Aliyekuwa katibu mkuu UVCCM Pemba ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,004
Friday, May 20, 2016
Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe.

Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.
Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.
Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.
“Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.
Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein, akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa haki.
 
Usipoziba ukuta utajenga ukuta! Demokrasia isiyozingatia sheria za nchi ni hatari sana. Tukichelea Zanzibar itakuwa kama Siria hivi karibuni. Afadhali ya Besige wa Uganda kuliko ya Maalim Seif wa Zanzibar. Ashughulikiwe once and for all na chama chake cha CUF kifutwe.
 
DUH WE NI HATARI KAMA UKOMA, AKISHUGHULIKIWA HUYU JAMAA UNAUHAKIKA HATATOKEA MWINGINE NA CHAMA KINGINE HATARI KAMA CUF? SHUGHULIKIA DOMOCRATIA? NDO SULUHISHO.
 
walichokifanya ccm hawajaridhika nacho sasa wanaenda mbali zaidi hadi maalim seif akamatwe ukizoea kula nyama za watu huwezi kuacha.
 
Friday, May 20, 2016
Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe.

Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.
Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.
Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.
“Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.
Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein, akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa haki.

Gazeti la Raia Tanzania, itueleze ukweli wa " tamko au kauli" hii wameitoa au kuipata wapi? kwa mkewe? Tunavyojua Nd. Sukwa sasa ni mlemavu wa macho, hatoki na hatembei.Mahojiano hayo yalifanywa kwa njia ya simu au ya kulazimisha?
 
Usipoziba ukuta utajenga ukuta! Demokrasia isiyozingatia sheria za nchi ni hatari sana. Tukichelea Zanzibar itakuwa kama Siria hivi karibuni. Afadhali ya Besige wa Uganda kuliko ya Maalim Seif wa Zanzibar. Ashughulikiwe once and for all na chama chake cha CUF kifutwe.

Jifariji na misemo uchwara na usiyoijua! Pole sana na wangekushugulikia wewe kwanza kabla ya cuf
 
Usipoziba ukuta utajenga ukuta! Demokrasia isiyozingatia sheria za nchi ni hatari sana. Tukichelea Zanzibar itakuwa kama Siria hivi karibuni. Afadhali ya Besige wa Uganda kuliko ya Maalim Seif wa Zanzibar. Ashughulikiwe once and for all na chama chake cha CUF kifutwe.
Hongera kwa akili za kushikiwa!
 
Back
Top Bottom