Aliyefanikiwa kuondoa kitambi naomba anishauri

GAZETI,

Mazoezi bila kuzingatia intake yako ya chakula ni sawa na kazi bure kwasababu calories unazochoma ndo hizo hizo unaingiza, pengine hata zaidi.

Kama unataka mabadiliko kweli anza na kiasi, pia aina ya vyakula unavyokula. Punguza vitu vya sukari, mafuta na carbs alafu zingatia mboga mboga, matunda na protein.

Ukifanya hivyo bila hata mazoezi utaanza kuona mabadiliko taratibu.
 
Aisee asikwambie mtu, CHAKULA CHAKULA CHAKULA ndio suluhisho, ukiweka nidhamu ya chakula aaaah mbona unapungua fasta.

Leo asubuhi nimeamka na yai la kuchemsha na andazi moja! hapa nina mtindi kwenye glass ofisini, naupiga taratiiibu mpaka saa 6 mchana!
 
Punguza vyakula vya wanga kwa kiasi kikubwa. Sasa hivi narudi kuwa flat baada ya kupunguza kula wanga
 
Nunua hicho kitabu soma kisha fuata maelekezo, mimi nilikuwa ninafuatilia lishe nukashusha kama kilo 7 ndani ya mwezi, daaah ila konyagi na kitimoto sasa
 
Nunua hicho kitabu soma kisha fuata maelekezo, mimi nilikuwa ninafuatilia lishe nukashusha kama kilo 7 ndani ya mwezi, daaah ila konyagi na kitimoto sasa

IMG_0058.JPG
 
Dana ya kitambi ni stress. Hey jitafutie stress kidogo utaleta mrejesho.

Luna kipindi nilikuwa nakula moo Mona turn kwa siku lakini wapi.

Nikajapigwa na stress za kazini. Kitambi hicho kikaondoka.

God save us
 
Nimefanikiwa kupungua aise, nimepunguza kula ngano (chapati, maandazi na jamii za vyakula vya ngano), nimepunguza kula wali maharage hasa usiku.
niliacha kula mchana kwa muda wa wiki tatu nilikuwa Nikila usiku tu nimepunguza kg 3.
Kazini watu wananiuliza mbona nimepungua sana au naumwa! Haaaa haaaa haaaa kakitambi kamekata so kama unataka kupungua amua kujitesa kidogo utafanikiwa!).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiasilimia hapo No 1 ni menyu. Mimi ni mvivu wa mazoezi lakini kwenye menyu nina nidhamu sana. Sina kitambi. Nikiamua kupiga menyu bila kujizuia, mwezi hauishi, tumbo hilo linaning'inia...
80% ya uzito wako hutokana na vyakula unavyokula . 20% ni kutokufanya mazoezi ya viungo.

Ukitaka kufanikiwa panga discipline katika yote mawili.
 
Back
Top Bottom