Aliyemtusi Rais Magufuli apata dhamana

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Screenshot from 2016-04-18 14:17:09.png

Mtuhumiwa Isaac Abakuki aliyekamatwa kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli kwenye ukurasa wake wa Facebook amepata dhamana.

Chanzo: Millard Ayo
 
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imempa dhamana Mtuhumiwa Isaac Abakuki anayetuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Hakimu mfawidhi Agustino Rwezire amesema Mahakama baada ya kupitia hoja mbili zilizotolewa na upande wa mashtaka na mshtakiwa, imeridhia kutoa dhamana kama haki ya msingi ya mshtakiwa kutokana na kosa alilotenda ambapo dhamana hiyo ni ya Wadhamini wawili waliotakiwa kuwa na jumla ya shilingi milioni tano.
 
habari njema hizi...
 
habari njema hizi...

Nakubaliana na wewe, hizi ni habari njema...ila ni funzo kubwa kwetukwamba mitandao hii ni hatari...mtu unaweza ukaandika mawazo yako na ukadhani kuwa uko sahihi kumbe miongoni mwa yale uliyoandika ni balaa, unashangaa watu wako mlangoni kwako.
 
ni kweli kabisa lakini sheria zisiwe za upande mmoja.
 
Nakubaliana na wewe, hizi ni habari njema...ila ni funzo kubwa kwetukwamba mitandao hii ni hatari...mtu unaweza ukaandika mawazo yako na ukadhani kuwa uko sahihi kumbe miongoni mwa yale uliyoandika ni balaa, unashangaa watu wako mlangoni kwako.
Huyu jamaa ametekeleza haki yake ya kikatiba ya kujieleza mawazo yake.

Hakuna haja ya kuogopa.

Inabidi apewe support yote kushinda kesi, ama sivyo kutakuwa na precedent ya kuminya uhuru wa kujieleza na hata JF tusifikiri itatukosa.

Hizi sheria za "Lese Majeste" zinatumika nchi za kifashisti.
 
Wakati mwingine tunakuwa na mihemko au tumekunywa bia wakati tunaposti mambo kwenye mitandao, mimi nawaomba JF waendelee na utaratibu wao wa kudelete haraka posti zinazoonekana ni utumbo
 
Huyu jamaa ametekeleza haki yake ya kijatiba ya kujieleza mawazo yake.

Hakuna haja ya kuogopa.

Inabidi apewe support yote kushinda jesi, ama sivyo jutakuwa na precedent ya kuminya uhuru wa kujieleza na hata JF tusifikiri itatukosa.

Hizi sheria za "Lese Majeste" zinatumika nchi za kifashisti.

Thanks, naomba uwe una-edit post zako kabla hujapost:

Kwa mfano:

kijatiba>>>>>>>>>>>>>>kikatiba
jesi>>>>>>>>>>>>>>kesi
jutakuwa>>>>>>>>>tutakuwa

Lakini pamoja na hayo mimi binafsi sikubaliani na mawazo yako.

Kusema Fulani ni 'bwege' huko siyo kutekeleza haki ya kikatiba. Pamoja na ukweli kuwa Ibara ya 18 ya katiba inatoa uhuru wa kutoa mawazo lakini ziko ibara nyingine ndani ya katiba hiyo hiyo zinazokataza kufanya matusi au kuwadhalilisha wengine.

Suala la katiba ni nyeti ambapo mtu unapaswa kusoma katiba yote na kuielewa. Uhuru wa kutoa mawazo unaruhusiwa lakini usibughudhi wengine.

Pili, sikubaliani na wewe kwamba hizi sheria za mitandao zinatumika kwenye nchi za kifashsti. Siyo kweli hata kidogo. Kila nchi ina sheria zake, Marekani ina sheria, China, Urusi, Uingereza na kadhalika na kadhalika. Huko Marekani mtu huwezi ukaanza kutoa siri za kijeshi kwenye mitandao, kwa mfano, kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa mawazo. Utawindwa kama yule Mmarekani (nadhani anaitwa Edward Snowden) aliyekimbilia Urusi.

Tatu, nakubaliana na wewe kwamba huyo Ndugu inabidi asaidiwe katika kesi yake ili aweze kuendelea na maisha yake yeye na familia yake.

kijGT
 
Hivi kwa nini serikali kupitia mahakama zake uwa inataka watu hata wa kipato cha chini kupewa dhamana kwa hela ndefu hivyo wakati yenyewe utoa mishahara kidogo sana kwa watumishi wake walio wengi bila kujali hali halisi ya maisha?
 
Thanks, naomba uwe una-edit post zako kabla hujapost:

Kwa mfano:

kijatiba>>>>>>>>>>>>>>kikatiba
jesi>>>>>>>>>>>>>>kesi
jutakuwa>>>>>>>>>tutakuwa

Lakini pamoja na hayo mimi binafsi sikubaliani na mawazo yako.

Kusema Fulani ni 'bwege' huko siyo kutekeleza haki ya kikatiba. Pamoja na ukweli kuwa Ibara ya 18 ya katiba inatoa uhuru wa kutoa mawazo lakini ziko ibara nyingine ndani ya katiba hiyo hiyo zinazokataza kufanya matusi au kuwadhalilisha wengine.

Suala la katiba ni nyeti ambapo mtu unapaswa kusoma katiba yote na kuielewa. Uhuru wa kutoa mawazo unaruhusiwa lakini usibughudhi wengine.

Pili, sikubaliani na wewe kwamba hizi sheria za mitandao zinatumika kwenye nchi za kifashsti. Siyo kweli hata kidogo. Kila nchi ina sheria zake, Marekani ina sheria, China, Urusi, Uingereza na kadhalika na kadhalika. Huko Marekani mtu huwezi ukaanza kutoa siri za kijeshi kwenye mitandao, kwa mfano, kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa mawazo. Utawindwa kama yule Mmarekani (nadhani anaitwa Edward Snowden) aliyekimbilia Urusi.

Tatu, nakubaliana na wewe kwamba huyo Ndugu inabidi asaidiwe katika kesi yake ili aweze kuendelea na maisha yake yeye na familia yake.

kijGT

Karibu post zote nazi edit, usually mara baada ya ku post.Sio tu kuhakiki spelling, bali pia ku organize mawazo vizuri zaidi ikibidi.There is no trade off between speed and accuracy.

Kusema fulani ni bwege kama ni bwege kweli ni kutekeleza haki yako ya kikatiba ya uhuru wa kujieleza. Kwa nini mtu ashindwe kusema ukweli kama nchi ina uhuru wa kujieleza wa kikatiba?

Zaidi ya hapo, suala la ubwege wa mtu ni argumentative na hivyo hakimu makini anatakiwa kulitupilia mbali.Bwege kwa mtu anayependa hela anaweza kuwa mtu anayetoa mshahara wake wote kusaidia masikini huku yeye akiishi kimasikini, wakati kwa mtawa anayetoa maisha yake kusaidia masikini, mtu huyo huyo si bwege.Kwa hiyo ubwege wenyewe unaweza kuwa a matter of opinion than fact, kitu ambacho sharia haiwezi kuamua.

Kuhusu sharia hizi kutumika nchi za kifashiti, soma, angalau introduction tu ya hii study iliyofanywa kwenye nchi 90 kuhusu hili suala.

"Insult Laws:An Insult To Press Freedom"

http://www.wpfc.org/site/docs/pdf/Insult Laws-Text.PDF

Suala si kila nchi ina sheria yake ama la. Suala ni kwamba sheria hii inatumika nchi za kifashisti.
 
Nilifikiri ni mimi peke yangu ambae naona 'bwege' sio tusi..
 
Nashukuru comrade, kwa link hiyo uliyoniletea. Nitasoma kwa makini ili niweze kuongeza knowledge yangu. In fact it is among my areas of interest/study. Thank you very much for that.

Kuhusu 'bwege' sitaweza kusema zaidi hapa ikizingatiwa kuwa suala lenyewe liko mahakamani. Naishia hapo, mahakama yenyewe itafanya intepretation.

Kwamba sheria hii inatumika nchi za kifashti ni argument ya huyo aliyefanya utafiti. Mtu anaweza kuja akafanya utafiti mwingine na aka-prove otherwise. Ndiyo uzuri wa utafiti...kuhusu press freedom or freedom of the media. naomba usome kitabu au article ya Edward Herman and Noam Chomsky, The Manufacturing Consent: the political economy of the mass media. sina uhakika sana na title lakini uki-google nadhani utapata. Hata link yenyewe sina, kwa sasa. Wasomi hawa wameeleza vizuri sana kuhusu the performance of the mass media na kueleza kwa kina the notion of media freedom.
 
Kama ulivyokuwa na maadili ya kutotaka kuzungumzia zaidi jambo la "bwege" kwa kuzingatia kwamba suala liko mahakamani, ingefurahisha zaidi kama ungesubiri kusema kama sheria hii inatumika nchi za kifashisti ama la mpaka usome hiyo study kwanza.Hata kama ni intro yake tu.

Chomsky namsoma sana, ila hicho ulichokitaja sijakisoma. Kuna nuance hapa ya kuangalia na kuelewa kabla ya kuingiza habari za "mass media" katika issue iliyo pana kuhusiana na freedom of expression kuliko mass media. Hapa tunazungumzia kitu kipana zaidi ya mass media, hapa tunaongelea mpaka "citizen journalists" na plain citizens rights to freedom of expression.

Huyu mshtakiwa si muandishi wa habari au mtangazaji as far as I know. Ni mwananchi wa kawaida tu aliyekuwa anaeleza maoni yake ya kisiasa Facebook.Kwa hiyo ingawa kuna masuala yameelezewa in the light of "mass media", the issue is much broader. Any critique that will be based on "mas media" may not be applicable to citizen journalists or plain citizens.

While Chomsky often lambasts mass media as a tool of the capitalist system/ ruling class, the same cannot be said when the issue of freedom of expression is looked at from the perspective of citizen journalists/ plain citizens.

While the study is focused on press freedom, the core idea is freedom of expression which applies at a much broader scope than just the press/ media.
 
Kama ulivyokuwa na maadili ya kutotaka kuzungumzia zaidi jambo la "bwege" kwa kuzingatia kwamba suala liko mahakamani, ingefurahisha zaidi kama ungesubiri kusema kama sheria hii inatumika nchi za kifashisti ama la mpaka usome hiyo study kwanza.hata kama ni intro yake tu.

Chomsky namsoma sana, ila hicho ulichokitaja sijakisoma. Kuna nuance hapa ya kuangalia na kuelewa kabla ya kuingiza habari za "mass media" katika issue iliyo pana kuhusiana na freedom of expression kuliko mass media. Hapa tunazungumzia kitu kipana zaidi ya mas media, hapa tunaongelea mpaka "citizen journalists" na plain citizens rights to freedom of expression.

Huyu mshtakiwa si muandishi wa habari au mtangazaji as far as I know. Ni mwananchi wa kawaida tu aliyekuwa anaeleza maoni yake ya kisiasa Facebook.Kwa hiyo ingawa kuna masuala yameelezewa in the light of "mass media", the issue is much broader. Any critique that will be based on "mas media" may not be applicable to citizen journalists or plain citizens.

While Chomsky often lambasts mass media as a tool of the capitalist system/ ruling class, the same cannot be said when the issue of freedom of expression is looked at from the perspective of citizen journalists/ plain citizens.

While the study is focused on press freedom, the core idea is freedom of expression which applies at a much broader scope than just the press/ media.

I like your arguments, comrade...nitasoma article uliyonitumia I promise...naona kweli umemsoma sana Professor Chomsky, anyway, tutawasiliana tena, but as a scholar I should admit your arguments are healthy, ingawa of course we differ in/on perception...
 
Back
Top Bottom