Of course wanaweza, yaani hilo nalo ni neno, lakini labda uniambie kwamba wale jamaa nao ni mashushushu (Vigogo) ambao wanayo influence serikalini hata leo, kwamba wanaweza kuamuru vijana wao wamlimboka daktari wetu. Kama ndivyo yataanikwa tu, humwagi damu ya binadamu ukawa salama, haiwezekani. Kama unadhani nabisha muulize Kaini aliyemuua nduguye Habili wakiwa peke yao porini. Ardhi ni shuhuda mzuri na anajua kuelezea mambo. Bado mimi napata shida sana kutenganisha maneno ya "LIWALO NA LIWE" na tukio zima la Ulimboka connected so closely in time hata katoto kachanga kanaweza kuelewa muunganiko huo. My take, yeyote atajwaye ni kwa jina la serikali. Waombe Mungu sana apone haraka na wala wasijaribu kumfuatilia kummalizia, kwa sababu watatangula wao kumalizwa, maana sasa janja ya nyani madaktari wameishaitambua. Walidhani wanatibu kumbe walichofikiri ni maji ya kuzimia moto ni petrol. Shame on them!
Ulimboka usihofu, utapona tu mwanangu. Wanaokujua na hata wasiokujua, kwa sasa wameunganika kulikabidhi jina lako kwa Mungu aliyekunusuru, ili akuimarishe urudi barabarani tena, kiwembe kikali zaidi kuliko kwanza, sababu umepitishwa kwenye tanuri la moto mkali. Mzee Nelson Mandela alishasema "Mtu maarufu maisha yake ni machungu sana" Huo ndio msalaba Mungu kakukabidhi ubebe, mrudishie Mungu wako Utukufu, maana leo hii unasikiliza watu wanavyoguswa, ambapo adui zako hawakutaka ushuhudie haya masikitiko ya watu hawa. Doctors, be serious, unite!