Aliyeandika hapa alimaanisha nini?

prickle

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
293
427
Aliyeandika hapa alikuwa na maana gani?

screenshot_2017-02-18-15-23-03-jpg.471726
 
Pengine amemaanisha kua sekta nzima ya mapato na kodi hapa nchini imegubikwa na visasi kati ya TRA na Wafanyabiashara,
Na ndio maana kila kukicha hua wanafungianaga maduka.
 
huenda ikawa alimaanisha kiukwelii!... haya makodi yasiyoeleweka, makadirio makuuubwa kwa vibiashara vidooogooo!... bidhaa zinakatwa kodi zaidi ya mara moja... ikiingizwa, ikisambazwa, ikiuzwa maduka ya jumla, ikiuzwa maduka ya rejareja... hadi mwisho ni limbikizo la kodi kibao lazima wa mwisho abebe!... ni kama wanawakomoa au kisasi kwa wafanyabiashara na walaji wa mwisho!... Nampongeza ameliona hilo na kuandika revenge!... Aendelee na kuvibadili vibao vingine vilivyobakia!...
 
Jaman hat kiongoz hata naye ongoza taasisi hii hajona kweli
 
Aliyeandika hapa alikuwa na maana gani?

screenshot_2017-02-18-15-23-03-jpg.471726
Ngoja nikupe scenario ya hii kitu.Hapa kuna watu wawili: aliyeagiza bango liandikwe(afisa wa tra obviously) na mwandika bango(signwriter).Masignwriter wengi kiingereza kipo kushoto na maafisa wetu wengi hati zao za mwandiko si nzuri.Signwriter kapewa kikaratasi kilichocharazwa kwa hati ya mkono: tanzania revenue authority. Hati ya afisa haisomeki vizuri, signwriter ameona herufi nne za mwanzo za neno revenue ila herufi ya tano na sita kwake inasomeka 'n' na 'g'. Kwa hiyo anaandika revenge badala ya revenue.
Na wakati wa kuchukua bango afisa anatuma kijana wa masjala kwenda kulichukua na kulichimbia ie hakuna kukagua final work.
Kwa maneno mengine kilichotokea hapa ni UZEMBE wa hali ya juu! Jambo hili la uzembe ni kansa kubwa kwenye ofisi zetu: mgonjwa anapasuliwa kichwa badala ya goti, mfanyakazi kuhamishiwa kibondo na mshahara wake kwenda kilosa nk nk.
 
Kosa kubwa zaidi ni bango hilo kukaa hapo muda mrefu, uchakavu wa bango unaonyesha hivyo. Ni dhahiri kuwa maafisa wa TRA wameshapita kwenye hilo bango mara kadhaa. Elimu hoyeee
 
sasa Huyo alieandika hakusoma elimu bure yupo hivi je hawa watt wetu huko shule na elimu bure sindo wanakuja kutuandikia upumbavu zaidi ya huo
 
Ngoja nikupe scenario ya hii kitu.Hapa kuna watu wawili: aliyeagiza bango liandikwe(afisa wa tra obviously) na mwandika bango(signwriter).Masignwriter wengi kiingereza kipo kushoto na maafisa wetu wengi hati zao za mwandiko si nzuri.Signwriter kapewa kikaratasi kilichocharazwa kwa hati ya mkono: tanzania revenue authority. Hati ya afisa haisomeki vizuri, signwriter ameona herufi nne za mwanzo za neno revenue ila herufi ya tano na sita kwake inasomeka 'n' na 'g'. Kwa hiyo anaandika revenge badala ya revenue.
Na wakati wa kuchukua bango afisa anatuma kijana wa masjala kwenda kulichukua na kulichimbia ie hakuna kukagua final work.
Kwa maneno mengine kilichotokea hapa ni UZEMBE wa hali ya juu! Jambo hili la uzembe ni kansa kubwa kwenye ofisi zetu: mgonjwa anapasuliwa kichwa badala ya goti, mfanyakazi kuhamishiwa kibondo na mshahara wake kwenda kilosa nk nk.
Hata sijui huyo aliyepeleka maneno kwa mwandika bango ni afisa wa TRA kweli maana hata jina la ofisi hiyo kwa kiswahili halijui zaidi ya hapo bango hilo linaonekana limewekwa hapo siku nyingi hivi kwa wakazi wote wa Urambo na hata waliotembelea ofisi hiyo hawajaona kosa hilo wakiwemo maafisa wa Mkoa wa ofisi hiyo
 
Nimekuelewa kaka ila katika nchi hii kuna mentality ya 'inanihusu nini hiyo?' Afisa wa tra wa mkoa anakatiza mtaa kwa haraka kwenda kwa mchepuko wake saa ngapi atasimama kuangalia eti revenue imeandikwa 'revenge' kwa hiyo bango ling'olewe na kusahihishwa! No time my dear.
 
Back
Top Bottom