Aliyetoa wazo la kusajili YouTube Channels pia aangalie namna ya kusajili akaunti za facebook,kuna video zinarushwa tena laivu,wapinzani wamejaa huko

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,509
21,578
Naona teknolojia inataka kuipiga kumbo sheria yetu iliyokuwa inadhibiti traditional media-magazeti-tv-redio. Hizi ilikuwa rahisi, unapiga pini tu wote kimya.

Lakini sasa teknolojia inataka kuleta mchezo wa paka na panya,tunakaba huku, teknolojia inaleta hiki,unakaba hiki, inaleta hiki, ila hatuchoki, tutakabana tu.

Aliyetunga kanuni za YouTube channels alisahau huko Facebook, tumefanikwa kuzuia TV na redio na magazeti yasirushe au kuandika mambo ya wapinzani, lakini Facebook hawa jamaa wanaenda laivu na wanaacha clips za kuangalia ambao hawakuona mapema.

Hizi live za Facebook na video ziangaliwe

Ikibidi kila mwenye akaunti Facebook aisajili na ailipie kama anavyolipia sanduku la posta

Viva Magufuli
#matege
 
Back
Top Bottom