Aliyetuhumu polisi, mgonjwa wa akili

Aliyetuhumu polisi, mgonjwa wa akili

DISKETI

Member
Joined
May 20, 2013
Posts
17
Reaction score
4
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa ambayo imekuwa ikiripotiwa katika gazeti la Jamhuri la siku ya Jumanne tarehe 21 – 27 Mei, 2013 toleo No. 81 na la tarehe 28 Mei -Juni 3, 2013 toleo No. 83, yenye kichwa cha habari "MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW".
Taarifa hiyo siyo sahihi, kwa sababu mtu aliyehojiwa na gazeti hilo anayejulikana kwa jina la Mohamed Edward Malele ni mgonjwa wa akili ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mara kadhaa mtu huyo amekuwa na tabia ya kuwatuhumu viongozi na watu mbalimbali juu ya tuhuma zisizo na ukweli wowote kutokana na ugonjwa wake wa akili.
Jeshi la Polisi nchini linatoa rai kwa gazeti la Jamhuri kuwa makini na habari wananzoziandika ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha zenye lengo la kupotosha jamii. CHANZO: HABARILEO NA MAJIRA
 
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa ambayo imekuwa ikiripotiwa katika gazeti la Jamhuri la siku ya Jumanne tarehe 21 – 27 Mei, 2013 toleo No. 81 na la tarehe 28 Mei -Juni 3, 2013 toleo No. 83, yenye kichwa cha habari “MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW”.
Taarifa hiyo siyo sahihi, kwa sababu mtu aliyehojiwa na gazeti hilo anayejulikana kwa jina la Mohamed Edward Malele ni mgonjwa wa akili ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mara kadhaa mtu huyo amekuwa na tabia ya kuwatuhumu viongozi na watu mbalimbali juu ya tuhuma zisizo na ukweli wowote kutokana na ugonjwa wake wa akili.
Jeshi la Polisi nchini linatoa rai kwa gazeti la Jamhuri kuwa makini na habari wananzoziandika ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha zenye lengo la kupotosha jamii. CHANZO: HABARILEO NA MAJIRA
Huyu ni mwendawazimu mwenye akili, maana inaonyesha analijuwa sana jeshi la polisi... HIVI KWA NINI HAKUITUHUMU BoT?
 
Khaaa! Mara hii keshakuwa chizi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Polisi kwa hili mmetisha yaani mmecheza kama SG8 kwamba jamaa ni mgonjwa wa akili!..

Hivi hizi stori polisi wanazotengeneza huwa zinawafaidisha nini,yaani vitu vingine viko wazi wanataka na watu wengine

wafikiri kama wao?.

Tuliona kwa Dr. Ulimboka wakatengeneza stori,Lema wametengeneza stori na hii tena wameshampa kichaa mtu!..
 
Nani hajui kuwa polisi ndiyo wenye matatizo ya akili! Hamjawahi kuwaona wanavyogombania kwenda kwenye kuteketeza mashamba ya bhangi halafu waangalie mara moshi wa bhangi utakapoanza wanavyofurahi badala ya kukaa mbali na kukwepa moshi,wao wanakaa kule kule moshi unakoelekea,sasa kama moshi wa bhangi unakaa kichwani miaka saba mbona askari wengi si wazima!
 
Da ! Kali ya mwaka ! Mbona hajapelekwa milembe?
 
dah...wasimuue tu mwendawazimu wa watu!

Huyo ana akili zake na anakijua vizuri sana anachokiongelea,mbona hajayasema ya wizara ya fedha au hajataja ya JWTZ?? Wacheni kutubabaisha polisi baadhi ya maofisa wake wabaya sana
 
Haki ya Mungu, "Mbwa akimng'ata binadamu si habari, habari ni pale binadamu anapomng'ata mbwa"

Ikiwa angesema "Nimekuja hapa Dodoma kutoa ripoti kwa Mh. Pinda kwamba polisi wa Mwanza waliniambia niue bunduki nikakataa" ningemuona ni kichaa.
 
Sipendi niumize sana kichwa changu kwasababu Advera Senso analipwa kwa UPOTOSHAJI KAMA HUO.
 
Back
Top Bottom