Aliyeruhusu ujenzi wa vibanda juu ya Mtaro wa Maji Mbezi Luis anapaswa kuwajibishwa

Wapendwa uchafuzi wa mazingira unakua kwa kasi sana huko Mbezi Luis, biashara holela, kuziba njia za watembea kwa miguu, kuziba mitaro ya maji taka na kujenga mabanda yasiyokidhi viwango vya ujenzi kumeichafua sana Mbezi Luis...
Mbaya ni hilo la uchavuzi wa mazingira, hilo likikua linahitaji msimamizi mzuri na mazingira mazuri ya kufanya usafi.

Lakini umewahi kujiuliza ndugu mleta mada kwamba hao ndugu unaowatuhumu maisha yao yatakuwaje baada kuondolewa hapo?
 
Ingekuwa haina hata haja ya nguvu kama hali hii ingedhibitiwa mwanzoni walipoanza, kule Buguruni na Ubungo kuelekea Riverside mida ya jioni. Hili ni tatizo lina rudi nyuma miaka hata 10. Sema tu kipindi cha Magu akatamka hadharani wasibugudhiwe ndio ikawa fungulia mbwa, sasa tule matunda ya tulichopanda miaka mingi nyuma huko.

Ila ukweli ni kuwa maeneo kama Mbezi Luis na Mbagala yanakera sana, iwe kwa waenda kwa miguu kwa kukosa pa kupita au kwa wenye magari kwa misongamano ambayo ingeweza kupunguzwa kwa shughuli za kibiashara kuondolewa kando kando ya barabara.
 
Mbaya ni hilo la uchavuzi wa mazingira, hilo likikua linahitaji msimamizi mzuri na mazingira mazuri ya kufanya usafi.

Lakini umewahi kujiuliza ndugu mleta mada kwamba hao ndugu unaowatuhumu maisha yao yatakuwaje baada kuondolewa hapo?
Nimejiuliza mara nyingi tu na majibu nilipata kwamba hao ndugu wamelelewa vibaya, yaani sio siri wamelelewa ktk njia isiyopaswa.

Mwana umleavyo ndivyo akuavyo, viongozi wawajibike ktk hili
 
Kweli Miji imechafuka sana, kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuifanya miji ionekane vizuri
Ili miji ionekane vizuri, lazima viongozi wanaoshindwa kusimamia kazi wawajibishwe na nafasi zao zichukuliwe na wenye uwezo wa kusimamia
 
Back
Top Bottom