Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,968
- 955
MBUNGE JAFARI CHEGE - KIJANA ULIYEMSAIDIA ADA MIAKA 10 ILIYOPITA LEO HII NI MBUNGE WA JIMBO LA RORYA
"Miaka 10 iliyopita, mwaka 2003 nikiwa kidato cha Tatu wakati nikiwa nahangaika kutafuta Ada kwaajili ya kunifanya niendelee na masomo yangu. Wakati ule Mhe. Jakaya Kikwete ulikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, nilikutana na wewe Chang'ombe" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Ndugu yangu mmoja anaitwa Julius amehudumu kama msaidizi wako Mhe. Jakaya Kikwete baada ya kusikiliza ukasema huyu kijana anasoma wapi, shida ni nini kwamba huyu bwana mdogo anahitaji Ada ya Shilingi 321,000 ili aweze kumaliza masomo yake na amebakiza siku tatu afanye mtihani wake. Nakumbuka ulitoa Shilingi 400,000 ukampatia Julius ukamuambia mpe huyu kijana aende kusoma na ukanipa usia" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Binafsi imebaki kwenye nafsi yangu, lakini nikushukuru na kukuambia kuwa Kijana uliyemsaidia zaidi ya miaka 10 iliyopita bila kujua ndoto na dhamira yake ya mbele ndiye aliyesimama hapa mbele na ni Mbunge wa Jimbo la Rorya" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Mungu aendelee kukuongezea, Akupe maisha Marefu na sisi kama Viongozi wabunge vijana tunayo ndoto ambayo tunakuiga kwa namna ulivyokuwa unaongoza nchi hii. Umekuwa mstaarabu, Mvumilivu hata pale unapopigwa mishale" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Ndugu zangu wa Rorya, nimeshiriki nanyi tangu ujenzi wa Kanisa, harambee ya kwanza ya vifaa vya Kanisa, ikaja Harambee ya pili kwaajili ya ujenzi wa Kanisa, kwa mara nyingine ya tatu nitachangia Shilingi Milioni Moja (1,000,000) - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya