"Aliyekosea kupenda basi kayakosea maisha"

Mogadishuu

Member
Joined
Jun 22, 2019
Posts
33
Reaction score
65
Huu ni usemi nilisikia kwa Sheikh mmoja hivi, nahisi amenigusa mimi kabisa. Nimekosea kupenda hivyo nimeyakosea Maisha yangu kabisa. Nipo kwenye ndoa lakini niliyemuoa nilikuja gundua simpendi japo yeye ananipenda sana na ninayempenda siwezi kumuoa ilimradi tabu tupu.

Natamani siku zirudi nyuma nirekebishe makosa lakini haiwezekani sijui hata nifanye nini. Natamani niishi peke yangu tu lakini najiuliza mimi ni mwanaume nikishikwa na hamu itakuwaje? Nizini? Siwezi. Au nibaki kwenye ndoa lakini tuishi mbali mbali na huyo mke wangu, maana simtendei haki kuwa nae karibu, namkosea mpaka nafsi inanisuta.

Naona bora nibaki peke yangu tu, niwahudumie familia nikiwa mbali nao, nimpe na uhuru huyo mke wangu kama akipata mtu nimpe talaka ili aolewe na mwingine.

Na huyo ninayempenda hatuwezi kuwa wote tena. Shida
 
Kazi kweli, fanya kile unaona kitakupatia furaha katika maisha yaliyobakia hapa duniani
 
Huu ni usemi nilisikia kwa Sheikh mmoja hivi, nahisi amenigusa mimi kabisa. Nimekosea kupenda hivyo nimeyakosea Maisha yangu kabisa. Nipo kwenye ndoa lakini niliyemuoa nilikuja gundua simpendi japo yeye ananipenda sana na ninayempenda siwezi kumuoa ilimradi tabu tupu.
Natamani siku zirudi nyuma nirekebishe makosa lakini haiwezekani sijui hata nifanye nini. Natamani niishi peke yangu tu lakini najiuliza mimi ni mwanaume nikishikwa na hamu itakuwaje? Nidhini? Siwezi. Au nibaki kwenye ndoa lakini tuishi mbali mbali na huyo mke wangu, maana simtendei haki kuwa nae karibu, namkosea mpaka nafsi inanisuta. Naona bora nibaki peke yangu tu, niwahudumie familia nikiwa mbali nao, nimpe na uhuru huyo mke wangu kama akipata mtu nimpe talaka ili aolewe na mwingine.
Na huyo ninayempenda hatuwezi kuwa wote tena. Shida
Pole sana mkuu, mitihani yetu inaweza kufanana, hiyo ni njia panda mbaya sana katika maisha
 
Hamuwa vema kk, lakini kaa ukitambuwa aupati unacho kitaka lakini unapata unacho staili

Ule ndo wako
 
Siku za nyuma kidogo nilienda kuchumbia sehemu....na kilichonivuta pale ni maadili aliyokuwa nayo yule binti....si unajua waislamu wanaovaa stara.....ila ilinibidi ni stop mchakato mzima baada kulisoma game niligundua binti hanipendi ila ameamua kukubali kuolewa kuzikimbia dhiki za nyumbani kwao....baadae ingekuwa ndoa ndoano hii........
 
Ulijuaje kama ndo nia yake? Huenda alikupenda kweli.
 
Siku za nyuma kidogo nilienda kuchumbia sehemu....na kilichonivuta pale ni maadili aliyokuwa nayo yule binti....si unajua waislamu wanaovaa stara.....ila ilinibidi ni stop mchakato mzima baada kulisoma game niligundua binti hanipendi ila ameamua kukubali kuolewa kuzikimbia dhiki za nyumbani kwao....baadae ingekuwa ndoa ndoano hii........

bora ulijua mapema
 
Mwanamke hapendi mkuu kama unasubiria kuoa mwanamke anayekupenda utachelewa Sana maana mwanamke anatii na mwanaume anapenda ndo maana mtu anatoka mwanza huko anaenda kuoa tanga kwa mwanamke aliyeonyeshwa siku moja tu ndugu zake wa karibu.
 
Huu ni usemi nilisikia kwa Sheikh mmoja hivi, nahisi amenigusa mimi kabisa. Nimekosea kupenda hivyo nimeyakosea Maisha yangu kabisa. Nipo kwenye ndoa lakini niliyemuoa nilikuja gundua simpendi japo yeye ananipenda sana na ninayempenda siwezi kumuoa ilimradi tabu tupu.

Natamani siku zirudi nyuma nirekebishe makosa lakini haiwezekani sijui hata nifanye nini. Natamani niishi peke yangu tu lakini najiuliza mimi ni mwanaume nikishikwa na hamu itakuwaje? Nizini? Siwezi. Au nibaki kwenye ndoa lakini tuishi mbali mbali na huyo mke wangu, maana simtendei haki kuwa nae karibu, namkosea mpaka nafsi inanisuta.

Naona bora nibaki peke yangu tu, niwahudumie familia nikiwa mbali nao, nimpe na uhuru huyo mke wangu kama akipata mtu nimpe talaka ili aolewe na mwingine.

Na huyo ninayempenda hatuwezi kuwa wote tena. Shida
Kuna mahali niliwahi kusikia wajuzi wa mambo wakisema, "wengi walioko kwenye ndoa hawapendani, na wengi ambao wanapendana hawako kwenye ndoa".

Hadithi yako inasadifu falsafa hiyo hapo juu.
 
Huu ni usemi nilisikia kwa Sheikh mmoja hivi, nahisi amenigusa mimi kabisa. Nimekosea kupenda hivyo nimeyakosea Maisha yangu kabisa. Nipo kwenye ndoa lakini niliyemuoa nilikuja gundua simpendi japo yeye ananipenda sana na ninayempenda siwezi kumuoa ilimradi tabu tupu.

Natamani siku zirudi nyuma nirekebishe makosa lakini haiwezekani sijui hata nifanye nini. Natamani niishi peke yangu tu lakini najiuliza mimi ni mwanaume nikishikwa na hamu itakuwaje? Nizini? Siwezi. Au nibaki kwenye ndoa lakini tuishi mbali mbali na huyo mke wangu, maana simtendei haki kuwa nae karibu, namkosea mpaka nafsi inanisuta.

Naona bora nibaki peke yangu tu, niwahudumie familia nikiwa mbali nao, nimpe na uhuru huyo mke wangu kama akipata mtu nimpe talaka ili aolewe na mwingine.

Na huyo ninayempenda hatuwezi kuwa wote tena. Shida
Pole sana ndugu yangu.
Naombeni kila mtu avumilie na ndoa kama umeshaingizana kwenye hiyo kipegele ya maisha ya ndoa. Naomba muelewe hakuna aliye kwenye ndoa anafurahia 100% ya ndoa yake labda tu pale ndoa ikiwa changa huwa mtapendana sana lakini kadiri mnavozidi kuishi kwenye ndoa lazima mapenzi yapungue na ukitaka yasipungue muishi mbali mbali ili mkikutana mtakuwa na hamu na mwenzako. Mwanamke anakuaga mzuri sana mnapoanza maisha ya ndoa lakini mkianza kuishi kidogo kidogo anapoteza mapenzi kwa mume wake tena muwe na watoto sijui huwa ni kitu gani mkishapata watoto mke huwa hana hamu tena na mumewe mpaka hata kupewa haki ya ndoa anaona ni usumbufu na wengine watakuambia mimi (yeye) siyo wa kuliwa kila siku. Sitaki niandike mambo mengi lakini ujue hakuna mwanamke aliezaliwa na mnadamu akawa anakupenda kama utakavo wewe kitu cha msingi mheshimiane na mvumilianeni na kama unataka kujua hakuna anayekupenda 100% mfukuze au umpangishee sehemu nzuri na umdanganye alafu wewe oa huyo ulienae mpenda halafu baada ya mwaka utapata matokeo.

Ushauri wangu;
1)Ili ufurahishe nafsi yako wewe jitahidi kupata huduma zako za kimapenzi kwa huyo unaempenda sana kwa sasa ila umheshimu huyo wa nyumbani. Fanya mambo yako lakini yeye asijue then jion/ usiku unarudi kwa familia yako; nasema hivi kwasababu huyo huyo ukija kukaa nae pia zitakuja changamoto zingine ambzao hujawahi kuwaza kuwa yeye atakufanyia.
2)Ishi na huyo mwanamke anayekupenda kuliko unayempenda. ndugu yangu utateseka sana kama utamuoa mwanamke unayempenda wewe kuliko anaekupenda. Iko siku utalia kama mbwa "I am telling you" ukawaulize wanaume waliopitia ndoa kwa muda mrefu- Sasa hapo kuna namna ufanye ili usimkwaze pia; safari ya maisha ni ndefu please epuka kukwaza mwenza wako maana ndo mtasaidiana kwenye haya maisha.

Hitimisho;
Kumpata mke anayekupenda ni ngumu sana lakini kumpata mke unayempenda ni rahisi sana. Hapo uchaguzi ni wako maana maisha ni ya kwako IKO SIKU UTAENDA KUMTAFUTA HUYO ANAEKUPENDA na kumwacha unayempenda.
 
Back
Top Bottom