Aliyebaka akatoroka jela arudishwa miaka 30

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,400
Siha. Mahakama ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanajaro, imemhukumu Goodluck Lazaro (23) maarufu babuu mkazi wa kijiji cha Merali kutumikia kifungo cha 30 jela kwa kosa la ubakaji.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu Jasmine Abdul baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi watano akiwamo daktari, mwanamke aliyebakwa na mwenyekiti wa kijiji hicho.

Hakimu Jasmine alisema ushahidi huo haukuacha shaka ndani yake na Mahakama imemtia hatiani kwa kosa hilo.

Awali, mwendesha mashtaka wa Serikali, Simon Feo alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 4 saa 10:00 jioni kijijini hapo kwa baada ya kutoroka gereza la Karanga Moshi.

Feo alidai mshtakiwa wakati anarudi kijiji kwao akiwa njiani alikutana na mwanamke na kumkamata kwa nguvu kisha kumburuza kwenye Pori la Kwanduli na kumuingilia bila ridhaa yake.

Aliendelea kuwa mshtakiwa alihukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kosa la wizi kesi namba 164/ 2018 na Mahakama ya Mwanzo Sanya juu Aprili 4 na ilitegemewa kumaliza kifungo chake Agosti 7, lakini siku tatu kabla ya kumaliza kifungo alipotoroka gerezani.

Huyo mshtakiwa alibakiza siku chache kumaliza kifugo chake lakini akatoroka gerezani alipokuwa anarudi kijijini kwao akakutana na huyo mwanamke na kumbaka.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashtaka aliomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa kutokana na usugu wake na amefikia hatua ya kutoroka kifungoni.

Chanzo: Mwananchi
 
kweli jamaa kauzu sana huyo.... aiseee...AMETOROKA, AKAUTANA NA MWANAMKE AKAMBAKA.....
 
Hakuna mtu humo. Wangempeleka mirembe kupimwa.

Unatorokaje gerezani sababu bado siku 3?

Ila nadhani kilichomtorosha ni genye. Ama kweli wanaume wanaendeshwa na kichwa kidogo nimeamini. Kamanda kashindwa kabisa kufanya maamuzi ya busara sababu ya kichwa kidogo kimechachamaa. Na ndio maana njia nzima anaangalia wa kukituliza tu hadi masikini katokea mama wa watu.

Ngoja sasa akaone kama inawezekana kuishi maisha yote bila matumizi ya kichwa kidogo
 
Siha. Mahakama ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanajaro, imemhukumu Goodluck Lazaro (23) maarufu babuu mkazi wa kijiji cha Merali kutumikia kifungo cha 30 jela kwa kosa la ubakaji.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu Jasmine Abdul baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi watano akiwamo daktari, mwanamke aliyebakwa na mwenyekiti wa kijiji hicho.

Hakimu Jasmine alisema ushahidi huo haukuacha shaka ndani yake na Mahakama imemtia hatiani kwa kosa hilo.

Awali, mwendesha mashtaka wa Serikali, Simon Feo alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 4 saa 10:00 jioni kijijini hapo kwa baada ya kutoroka gereza la Karanga Moshi.

Feo alidai mshtakiwa wakati anarudi kijiji kwao akiwa njiani alikutana na mwanamke na kumkamata kwa nguvu kisha kumburuza kwenye Pori la Kwanduli na kumuingilia bila ridhaa yake.

Aliendelea kuwa mshtakiwa alihukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kosa la wizi kesi namba 164/ 2018 na Mahakama ya Mwanzo Sanya juu Aprili 4 na ilitegemewa kumaliza kifungo chake Agosti 7, lakini siku tatu kabla ya kumaliza kifungo alipotoroka gerezani.

Huyo mshtakiwa alibakiza siku chache kumaliza kifugo chake lakini akatoroka gerezani alipokuwa anarudi kijijini kwao akakutana na huyo mwanamke na kumbaka.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashtaka aliomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa kutokana na usugu wake na amefikia hatua ya kutoroka kifungoni.

Chanzo: Mwananchi

Duh,jamaa alikuwa na ngale balaa
 
Aisee pale Karanga ukitoroka ukirudishwa unakula kichapo hatari Sana... Yaani inshort kijana ajipange physical and psychologically
 
Atakuwa na upungufu wa akili.
Maana haiwezekani umebakiza Siku 3 kuwa huru alafu unatoroka na baadae kubaka.
Waangalie na background yake tatizo ni nini hasa?
Anyway kwa kuwa hukumu tayari tuache kama ilivyo,lakini kama itaonekana inafaa wafanzie kazi maoni yetu kama yapo yanayowafaa.
 
Yaani amebakiza Siku chache amalize kifungo akatoroka halafu njiani anakutana na mwanamke anambaka.

Huyu ana matatizo makubwa sana

Hivi kweli nyie wote mnaoshangaa hamjui kuwa kuna watu wanaona kuwa Jela maisha ni raha kuliko kuishi uraiani? nendeni mkaongee na askari magereza mtapata story za hao watu mwanzo mwisho.
 
Bangi nini? Umebakiza siku 3 kumalizia kifungo chako unatoroka? Au zilimbana akashindwa kuvumilia.
 
Back
Top Bottom