Aliyedhamini Shindano la Kunywa Gongo Mtwara Asakwe

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,556
Mtu mmoja amefariki baada ya watu wanne kuingia katika shindando LA kumtafuta atakaeweza kumaliza mizinga minne ya gongo kwa mkupuo,yasemekana wawili waliishia raundi ya pili wakati wengine wawili walijribu wamalize lakini mmoja akaishia raundi ya tatu ambapo marehemu baada ya kumaliza mzunguko Wa mwisho alianguka na kufariki
Mwito kwa Serikali kuwasaka wote walioandaa na kudhamini mchezo huo mchafu ambao zawadi kwa mshindi ilikua ni Tsh 2000/- ,maana yasemekana kulikuwepo na refalii ambae alipuliza kipenga kuashiria kuanza kwa mpambano,Serikali ionyeshe ukali wake hata kwa MTU aliyepeleka hiyo Pesa Tsh 2000/eti ikanunue sanda!hii ni dhihaka kwa wafiwa na ikumbukwe si Mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea,nasikia Iliwahi tokeaga Korogwe pia shindano LA kunywa pilipili kichaa bakuli zima ulevini ambapo pia maisha ya MTU yakapotea,Ni bora sasa wanaoshabikia matukio haya wachukuliwe hatua Kali iwe onyo kwa wengine.
 
Utakuta aliye-bet ni huyo-huyo mshindi ambaye ni marehemu.
Aliyekufa vitani ndiyokauona mwisho wa vita.
 
"wamenipa nipaaaa"

wamekupa nini?"wamenipa nipaaaa'
 
So sad.
Lakini upande mwingine ni sifa za kijinga. Biashara hii ni haramu na gongo haijathibitishwa na tbs. Aliyepiga firimbi, aliyeuza, watatu walioshiri waliobaki na mdhamini wote wakamatwe
 
si mdhamini tu, hata walioshiriki shindano wanapaswa kuadhibiwa, hawa watu naona ni mzigo tu kwa taifa maana hakuna cha maana hapo zaidi ya ujinga, eti mtu unashindana kunywa gongo how comes!!!
 
You must be joking..
Kama una jamaa mtwara uliza,au hata Leo asubuhi ungesikiliza Wapo FM Kipindi cha Habari na matukio SAA 1:15 wametoa story hii baada ya kumaliza ile ya Akina Lema arusha
 
si mdhamini tu, hata walioshiriki shindano wanapaswa kuadhibiwa, hawa watu naona ni mzigo tu kwa taifa maana hakuna cha maana hapo zaidi ya ujinga, eti mtu unashindana kunywa gongo how comes!!!
Mshindi namba 2 ambae alifika fainali na marehemu yuko taabani hospitali nasikia alijaribu kunywa mikojo yake ili Ku neutralize haikusaidia
 
yani mi mpaka siwaelewi hao watu, sijui tatizo ni njaa tu mpaka waitamani hiyo 2000 au ukosefu wa akili, nadhani baada ya kukutwa na hayo majanga labda wengine watajifunza
 
Back
Top Bottom