youngsharo
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 2,491
- 500
Ndugu wanajukwaa,
Mnamo mwezi wa 7 tar.1 kama sikosei nilileta uzi hapa kuwa mpenzi/mwanamke niliyekuwa ninaishi nae alisafisha kila kitu na kutoroka wiki moja kabla sijaleta uzi huo.
Kwa kumbukumbu ilikuwa kama tar 22 mwezi wa 6,Jana majira ya mchana nikiwa kwenye chumba changu cha kupanga alichoniacha nikiwa sina kitanda wala nguo ya kubadilisha nikasikia watu wanapiga hodi.
Baada ya kufungua nikamkuta ni yule aliyekuwa mpenzi wangu yupo na rafiki yake na wakati huo alikuwa analia akiomba nimsamehe kwa alichokifanya.
Nikajaribu kumuuliza vitu alivipeleka wapi amedai eti yeye aliviacha ndani hakuchukua chochote isipokuwa wakati anaondoka hakufunga mlango kwahiyo wezi wanaweza kuwa waliingia baada ya yeye kuondoka.
Lakini sikuishia hapo nikamuuliza nini kilimfanya atoroke akaniambia yeye mwenyewe haelewi kwanini alifanya vile na bado ananipenda anahisi ni pepo tu lilimuingia.
Kibaya zaidi nilipoenda kumpima tayari ana mimba ya wiki 3 ila hajaathirika.
Je, kama ndo wewe ungemfanyaje?