Aliyeumba upendo kumbe ndiye aliyeumba chuki na hasira pia iweje utukuzwe upendo pekee?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Habari za jumapili.

Tunapoutakafakari upendo; Unathibitika na kuonekana wa maana katika chuki, hasira na gadhabu!

Kama ilivyo mwanga unavyoonekana wa maana katika giza! Hivyo basi giza ni nalo ni muhimu liwepo ili nuru ipate kuthibitika! (Hivyo twapaswa kulitukuza na giza pia)

Maonyo na amri nyingi zinahubiri upendo pekee!
  • Upendo hauhesabu mabaya
  • Upendo hauhesabu shahada na Phd
  • Upendo haujivuni
  • Upendo unahamisha milima na mabonde
  • Upendo haupunji
  • Upendo haudhulumu n.k!
Hayo na mengine kedekede yanatajwa kusifu upendo pekee!

Mpende jirani yako kama nafsi yako!
Je, wanaojinyonga na kujiua nafsi zao watahesabika wamefanya upendo wakiua jirani zao kabla ya kujinyonga?

Upendo ni demokrasia inayobainika mbele ya chuki, hasira na gadhabu!

Upendo ni kama siasa ya vyama vingi, huwezi kuwa mshindi pasipo kutaja nguvu ya upinzani!

IKIWA KWELI UPENDO PEKEE NDIO WA MAANA
  • Kwanini wafuasi wa upendo tunadai madeni?
  • Kwanini wafuasi wa upendo (viongozi) tunaumiza wananchi?
  • Kwanini wafuasi wa upendo tunaishi maisha ya wafuasi wa chuki?
  • Kwanini wafuasi wa upendo madukani mwetu nasi tunapatanisha bei za bidhaa kwa dhuluma?
  • Kwanini wafuasi wa upendo tunaoneana wivu?
Hivyo kuna umuhimu wa kuona umuhimu wa kuihubiri chuki pia!

CHUKI INALIPA
  • Chuki inaleta adabu
  • Chuki inahakikisha deni linalipwa
  • Chuki inaleta ushindani wa maendeleo
  • Chuki inaleta nguvu ya kushindana
  • Chuki inaleta vita faida kwa viwanda vya silaha
  • Chuki inalinda mali
  • Chuki inapambaniwa
  • Chuki ni maisha
Aliyeumba upendo ndiye aliyeumba chuki, na vyote vinalipa!

Upendo ni mlango wa mbele, na chuki ni mlango wa nyuma!

Mlango wa mbele ukifutwa, wa nyuma nadhani si kosa kuutumia!!

Niwatakie Jumapili njema na maandalizi mema ya kampeni za uchaguzi serikali za mtaa.
 
Mungu hakuumba upendo Wala chuki.Yeye aliumba mtu .Huyo mtu ndie mwenye uamuzi wa kupenda au kuchukia
 
Upendo na chuki vinaishi pamoja na kila kimoja kinapotekelezwa kwa nafasi na muda muafaka ndipo manufaa huzaliwa, kinyume chake, hata upendo ukitekelezwa kinyume na wasaa na mahali huo upendo utakuwa ni bure.

Upendo ni kipimo cha chuki na hivyo hivyo chuki ni kipimo cha upendo.

They inter play.
 
Mungu aliumba mtu kwa sura na mfano wake!
andiko linatamka pia chanzo cha kuiangamiza sodoma ilikuwa gadhabu
 
Upendo ni amri kuu Yesu alituachia. Upendo huzaa amani. Ukimpenda mwenzako kama nafsi yako huwezi kumdhuru.

Upendo ukipelekwa pasipo na upendo huleta maumivu makubwa siku za mwanzo lakini matokeo yake ni furaha mbeleni.
 
Upendo na chuki vinaishi pamoja na kila kimoja kinapotekelezwa kwa nafasi na muda muafaka ndipo manufaa huzaliwa, kinyume chake, hata upendo ukitekelezwa kinyume na wasaa na mahali huo upendo utakuwa ni bure.

Upendo ni kipimo cha chuki na hivyo hivyo chuki ni kipimo cha upendo.

They inter play.
100% true
 
Upendo ni amri kuu Yesu alituachia. Upendo huzaa amani. Ukimpenda mwenzako kama nafsi yako huwezi kumdhuru.

Upendo ukipelekwa pasipo na upendo huleta maumivu makubwa siku za mwanzo lakini matokeo yake ni furaha mbeleni.
Kuna watu wanazidhulumu hadi nafsi zao, kuna watu wanajiua, wakikupenda ww kama wanavyojipenda wao utahesabu huo nao ni UPENDO
 
Upendo ni amri kuu Yesu alituachia. Upendo huzaa amani. Ukimpenda mwenzako kama nafsi yako huwezi kumdhuru.

Upendo ukipelekwa pasipo na upendo huleta maumivu makubwa siku za mwanzo lakini matokeo yake ni furaha mbeleni.
Upendo ni amri kuu Yesu alituachia. Upendo huzaa amani. Ukimpenda mwenzako kama nafsi yako huwezi kumdhuru.

Upendo ukipelekwa pasipo na upendo huleta maumivu makubwa siku za mwanzo lakini matokeo yake ni furaha mbeleni.

Wewe ni dini gani auntie??
 
Dunia ni ya ajabu sana......Muda mwingine huwa nawazaga Kwanin Duniani kuna chuki hasa kwa sisi Watu weusi kwanin hawatupendi mbona sisi tuna wapenda kwani tuliwakosea nini?.....Waarabu na Wazungu walituletea Dini na wakajinasibu kuwa wametufundisha Ustaharabu na upendo lakin mbona wao ndo wanaongoza kutuchukia bila sababu....Waarabu huku mtaani kwetu wanatamba na Dada zetu lakini mbona si tukiwamega Dada zao wanataka kutuua....Kuna mchizi wangu mpaka leo hana meno ya mbele Aling'olewa huko Wilolesi na kitako cha bunduki kisa alimla mtoto wa kiarabu mbona sisi hatuwang'oi meno wakitembea na dada zetu?? Hapa ni chuki kwa anae kuchukia ndo mpango
 
Halafu akichorwa shetani au pepo lazima awe mwafrika ngozi nyeusi
 
Back
Top Bottom