Aliyepanda treni ya Dar - Moshi aje atupe mawili matatu

Aliyepanda treni ya Dar - Moshi aje atupe mawili matatu

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
682
Reaction score
2,348
Salama wakuu,

Kama mjuavyo JF ni uwanja mpana sana kwa kuwa unahusisha watu wengi wa kila aina.

Wiki iliyopita treni ya Dar - Moshi ilianza kazi mara baada ya kutofanya kazi kwa miaka takribani 25. Ukipita mitandaoni utaona jinsi inavyosifiwa.

Kuna mwana JF yoyote ambaye amewahi kupanda treni hiyo? Kama yupo basi asisite kupita hapa na kutupa mawili matatu yanayopatikana katika treni hiyo. Nina mpango wa kwenda kula X-mas kwa mshikaji wangu Moshi, so ningependa kuipanda treni hiyo lakini mpaka nipate mawili matatu hapa.

Karibuni wakuu
 
Watu wa Moshi pombe zinaturudisha nyuma jamani, yaani tungekuwa mbele zaidi kama sio huu unywaji

Pombe licha ya kupoteza hela na muda, pia inakufanya kichwa chako kutokua sharp kuwaza mambo ya muhimu

Hapo ilikuwa saa ngapi? Kama usiku mnene hivi
 
Nilisemaga sipandi tena treni baada ya kupanda treni ya mwanza to tabora.... tulijazwa kama magunia hamna hata sehemu ya kusogeza mguu wala kujikuna... nilibanwa mkojo mpaka nikazikumbuka kanyelamumo. Nikaja kupanda ile deluxe toka kigoma mpaka Dodoma angalau nilienjoy japo mwendo wa kobe sababu reli ilikua imezeeka. Ila kwa hii ya Moshi nahamasika kupanda kwa sababu nyingi za ziada.


Sent using Subaru Forester
 
Back
Top Bottom