Aliyetabiri mwisho wa Dunia, afariki!

Aliyetabiri mwisho wa Dunia, afariki!

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,852
Hakuna ajuaye mwisho wa dunia ni lini zaidi ya aloumba dunia hii.

Kiongozi mmoja wa dini ambaye alipata umaarufu nchini Kenya kwa kutabiri mwisho wa dunia mwaka 2006 amezikwa katika kijiji cha Bomet.

Kiongozi huyo wa madhehebu ya House of Yahweh Willy Kiplangat Sang alizikwa masaa machache baada ya kifo chake katika shamba la babaake kijijini Matarmat katika sherehe iliohudhuriwa na jamii yake, majirani na wafuasi wa kanisa hilo.

Ndugu za nabii huyo aliyezingirwa na utata wanasema aliugua ugonjwa wa kifua kikuu nyumbani mwake huko Mauche kaunti ya Nakuru ambapo alikuwa mkulima na muhubiri.
 
Kufa kila mtu atakufa mkuu. Kwa hiyo kifo akizuii mtu kutabiri mambo.
 
mwisho wa dunia ni siku yako ya kufa. dunia aina mwisho
 
afadhali alichotabiri kimemtokea sema alikosea kdg kutabir japo matokeo hayakua tofauti!!
 
Harold Camping ( July 19 1921- Dec 15 2013) alifanya hivyo pia, Huyu katika maisha yake alitabiri mara nne.
 
Last edited by a moderator:
Hahahajajahaj..., usionyeshe ujinga Mbele ya watu wengi hivi.., eti dunia haina mwisho..?!

Acha niseme hivi' kama haujui kitu na haujitambui kama haujui wewe ni mpumbavu!!
Basi huyo mkuu kadhihirisha hako kausemi.
Mungu amsaidie kutoka kwenye hayo mawazo,
 
Na akija "israeli je"?bado utakataa?*%#*

Israel unamaanisha mtoa Roho?? Sasa Kama Mungu mwenyewe ndo anajua Mwisho Lini Hata Yesu mwenyewe hajui... Huyo Israel ndo atanishawishi
 
Watafiti wa NASA wanasema katika sayari ya mars inaonekana kulikuwa na uhai kama miaka BILLIONI 4 iliyopita,mwisho wa dunia(uhai wa viumbe) tutasubiri sana tu!!!!

BULLDOG hebu mwaga data hapa inaonekana una ufahamu sana na hii kitu.
 
Hakuna ajuaye mwisho wa dunia ni lini zaidi ya aloumba dunia hii.

Kiongozi mmoja wa dini ambaye alipata umaarufu nchini Kenya kwa kutabiri mwisho wa dunia mwaka 2006 amezikwa katika kijiji cha Bomet.

Kiongozi huyo wa madhehebu ya House of Yahweh Willy Kiplangat Sang alizikwa masaa machache baada ya kifo chake katika shamba la babaake kijijini Matarmat katika sherehe iliohudhuriwa na jamii yake, majirani na wafuasi wa kanisa hilo.

Ndugu za nabii huyo aliyezingirwa na utata wanasema aliugua ugonjwa wa kifua kikuu nyumbani mwake huko Mauche kaunti ya Nakuru ambapo alikuwa mkulima na muhubiri.

ni kiongozi wa dini gani? alikuwa anatumia kitabu gani kufanya ibada?
 
Back
Top Bottom