Aliyedaiwa kufa kwa Ebola azikwa

Aliyedaiwa kufa kwa Ebola azikwa

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

ebola+tz.jpg

Wataalamu wa afya wilayani Sengerema mkoani Mwanza wakisimamia mazishi ya mgonjwa aliyedaiwa kufariki dunia kwa ugonjwa wenye dalili zinazofananishwa na ebola, juzi. Picha na Mpigapicha wetu.

Kwa ufupi
Alielezwa kuwa na homa kali, baadaye akaanza kutoa damu sehemu mbalimbali, vipimo vyasubiriwa kutoka wizarani

Sengerema
Mwili wa Salome Richard (17) aliyefariki dunia katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza akidaiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola ulizikwa juzi katika makaburi ya misheni mjini hapa chini ya uangalizi maalumu.

Mgonjwa huyo alifariki dunia Ijumaa saa 2 usiku baada ya kufika hospitalini hapo akiwa na homa kali. Vile vile madaktari waliokuwa wanatoa huduma kwa mgonjwa huyo wamewekwa kwenye chumba maalumu kwa ajili ya uangalizi wakati uongozi wa hospitali hiyo ukisubiri majibu ya sampuli kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Hata hivyo, uongozi wa hospitali hiyo ulisema hakuna mgonjwa aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa ebola na kwamba mgonjwa huyo aliyetoka katika eneo la Nyehunge, alikuwa akisumbuliwa na homa kali.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Mary Jose alisema Salome alifikishwa hospitalini hapo Ijumaa saa 4:30 asubuhi akiwa na homa kali.

Alisema muda mfupi baadaye alianza kutokwa na damu puani, mdomoni na sehemu ya haja kubwa, ndipo aliwekwa katika chumba maalumu kwa uangalizi wa madaktari watatu.

"Jana (Juzi) tulichukua sampuli na kuzipeleka Dar es Salaam Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa uchunguzi zaidi, lakini hatuwezi kusema kwamba ana ugonjwa wa ebola hadi majibu yatakapokuja, tuliamua kuchukua tahadhari. Tulimlaza kwenye chumba maalumu ili kumfanyia uchunguzi wa kina," alisema Dk Jose.

Wakati jana uongozi wa Wizara ya Afya haukupatikana kwa simu kuzungumzia ugonjwa huo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeahidi kutoa tamko leo kuhusiana na kifo hicho.

Mwezi uliopita mgonjwa mwenye dalili kama hizo aliwahi kupatikana katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, ambaye baada ya wiki moja alifariki dunia na majibu ya vipimo vyake yalionyesha kwamba alifariki kutokana na ugonjwa wa chikungunya.

CHANZO:
Mwananchi
 
Vipimo vimechelewa sana yaani sasa hivi tunahisi Ebola ipo kupitia nguo za hao wazikaji.
 
Hivi tanzania ninayoijuwa inaweza kuwa na vipimo vya ebola?
MUNGU utunusuru tu.
 
ebola+tz.jpg

Sengerema.
Mwili wa Salome Richard (17) aliyefariki dunia katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza akidaiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola ulizikwa juzi katika makaburi ya misheni mjini hapa chini ya uangalizi maalumu.

Mgonjwa huyo alifariki dunia Ijumaa saa 2 usiku baada ya kufika hospitalini hapo akiwa na homa kali. Vile vile madaktari waliokuwa wanatoa huduma kwa mgonjwa huyo wamewekwa kwenye chumba maalumu kwa ajili ya uangalizi wakati uongozi wa hospitali hiyo ukisubiri majibu ya sampuli kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Hata hivyo, uongozi wa hospitali hiyo ulisema hakuna mgonjwa aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa ebola na kwamba mgonjwa huyo aliyetoka katika eneo la Nyehunge, alikuwa akisumbuliwa na homa kali.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Mary Jose alisema Salome alifikishwa hospitalini hapo Ijumaa saa 4:30 asubuhi akiwa na homa kali.

Alisema muda mfupi baadaye alianza kutokwa na damu puani, mdomoni na sehemu ya haja kubwa, ndipo aliwekwa katika chumba maalumu kwa uangalizi wa madaktari watatu.

“Jana (Juzi) tulichukua sampuli na kuzipeleka Dar es Salaam Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa uchunguzi zaidi, lakini hatuwezi kusema kwamba ana ugonjwa wa ebola hadi majibu yatakapokuja, tuliamua kuchukua tahadhari. Tulimlaza kwenye chumba maalumu ili kumfanyia uchunguzi wa kina,” alisema Dk Jose.

Wakati jana uongozi wa Wizara ya Afya haukupatikana kwa simu kuzungumzia ugonjwa huo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeahidi kutoa tamko leo kuhusiana na kifo hicho.

Mwezi uliopita mgonjwa mwenye dalili kama hizo aliwahi kupatikana katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, ambaye baada ya wiki moja alifariki dunia na majibu ya vipimo vyake yalionyesha kwamba alifariki kutokana na ugonjwa wa chikungunya.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Asante kwa kununua
gezeti la mwanainchi,

umetuhabarisha vzr sana
 
Hivi ukichimba kaburi la mgonjwa wa ebora bila kujikinga na ww unaipata,hao wachimba kaburi walikua na ulazima gani wa kijikinga kiasi hicho wakati maiti bado imeifadhiwa.?au ndo mbwembwe za wabongo.?
 
Ni safi sana na ukijaliwa tena nunua tena dazete ili utupashi vizuri na hizo habari maana siku hizi hiyo bei ya gazeti ni sawa sawa na ugari mkavu kwa sisi wavimba macho
 
Rest in peace salome Richard. U died at an early age. Mungu awafarij na kuwapa nguvu familia ya marehem.
 
Hivi ukichimba kaburi la mgonjwa wa ebora bila kujikinga na ww unaipata,hao wachimba kaburi walikua na ulazima gani wa kijikinga kiasi hicho wakati maiti bado imeifadhiwa.?au ndo mbwembwe za wabongo.?
wabongo kwa misifa na kuiga tu yaan acha tu. Tunapenda kuiga sana. Mbwembwe kibao na wakat deni la taifa linazid kupaa. Kwa ufup 2 nchi yetu imejeaa na kushehen maamuma waliokubuhu. Nyambaff zetu!!!
 
Ni safi sana na ukijaliwa tena nunua tena dazete ili utupashi vizuri na hizo habari maana siku hizi hiyo bei ya gazeti ni sawa sawa na ugari mkavu kwa sisi wavimba macho

Kwani linauzwa shilingi ngapi? maana sijasoma magazeti mda.
 
Back
Top Bottom