Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Rufiji (Rubada), Aloyce Masanja, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la wizi wa Shilingi Milioni 86.
Pia, mahakama hiyo imemuamuru mshtakiwa Masanja kulipa fidia ya Sh. milioni 86 kwa kampuni mbili za kilimo zilizoingiza fedha kwa mshitakiwa huyo.
Hukumu hiyo imesomwa leo Septemba 16, 2020 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.