeli ambaye ndiye mama mzazi wa Osman alipewa hifadhi na Ndugu Mohamed Kissoky ili ajisitiri kwenye nyumba ya msaidizi kwa muda baada ya kuwa na matatizo ambayo yalimfanya kuondoka katika nyumba yao ya familia ambayo ipo karibu kabisa na nyumba wanayoishi kwa sasa.
“Bi Imelda alikaa katika nyumba hiyo ambayo mpangaji alikuwa Kissoky kwa muda kisha akanza kufuatilia kwa msajili wa majumba (sasa shirika la nyumba la taifa NHC) ili aweze kupangishwa kabisa katika servant quarter ambayo hapo awali alipewa kama hifadhi,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Hata hivyo barua hiyo ilieleza zaidi kuwa hatua hiyo ya Bi Imelda kutaka kupewa upangaji kwenye (servant quarter) ilileta mgogoro ambao wenyeji waliomkaribisha walitaka ahame kwenye servant quarter hiyo kwa kuwa ni sehemu ya nyumba kubwa na waliona itakuwa si haki kwa mgeni kupangishwa sehemu ya nyumba ya mwenyeji bila mwenyeji huyo kuridhia.
“Kitendo cha Bi. Imelda kuomba kupangishwa nyumba ya msadizi ambayo ilipaswa kutumiwa na mpangaji wa nyumba kubwa (main building) ambaye pia alikuwa akiliipia kodi, ndio chanzo cha mgogoro huo.
“Kumbukumbu zinaonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa mawasiliano mengi yakihusisha ofisi mbalimbali za serikali ikiwemo wizara ya Ardhi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais kuhusu mgogoro huu, ukweli unaonesha kuwa kosa lilifanyika kwa kumpangisha Bi. Imelda kuwa mpangaji halali kwenyeservant’s quarter kinyume na taratibu za upangishaji.”
Pia baada ya kupangisha, servant’s quarter iliyokuwepo haikukidhi mahitaji ya Bi Imelda hivyo kusababisha yeye kuongeza kwa kujenga mabanda mengine pamoja na kubadilisha mfumo wa maji taka.
Sambamba na mabanda yaliyoongezwa kwa ajili ya Bi. Imelda, barua hiyo imesema wapangaji wa nyumba kubwa nao pia walilazimika kuomba kujenga mabanda mengine kwenye kiwanja na bado mpangaji mmoja anahitaji kujenga banda ili kukidhi haja ya watumishi wake, hali ambayo itazidi kuharibu mandhari ya makazi husika.
Iliongeza kuwa katika kutafuta utatuzi wa mgogoro huu baada ya malalamiko kufika ofisi ya waziri mkuu, na yeye (Osman) kutoa maelezo kwa shirika, timu ya wataalamu wa shirika kwa kumshirikisha ilifanya ikaguzi wa kimazingira tarehe 20/5/2016.
“Katika ukaguzi huo ilionekana kuwa jengo haliwezi kuendelea kukidhi mahitaji yako, na pia ilionekana kuwa mazingira yanayozunguka nyumba unayopanga ni machafu na kumejengwa mabanda mengi kinyume na masharti ya upangaji na hayakupata kibali cha ujenzi na yanakiuka sheria za mipango miji.
“Kutokana na hali tuliyoikuta tulikupa muda wa wiki mbili ili uweze kuboresha mazingira pamoja na kuvunja mabanda yalijengwa bila ya vibali ambavyo pia yalionekana ni hatarishi kwa afya na kuweza kusababisha majanga ya moto.
“Tunasikitika kuwa tulifanya ukaguzi mwingine tarehe 16/06/2016 ambapo ilionekana kuwa hakuna chochote ulichofanya kuboresha mazingira yaliyopo na mabanda ambayo tulikwambia uyavunje hayakuvunjwa kinyume na matarajio na maelekezo tuliyokupatia.
Hata hivyo barua hiyo ilisema kuwa shirika liliwahi kumpa notisi mara nyingi na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za kuvunja mabanda yaliyojengwa kinyume na sheria ili kuepuka majanga ya moto na ya kimazingira kama milipuko ya magonjwa.
“Hivyo shirika kwa kuliona hilo na kwa lengo la kuepusha hatari lilikutafutia nyumba mbadala ambayo ni bora ili uhame hapo ulipo na hayo mabanda yaweze kuvunjwa, lakini cha kusikitisha sana ulikataa hiyo nyumba mbadala na badala yake ukaendelea
“hata hivyo, unapewa siku 30 uweze kujiandaa na ufike katika ofisi za shirika la Nyumba Makao makuu ili uweze kuonyeshwa na kupewa taratibu za upangaji na ukamilishe zoezi la kupangishwa rasmi,”.
Barua hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Milki,Hamad Abdallah na Mkuu wa Kitengo cha Sheria Martin Mdoe, imeonesha wazi jinsi ambavyo NHC imeshindwa kutetea wapangaji wake kadhalika na kulinda viwanja vyake dhidi ya wavamizi wanaolenga kusababisha migogoro isiyo na sababu za msingi.
Mgogoro huu ulianza mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambapo aliyekuwa mpangaji hapo awali,Mohamed Nassor Kissoky (MB), alimpa hifadhi Bi.Imelda baada ya kupatwa na masuala ya kifamilia ambapo alianza kutatua upangaji jambo lililozua mgogoro ambapo wenyeji walimtaka ahame.
Hata hivyo, Bi. Imelda hakuhama bali alianzisha ujenzi holela ambapo aliongeza mabanda mengi hali iliyowanyima wapangaji halali nafasi ya kutumia eneo hilo hivyo kuamua kushtaki NHC ambao hadi sasa hawajachukua hatua yoyote licha ya Waziri Mkuu kuelekeza kutatuliwa kwa mgogoro huo.