Aliyebaka mjamzito Aachiwa Huru, aliyebakwa Abaki Selo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyebaka mjamzito Aachiwa Huru, aliyebakwa Abaki Selo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, May 29, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIKA hali ya kushangaza imetokea juzi katika maeneo ya Boko baada ya babu mmoja kutuhumiwa kuwa amebaka mama mjamzito kuachiwa huru na polisi na mama huyo kubaki kushikiliwa na polisi.

  Tukio hilo la kusikitisha lilitokea juzi huko Boko katika Kituo cha polisi cha WazoHill baada ya wakazi wa eneo hilo kushangazwa na hatua iliyochukuliwa polisi wa kituo hicho.

  Mwanamke mjamzito mmoja [jina kapuni] alibakwa na babu mmoja na baada ya kupeleka taarifa hiyo polisi kuomba msaada kutokana na kitendo hicho alichofanyiwa cha kubakwa na mtu ambaye anamfahamu hali ilibadilika baada ya mtuhumiwa kufikishwa kituoni hapo kuachiwa na mama huyo mjamzito kushikiliwa na polisi.

  Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo la ubakaji walisema kuwa walifika eneo la tukio baada ya kusikia mama huyo anaomba msaada wa kuomba asidiwe ndipo walipofika na kumkamata mtuhumiwa.

  Walisema kuwa kutokana na kitendo hicho alichofanya babu huyo waliamua kutoa taarifa katika kituo cha polisi na mzee huyo kuja kuchukuliwa na polisi.

  Na mashuhuda hao wakiendelea kushuhudia na hadi mtuhumiwa huyo alipofikishwa kituoni na kujua nini kitatokea baada ya kufikishwa polisi kwa babu huyo.

  Katika hali iliyowashangaza waliowengi mahali hapo waliona babu huyo ameachiwa huru na polisi na kumshikilia mama aliyebakwa jambo ambalo hawakulielewa.

  Wakazi hao walianzisha vurugu kubwa kituoni kutaka mama huyo aachiwe na kuimba nyimbo na kutaka kuandama kutokana na kitendo hicho cha polisi cha kumshikilia mama huyo na kumuachia mbakaji.

  Mmoja wa aliyeshuhudia tukio hilo la ubakaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Saidi akiongea na Nifahamishe alisema kuwa babu huyo alifika kwa mama huyo na kuanza kumtukana na kisha kumfanyia fujo na kumbaka.

  Alisema mama huyo alikuwa akiishi peke yake na wakati akipiga makelele kuomba msaada walifika na kukuta babu huyo amemng’ang’ania mama huyo bila aibu.

  “Tunashangaa kuona polisi wamemuachia mtuhumiwa kwa kigezo kipi na sisi wenyewe tulishuhudia, huu ni uonevu”

  Akiongea kwa shida mama huyo alisema babu huyo alifika nyumbani kwake na kuanza kumtolea maneno machafu ndipo baadae alipochukua uamuzi wa kuniangusha chini na kuanza kunibaka .

  “Nilishindwa kujitetea kutoka pale chini kutokana na hali yangu hii ya ujauzito ndipo nilipopiga kelele watu wakaja kuniokoa” alisema

  Amesema walipofika polisi hapo kutoa maelezo katika kituo hicho cha Wazo alishangaa mtuhumiwa ameachiwa huru na yeye kuambiwa kuwa abaki kwa ajili ya mahojiano zaidi.

  Hata hivyo wakazi hao walionekana kuulalamikia uongozi na askari wa kituo hicho cha Wazo hill kwa kuwanyanyasa wananchi wa hali ya chini.

  Walisema kuwa askari wa kituo hicho huwa wanaangalia watu wenye uwezo na wasiokuwa nazo huwa hawasaidiwi.

  Source: http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2119838&&Cat=1
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MARA NYINGI KESI KAMA HIZI ZIMEJAA UTATA WA UBAMBIKIWAJI....!
  HUENDA JAMAA ALISTUKIA NA KUWAHI KUTOA TAARIFA KITUONI KITU AMBACHO KILIMUOKOA NA AIBU YA KUBAMBIKIWA.....!
  you cana find the lady aliwahi tamka.......mimi lazima nikulaze selo kwa kosa lolote.....halafu ikaja tokea jamaa anakatiza mama anapiga kelele na kujaza watu...the story goes kwa jamaa kufikishwa polisi.....bahati nzzuri tayari taarifa za kitu kama hicho zipo kituoni....!
  BILIV MI JAMAA LAZIMA AACHIWE NA MAMA ASHIKILIWE KWA MAHOJIANO ZAIDI.
  DEDICATION KWA WALE WOTE TULIOWAHI KUBAMBIKIWA...!
   
Loading...