Aliyekuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Makini, Coaster Jimmy Kibonde ameomba Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kumpatia Gari ambalo alipewa kama mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais Tanzania kwakuwa amelitendea haki kwa Kufanya kampeni karibu mikoa yote nchini Kunadi sera zake pamoja na kutangaza amani.