Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,652
- 13,393
Mahakama ya Wilaya ya Missenyi imemhukumu, Florian Kaizilege Method, adhabu ya kifungo cha miaka mitatu Jela.
Adhabu hiyo imetolewa baada ya kuthibitika kosa la Rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Mshtakiwa kwa makusudi alijipatia manufaa isivyostahili kiasi cha Shs.1,625,000/- alizozikusanya kutoka kwa Wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Bwenkoma wilayani Missenyi.
Aidha, Mahakama imeamuru mshtakiwa arejeshe fedha zote Shs. 1,625,000 kwa mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa taratibu za ujenzi Ofisi ya Kijiji - Bwenkoma.
Hukumu dhidi ya Florian Kaizelege Method imeamriwa katika shauri la Rushwa Na. 21076/2024 - Julai 26, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Missenyi Mh. Yohana Muyombo mbele ya waendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Daudi Jacob Oringa na Sospeter Joseph.
Mshtakiwa ameenda Gerezani kutumikia Kifungo cha miaka mitatu